Kuelekea Maadhimisho ya IDUAI 2026: Unapataje Taarifa Sahihi katika enzi hizi za Kidijitali?

Kuelekea Maadhimisho ya IDUAI 2026: Unapataje Taarifa Sahihi katika enzi hizi za Kidijitali?

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,249
Reaction score
5,747
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa kwa Wote (IDUAI) hufanyika Septemba 28 ya kila mwaka, ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni “Kulinda Uadilifu wa Taarifa katika Enzi ya Kidijitali: Nafasi ya Upatikanaji wa Habari katika Kukabiliana na Upotoshaji wa Taarifa,” yakilenga kuhamasisha wananchi kutafuta, kuhakiki na kutumia taarifa kwa uwajibikaji.

Pia, yanalenga kujadili changamoto za taarifa potofu katika zama za kidijitali, pamoja na umuhimu wa Wananchi kuhakiki taarifa kabla ya kuzisambaza.

Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) unaadhimisha Kimataifa siku hii, kwa lengo la kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kupata taarifa sahihi, za kuaminika na kwa wakati.

Aidha, Takribani Wadau kutoka serikalini, Asasi za Kiraia, Vyombo vya Habari, Wasomi, Taasisi za Teknolojia na Haki za Kidijitali pamoja na vijana wanatarajiwa kushiriki katika majadiliano hayo.

Wewe Mdau unapataje taarifa sahihi nyakati hizi za Kidigitali?
 
1. AI na
2. Reputable sources' Social Media

Situmii TV za Kitanzania, sitaki kabisa, kwahiyo sources kubwa ni social media, sema natumia AI Kuverify.

Nyie JF mnapataje, tuanze na Admin mkuu.
 
Tetesi KABLA ya kuwa breaking niuz huwa naangalia kwanza jamiiforums. Atleast j f naweza kupata au AI
 
Katika ulimwengu wa sasa unaotawaliwa zaidi na teknolojia ya kidijitali, upatikanaji wa taarifa umekuwa rahisi zaidi kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari (mainstream media).
Hata hivyo, kutokana na ukuaji wa teknolojia na kuongezeka kwa matumizi ya mitandao ya kijamii, majukwaa haya yamechukua nafasi kubwa katika namna watu wanavyopata na kusambaza taarifa.

Kasi ya usambazaji wa taarifa kupitia mitandao ya kijamii imefanya watu wengi kuanza kuyatumia kama chanzo cha kwanza cha habari.
Licha ya ukuaji huo changamoto mtawaliwa ni ongezeko la taarifa zisizo sahihi ambazo huwafikia watumiaji wa mitandao ya kijamii regardless of umri wao, jinsia, na kadhalika

Katika moja ya njia ambazo zinatumiwa zaidi kupata taarifa ni
01.Vyombo vya habari(Mainstream media)
02.kurasa za mitandao ya kijamii za watu mashuhuri Duniani
03.mitandao ya kijamii instagram, facebook and twitter
04.Magazeti sambamba na ripoti kutoka taaasisi zinazo aminika
05.Mawasiliano ya moja kwa moja kutoka kwa mashuhuda au mtu wa karibu na chanzo cha habari
 
Back
Top Bottom