SoC03 Kuelekea mapinduzi ya kifikra kwa kila muafrika

SoC03 Kuelekea mapinduzi ya kifikra kwa kila muafrika

Stories of Change - 2023 Competition

madbadizo

New Member
Joined
Jun 23, 2023
Posts
1
Reaction score
1
Moja ya mambo muhimu tunayopaswa kuyafahamu kwa kila Muafrika haswa nchi zinazotaka kujitoa katika dimbwi la umasikini, ni lazima lizingatie umuhimu wa kuwaamsha kifkra vijana ili kuwaza zaidi kujikwamua kiuchumi.

Vijana wengi wa Kiafrika tumekuwa na ushawishi mdogo katika maswala ya kiteknolojia, hili linatokana na serikali zenu kushindwa kuwapa kipaumbele vijana kuhusu Teknolojia ambazo ndio msingi wa kujikwamua katika dimbwi la umasikini kwenye dunia ya leo na ya kesho.

Inashangaza kuona nchi kama Tanzania ina vyuo vikuu ambavyo vinatoa wasomi wenye stashahada za vyeti kichwani na sio ubunifu binafsi wa kuvumbuwa vitu ambazo vitakuwa suluhu katika kuinua nchi.

Mfano , Nchi yetu inatoa tenda kwa nchi zingine katika utengenezaji wa barabaea, madaraja, umeme n.k lakini cha kustaajabisha wakaguzi ni wazawa tena waswahili nddo wanaokuja kupima ubora wa mradi.

Swali kama wazawa ndo wakaguzu hamuoni haja ya kuwekeza katika teknolojia ili na sisi tukawa na viwanda vyenye uwezo wa kudhalisha mitambo ya kisasa kwajili ya miradi yetu..?

Iko haja ya kubadili mifumo ya elimu yetu na kuacha kuekeza zaidi kwenye taaluma za makaratasi na kuelekeza zaidi vitendo.

Serikali iwape vipaumbele watu wenye vipaji ili wazitumie katika kuinua teknolojia yetu. Nitoe mfano , mtaani kuna vijana ni wameweza kuunda ,mashine inayochakata mabaki ya karatasi na zikawa mkaa mzuri.

Je, kama serikali ikaamua leo kujenga vyuo ambavyo vitakuwa ni vya vijana wabuni na kufufua viwanda baada ya vijana hawa kupata elimu zaidi na kuja kufanya kazi katika viwanda huoni tutaongeza pato la kijana na Taifa.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom