Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars leo kinaingia Uwanjani kuwakabili timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars katika mfululizo wa michuano ya fainali ya mataifa ya Afrika AFCON2019, utakaopigwa leo Juni 27, 2019 saa 5:00 majira ya usiku Cairo, Misri.
Taifa Stars imetamba kucheza kufa na kupona ili kuweza kushinda mchezo huo wa kundi C na kuweza kufuzu hatua inayofuata huku Rais wa TFF Wallace Karia akiwatia moyo wale ambao wamekata tamaa baada ya Taifa Stars kufungwa na Senegal.
Kocha wa Taifa Stars Emmanuel Amunike, amesema anatambua umuhimu wa mchezo huo, huku akiongeza kuwa lazima ashinde ili matumaini yao ya kusonga mbele yasalie hai.
Harambee Stars wamekiri mchezo si rahisi mchezo itakuwa ngumu, lakini wametaja kuwa mchezo wao dhidi ya Taifa Stars kuwa ni fainali kwao ambayo inawapa fursa ya kipekee kushinda.
Kocha wa Harambee Stars, Sebastien Migne, amesema kwamba kupoteza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Algeria iliiweka timu yake pabaya hivyo amewataka vijana wake kuonyesha ukatili wao dimbani kwenye mechi na Taifa Stars.
••••Je? Wajeruhiwa Wawili wa Mechi Zao za Ufunguzi wa Michuano ya AFCON2019..Nchi gani Kung'ara? Tanzania ama Kenya?