Kuelekea mechi ya 'VPL' Kagera Sugar dhidi ya Simba SC, Wamezoea Lakini Leo Tunao!

Kuelekea mechi ya 'VPL' Kagera Sugar dhidi ya Simba SC, Wamezoea Lakini Leo Tunao!

Kikosi cha Simba SC kinachoanza leo dhidi ya Kagera Sugar...NguvuMoja
IMG_20190926_150558_437.jpeg
 
Kuelekea patashika ya ligi kuu Tanzania, Vodacom Premier League (VPL), nyasi za Uwanja wa Kaitaba Stadium, mkoani Kagera kuwaka moto ambapo leo September 26, 2019 Kagera Sugar, Wana Nkurukumbi, wanawakabili vilivyo Mabingwa wa Nchi Simba SC, Mnyama Mkali Mwituni, kutoka jijini Dar es salaam.

Mchezo huu kati ya Kagera Sugar na Simba SC, una vuta hisia za wapenda kandanda kote nchini, hivyo basi unatarajiwa kuwa mkali na wenye kusisimua kwa muda wote wa dakika tisini, kutokana na rekodi za timu hizi mbili hivi karibuni zinapokutana.

Kocha Patrick Aussems, amesema safari hii hawachomokei na amedhamiria kuondoka na alama tatu muhimu, huku akiongeza kuwa;

"Yaliyotokea msimu uliopita ni hamasa kwa wachezaji kufanya vizuri kuelekea mchezo huu, na nimeshawaambia kwamba lazima tuwaonyeshe kuwa sisi ni Simba SC". alisema Kocha Aussems.

•••Usikose Ukaambiwa, kuhusu burudani ya kandanda itakayovurumishwa kwenye dimba la Kaitaba Stadium. Kumbuka kipute hiki ni kuanzia saa 10:00 jioni.

•••Wamezoea Lakini Leo Hii TunaoView attachment 1216340View attachment 1216341
Kagera sugar tundu limejileta hilo
FB_IMG_1569252442812.jpg
 
Kikosi tayari kipo uwanjani kupasha misuli kabla ya mchezo..SimbaNguvuMoja
FB_IMG_1569501950320.jpeg
FB_IMG_1569501944808.jpeg
 
Dakika chache kabla ya kuanza mtanange huu, hatumwi mtoto dukani..!

Kagera Sugar Vs Simba SC
 
00' Naaaaaaaaaaaaaaam mpira umeanza Uwanja wa Kaitaba Stadium

Kagera Sugar 0-0 Simba SC
 
10' mchezo wa VPL, ambapo timu zinashambuliana kwa zamu, huku Kagera akijaribu kuvuka mstari wa kati
 
12' Anakwenda pembeni mwa uwanja kwake Ajibuuuuuuu Ooooooiiii

Ajibu anapiga mpira hafifi na golikipa anaudaka
 
Back
Top Bottom