Kuelekea mechi ya CAFCL, Kocha: Tunaanza kesho kupambana tunajua Nchi na Simba nini wanataka

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Kocha Mkuu wa Simba SC Juma Mgunda, amezungumza na waandishi wa vyombo vya habari nchini Malawi kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL, dhidi ya Nyasa Big Bullets ya nchini Malawi, huku akitanabaisha kuwa wanaanza kupambana kuanzia kesho kwasababu wanajua klabu ya Simba hitajio lao na nchi ya Tanzania kwa ujumla.

"Tunaanza kesho kupambana, tunajua nchi inataka nini na Simba inataka nini, kubwa kwetu ni kutimiza wajibu wetu."

"Nimewaona wapinzani wetu, nimeangalia baadhi ya video zao, ni timu ambayo sio ya kubeza, wanacheza kitimu na wanacheza nyumbani, tahadhari zote tutachukua".

"Ukishakubali kuvaa gwanda wewe ni mwanajeshi, naamini Vijana baada ya kuzungumza nao wanaelewa majukumu yao, naamini kesho watajitoa kwa ajili ya Simba SC".
Kocha Mkuu Juma Mgunda
 
Kwetu sisi mashabiki wa ukweli ambao si mashabiki papatu papatu, mashabiki wenye kujielewa wanaoshabikia timu kwa wakati wa shida na raha.

Timu yenye viwango vya CAF kwa nafasi ya 12 CAF kwa ubora

Timu yenye kutandaza Kabumbu maridhawa

Timu yenye kuteka hisia za mashabiki wa soka

Timu yenye kuvuta hadhira mujarabu

... Hitajio letu Wanamsimbazi ni ushindi tu, kila la heri Mnyama Mkali Mwituni Simba SC...
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…