Kuelekea mechi ya Kesho; Mnyama ana haya ya kuwajuza wa pili

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Baada ya timu ya Yanga S.C kuwapiga stop wachezaji, viongozi na hata mashabiki kuzungumza chochote kuhusu mechi ijayo dhidi ya Simba S.C hapo kesho Taifa Stadium... zifuatazo ni kauli za baadhi ya viongozi, makocha, wachezaji n.k.

“Lengo langu ni kuhakikisha navunja rekodi ya Kibaden ya hat trick, pia kufikia idadi ya mabao mengi kwa mechi za watani inayoshikiliwa na Omar Hussein" ~ Le Kapiteni, Mussa Hassan Mgosi.

“Nikiiangalia Yanga na nikiiangalia Simba ninaona tofauti kubwa, achilia mbali kuwa mimi niko Simba bali uwezo wa kukimbia kwa muda mrefu kwa wachezaji wa Simba ni mkubwa ukilinganisha na Yanga na taswira yake ni kuwa kuna dalili kuwa Simba watatawala mchezo zaidi" ~ Kocha bora wa viungo toka Serbia, Momcilovic.

“Nataka kumfunga Yanga Jumamosi, sioni sababu kws nini tushindwe kumfunga. Nina wachezaji wazuri na wote wako na afya njema kimwili na kiakili, hivyo sina wasiwasi" ~ Kocha mwenye leseni A ya kufundisha toka UEFA, Dylan Kerr.

“Kwa upande wangu nimejipanga na namjua Kamusoko vizuri hivyo basi nina uhakika nitamshinda na kuishinda timu yake pia, kwa maandalizi tuliyoyafanya tunatarajia kupata ushindi wa aina yoyote ule na siwezi kutoa ahadi kwamba la tutawafunga mabao fulani kwani ushindi ni ushindi tu, muhimu pointi tatu," ~ Kiungo bora kwa sasa katika VPL, Justice Majabvi.

“Maandalizi mengine yanaendelea kama kawaida na kila kitu kinakwenda vizuri. Hapa lengo ni kuwapa ndugu zetu hawa supu ya miiba.” ~ Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Pope.

“Wanakutana na wafalme wao ndiyo maana wameamua kukaa kimya. Watakaa kimya sana na hawatakuwa na nafasi ya kuzungumza tena. Watakuwa na kipi cha kuzungumza wakati watakuwa wamefungwa. Acha waendelee kukaa kimya,” ~ Haji Manara.

NB: Jamhuri Julio alishawahi kunena haya...

"Yanga S.C ni sawa na mti wa maembe uliopo uwani katika nyumba yako.. ukijisikia hamu ya kula embe, unachuma tu, na kukata kiu yako"

... nami sembo naamini kesho tunaenda kujichumia maembe yetu ya kutosha.
 
Laiti maneno yangekuwa yanacheza ..................
 
Habari yako mkuu,natumai umeamka poa ila nakukumbusha baada ya mechi kuisha uyarudie maneno yako haya maana huwa uchelewi kuleta visingizio
 
Yanga kipigo kama kawaida. Tukutane hapa baadae.
 
Simba pumzi shida, huo uwezo wa kumbia muda mrefu mmeutoa wapi? Sisi tu kimya, yetu macho
 
Habari yako mkuu,natumai umeamka poa ila nakukumbusha baada ya mechi kuisha uyarudie maneno yako haya maana huwa uchelewi kuleta visingizio

Mkuu leo ushindi ni lazima.. Usiwe na hofu, tupo pamoja.
 
Simba pumzi shida, huo uwezo wa kumbia muda mrefu mmeutoa wapi? Sisi tu kimya, yetu macho

Naona Mkuu unabishana na kocha bora kabisa wa utimilifu wa mwili kuwahi kutokea ulaya ya mashariki.. Mtalamu Momclovic... Alafu nadhani unaizungumzia Simba S.C ya msimu uliopita.
 
Laiti maneno yangekuwa yanacheza ..................

Mkuu tunaposema tunashinda ndani na nje ya uwanja tunamaanisha uwanjani tutawapiga goli za kutosha, na ushindi wa nje ya uwanja ndo kama huu.
 
Yanga italizwa kwa mara nyingine tena

Nimejiuliza mara kibao tu, hivi leo Yanga ataweza vipi kushinda, nimekosa kabisa jibu.. Na saa 10 ifike mapema.
 
Mkuu unanifanya nifurahi kupita maelezo maana leo Simba kufungwa ni lazima

Mkuu tukutane baada ya mechi, ambapo furahi yako Kiiza atakua kashaigeuza kua kilio.
 
Mkuu tukutane baada ya mechi, ambapo furahi yako Kiiza atakua kashaigeuza kua kilio.

Teh teh uyo kiiza wala hanitishi ukweli namwofia mgosi ila uyo babu wala hapati kitu maana huna beki wa kumzuia busungu kubali mtani
 
Teh teh uyo kiiza wala hanitishi ukweli namwofia mgosi ila uyo babu wala hapati kitu maana huna beki wa kumzuia busungu kubali mtani

Sasa kama humuogopi Mchezaji anayeongoza kwa kufunga magoli katika ligi.. Sijui utamuogopa nani sasa?
Ila uzuri tunapokutana, kila mchezaji hua mfungaji.. mf. gallas, awadh juma... na hata makipa hua wanafunga, mf. kaseja.. hivyo sina hofu kabisa.
 
Hahaha bado masaa nane kuanza iyo game,nitakua taifa mkuu sijui ww????
 
Hahaha bado masaa nane kuanza iyo game,nitakua taifa mkuu sijui ww????

Mkuu tangu siku ya jana nimesimamisha shughuli zote.. Hapa namalizia kujiandaa ili nisogee eneo husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…