Kuelekea mchezo wa starz vs Tunisia usiku huu tuitafakari Commoros

Kuelekea mchezo wa starz vs Tunisia usiku huu tuitafakari Commoros

mugah di matheo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
6,307
Reaction score
12,410
Commoros ni visiwa vilivyojirani sana na nchi yetu lakini kwa miaka mingi walionekana mpira sio fani yao kabisa. Ambapo vilabu vyao kufungwa 8,7,6,5 na simba,Yanga hata na Mtibwa nilikuwa jambo la kawaida.

Timu yao ya taifa ilikosa hata friendly match kutokana na ubovu wao. Ila leo wanahitaji point moja tu kwenye mechi mbili na hiyo endapo Kenya itashinda mechi zote mbili ikiwemo Kenya kuifunga misri.

Kiufupi nchi iliokuwa haipewi hata mwaliko wa mapinduzi cup imefuzu afcon mapema sana.

Nini wao wanafanikiwa sisi tunakishindwa?

Pia hata kesi ya Gambia
 
Unawazungumzia Gambia hawa hawa waliowalaza wachezaji wa Gabon airport bila ya kupokeelewa?
FB_IMG_1605593629181.jpg
 
Hatuna mipango, tumekalia ulaji.

Hivi ni kigezo gani kimetumika kumteua Milambo kuwa mkurugenzi wa ufundi, kigezo gani kimetumika kumchagua julio kocha wa vijana, kigezo gani kimetumika kumchagua Kidau kuwa katibu mkuu TFF.

Nafasi zote ni za kutangazwa na watu kuomba lakini kwa sababu ya ushikaji wamekaa wanapeana nafasi na hizo ndio nafasi nyeti kwa maendeleo ya soka.

Kama tutatengana na Zanzibar baada ya miaka mitatu hatutawafikia kisoka.
 
Hatuna mipango, tumekalia ulaji. Hivi ni kigezo gani kimetumika kumteua Milambo kuwa mkurugenzi wa ufundi, kigezo gani kimetumika kumchagua julio kocha wa vijana, kigezo gani kimetumika kumchagua Kidau kuwa katibu mkuu TFF...
Shida ni Tff tu au hata vilabu vyetu?
 
Sifa ya mbongo ni mjuvi wa mambo yote!!!. Ni mkosoaji na asiye penda cha kwake ila vya wenzake, ni mtu wa mitazamo hasi hajui kufikiri chanya, anapenda wengine wa feli ili apate ajenda ya kuongea kwan tabia yake ni kuongea tena Yale yaliyo mabaya. NA HUYU NDIO MBONGO!
 
Watu mnalaumu bure tu...
Commoro bado hakuna mpira, wapo vile vile( ligi yao).
Kilichotokea wamewachukua wachezaji wote wenye asili ya huko na kuwapa uraia.
Tanzania hilo swala haliwezekani, wamegoma kutoa uraia pacha.
Ila wachezaji huko nje ni wengi tu.
 
HiV

Hivyo hapa kinachotukwamisha ni Sera yetu ya uraia?
 
Michango mingi hapa ni ya kujenga kuliko nyuzi nyingine hukuta uzi umejaa malalamiko kifupi TFF na vilabu khasa hivi vikubwa vinahusika hapa miaka ya nyuma yanga ilikuwa na kikosi cha black stars ambacho baade kilitoa nyota wengi kina pondamali akina Adolf rishard na wengine wengi na hata miaka ya tisini yanga hiyo hiyo ilifumua kikosi chake na kuweka damu changa za akina anuary awadhy slivanus polisi akina maalim swaleh romario na wengine wengi. TFF kama mzazi wa soka ana jukumu kubwa la kuhakikisha kutoa maelekezo na ufuatiliaji wa soka ya vijana kama ilivyokuwa cocacola cup au uhai aaagh sijui nini kilitokea hivi nilikuwa naandika nini? nitarudi baaden.
 
Hatuna mipango, tumekalia ulaji .
Hivi ni kigezo gani kimetumika kumteua Milambo kuwa mkurugenzi wa ufundi, kigezo gani kimetumika kumchagua julio kocha wa vijana, kigezo gani kimetumika kumchagua Kidau kuwa katibu mkuu TFF.
Nafasi zote ni za kutangazwa na watu kuomba lakini kwa sababu ya ushikaji wamekaa wanapeana nafasi na hizo ndio nafasi nyeti kwa maendeleo ya soka.
Kama tutatengana na Zanzibar baada ya miaka mitatu hatutawafikia kisoka.
Sie siasa nyingi na kudanganyana kwenye magazeti oh pira biriani or pira mpapaso...wakati wanojua kupapasa mpira jana tumewaona. Calm kn the ball hamna papara yoyote.
 
Commoros ni visiwa vilivyojirani sana na nchi yetu lakini kwa miaka mingi walionekana mpira sio fani yao kabisa.
Ambapo vilabu vyao kufungwa 8,7,6,5 na simba,Yanga hata na Mtibwa nilikuwa jambo la kawaida.
Timu yao ya taifa ilikosa hata friendly match kutokana na ubovu wao.
Ila leo wanahitaji point moja tu kwenye mechi mbili na hiyo endapo Kenya itashinda mechi zote mbili ikiwemo Kenya kuifunga misri.
Kiufupi nchi iliokuwa haipewi hata mwaliko wa mapinduzi cup imefuzu afcon mapema sana.
Nini wao wanafanikiwa sisi tunakishindwa?

Pia hata kesi ya Gambia
Its a disgrace kabisaaa....yaani nchi ya watu less than a million wanaenda afcon sie tunaendeleza siasa za kijinga.
 
Back
Top Bottom