Kuelekea mechi ya VPL, Simba SC dhidi ya Azam FC, desturi ya ushindi inaendelea

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Nyasi za uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Jumatano ya Oktoba 23, 2019, zinatarajia kuwaka moto kwa mpambano mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika tishini, katika ile patashika ya Vodacom Premier League VPL, ambapo Mabingwa wa Nchi Simba SC, Mnyama Mkali, watakapokwaruzana na Wana Lamba lamba Ice Cream, Azam FC.

Katika kuendelea na desturi ya ushindi kwa asilimia 100 huku ikiwa imeshinda mechi zote zilizochezwa mpaka sasa, kikosi cha Simba SC chini ya kocha Professor Patrick Aussems, kimejiandaa vilivyo kuwapa burudani Wanasimba na Wadau wa kandanda pamoja na kuweza kupata ushindi na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa VPL.

Kulitaka Mwana...Kulipewa Mwana

Wanasimba na wapenda soka popote pale, jitokezeni kwa wingi kuwashangilia Mabingwa wa Nchi wenye kuonyesha radha ya mpira uwanjani, yaani burudani pamoja na ushindi...

Kandanda la viwango vilivyothibitishwa na Shirikisho la Soka Afrika CAF..NguvuMoja

 
moja kati ya vitu vinavyomuumiza kocha wa simba ni upangaji wa kikosi anashindwa kujua nani aanze na nani akae benchi hii inatokana na ubora wa wachezaji alionao
 
Kosi la kumwua Azam
1. Kakolanya
2. Kapombe
3. Shabalala
4. Nyoni
5. Wawa
6. Mzamilu
7. Ajibu
8. Shibobo
9. Kagere
10. Boko
11. Dilunga
 
Leo tunataka kakolanya aanze maana ameonyesha kitu cha tofauti kwenye match za kirafiki imefika mda sasa aishi akae kando but simba ushindi leo lazima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…