Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Naaaam!
Kuelekea patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League VPL, Jumamosi November 7 2020 kutavurumishwa mchezo wa watani wa Jadi katika soka la Tanzania kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
Wekundu wa Msimbazi Mabingwa wa Nchi, Simba SC klabu kubwa na bora Afrika, ambayo imekuwa ikitoa burudani uwanjani kwa soka la Pira Biriani pamoja na ushindi mnono, wapo tayari kabisa wakiwa wamejiandaa vilivyo kukutana na Yanga SC ambayo haijawa bora kutokana namna ambayo wanapata ushindi dhaifu kabisa kwenye Ligi Kuu Tanzania VPL, ushindi ambao umekuwa ukiwapa tumbo joto mashabiki wao.
Katika mchezo huo Simba SC kuhakikisha inawavuruga kabisa Wanajangwani, itaingia na mbinu ya kumiliki sana mpira uwanjani kama ilivyo asili ya Wanalunyasi, ambapo itawachukua takriban dakika 1-3-4 wakimiliki mpira hali itakayopelekea Yanga kupoteana uwanjani hatimaye kujikuta wakifungwa huku wakishangaa wasiamini kinachotokea.
Wanasimba na mdau wa soka popote pale shuhudia kabumbu lenye ushawishi kutoka kwa Simba SC lililothibitishwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF kutoka kwa Wekundu wa Msimbazi Mabingwa wa Nchi.
Tukutane kwa Mkapa. Zuio kipigo kama unaweza.