Kuelekea mechi ya 'VPL' Kagera Sugar dhidi ya Simba SC, Wamezoea Lakini Leo Tunao!

Kuelekea mechi ya 'VPL' Kagera Sugar dhidi ya Simba SC, Wamezoea Lakini Leo Tunao!

56' Mchezaji wa Kagera Sugar yupo chini baada kupata rabsha

Inapigwa faulo kuelekea Simba, inapigwaaaaa inakolewa na kuwa kona aaaa...Konaaaaa la la, mabeki wa Simba wanaokoa
 
61' Deo Kanda anatoka, anaingia Miraji Athuman upande wa Simba SC
 
65' Gooooooal....Mwamuzi wa pembeni kibendera kipo juu kuashiria Offside

Miraji aliweka kambani baada ya Ajibu kutandika shuti kali na kupanguliwa na golikipa hatimaye Miraji kumalizia
 
71' amekwenda kwenye benchi Ajibu, anaingia Dilunga upande wa Simba SC
 
75' pamoja na Kagera kujaribu kushambulia lango la Simba..Lakini kikwazo ni mabeki wa Simba wakiongozwa na Wawa, Tairone
 
Miraji amimina majalo inamkuta Shioub apiga kichwaaaaa goooooal la la la la njeeee.
 
79' anakwenda kupiga Maddie Kagere 1 2 3 4 Goooooooooooooooooooaaal Goooooooooooooooooooaaal

Meddie Kagere anaipatia Simba bao la tatu kwa njia ya mkwaju wa painati baada ya Miraji Athuman kuangushwa eneo la hatari

Kagera Sugar 0-3 Simba SC
 
87' Meddie Kagere anatoka nafasi yake anachukua Wilker

Kagera Sugar 0-3 Simba SC
 
90+5'

Kuelekea kumalizika mchezo huu wa VPL, Simba wakizidi kufikia lango la Kagera mara kwa mara
 
90+5'

Naaaaaaaaaaaaaaam mpira umekwisha uwanja wa Kaitaba Stadium ambapo Simba SC wakiibuka kidedea kwa ushindi wa mabao matatu bila majibu, yakiwekwa kimiani na Maddie Kagere mawili dakika ya 4' 79' na Tshabalala 35'

Kagera Sugar 0-3 Simba SC
 
Mwaka juzi kagera sugar, mwaka jana kagera shuga ala! Watoto wadogo mtusumbue kila uchao. Safari hii mmekula za uso mkalale huko! Hadi ndizi leo zitawashinda kula. Nyaambaf!!
 
Back
Top Bottom