sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
Baada ya timu ya Yanga S.C kuwapiga stop wachezaji, viongozi na hata mashabiki kuzungumza chochote kuhusu mechi ijayo dhidi ya Simba S.C hapo kesho Taifa Stadium... zifuatazo ni kauli za baadhi ya viongozi, makocha, wachezaji n.k.
Lengo langu ni kuhakikisha navunja rekodi ya Kibaden ya hat trick, pia kufikia idadi ya mabao mengi kwa mechi za watani inayoshikiliwa na Omar Hussein" ~ Le Kapiteni, Mussa Hassan Mgosi.
Nikiiangalia Yanga na nikiiangalia Simba ninaona tofauti kubwa, achilia mbali kuwa mimi niko Simba bali uwezo wa kukimbia kwa muda mrefu kwa wachezaji wa Simba ni mkubwa ukilinganisha na Yanga na taswira yake ni kuwa kuna dalili kuwa Simba watatawala mchezo zaidi" ~ Kocha bora wa viungo toka Serbia, Momcilovic.
Nataka kumfunga Yanga Jumamosi, sioni sababu kws nini tushindwe kumfunga. Nina wachezaji wazuri na wote wako na afya njema kimwili na kiakili, hivyo sina wasiwasi" ~ Kocha mwenye leseni A ya kufundisha toka UEFA, Dylan Kerr.
Kwa upande wangu nimejipanga na namjua Kamusoko vizuri hivyo basi nina uhakika nitamshinda na kuishinda timu yake pia, kwa maandalizi tuliyoyafanya tunatarajia kupata ushindi wa aina yoyote ule na siwezi kutoa ahadi kwamba la tutawafunga mabao fulani kwani ushindi ni ushindi tu, muhimu pointi tatu," ~ Kiungo bora kwa sasa katika VPL, Justice Majabvi.
Maandalizi mengine yanaendelea kama kawaida na kila kitu kinakwenda vizuri. Hapa lengo ni kuwapa ndugu zetu hawa supu ya miiba. ~ Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Pope.
Wanakutana na wafalme wao ndiyo maana wameamua kukaa kimya. Watakaa kimya sana na hawatakuwa na nafasi ya kuzungumza tena. Watakuwa na kipi cha kuzungumza wakati watakuwa wamefungwa. Acha waendelee kukaa kimya, ~ Haji Manara.
NB: Jamhuri Julio alishawahi kunena haya...
"Yanga S.C ni sawa na mti wa maembe uliopo uwani katika nyumba yako.. ukijisikia hamu ya kula embe, unachuma tu, na kukata kiu yako"
... nami sembo naamini kesho tunaenda kujichumia maembe yetu ya kutosha.