Kuelekea mechi za usiku wa Ulaya leo

Kuelekea mechi za usiku wa Ulaya leo

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Joined
Sep 11, 2020
Posts
69
Reaction score
105
IMG_20210217_123247_469.jpg


Sevilla atakuwa mwenyeji wa Borussia Dortmund katika Dimba la Ramon Sanchez- Pizjuan .

Mara ya mwisho kukutana kwenye michuano hii timu hizo mbili ilikuwa msimu wa 2010- 11 kwenye Europa ligi hatua ya makundi. Sevilla alishinda 1 -0 wakiwa Dortmund na mchezo wa marudiano ulimalizika kwa sare ya 2-2.

Kati ya mechi 10 za ligi ya klabu bingwa walizocheza Hispania, Borussia hajashinda hata mmoja na mechi 9 kati ya hiyo 10 wameruhusu magoli si chini ya mawili.

Ushindi wa Dortmund katika ardhi ya Hispania kwenye michuano hiyo ilikuwa ni mwaka 1996 dhidi ya Atletico Madrid ambapo walishinda 1-0.

Sevilla amekuwa mwenyeji wa timu za Ujerumani mara 12 kwenye mashindano ya Ulaya. Wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya hiyo 12 ambao ulikuwa dhidi ya Bayern Munich katika robo fainali ya ligi ya mabingwa msimu wa 2017/18.

Na katika mechi nyingine hii leo Fc Porto atakuwa nyumbani kuvaana na Juventus.

Takwimu zinaonesha kuwa Porto hajawahi kumpiga Juventus katika michezo mitano iliyopita waliyokutana kwenye mashindano ya Ulaya.

Kwa upande wa Juventus amefika hatua ya mtoano kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa misimu 7 mfululizo, huku Porto hii ni mara yao ya 4 kufika hatua hiyo ndani ya misimu mitano iliyopita.

Fc Porto ndiyo timu pekee ambayo bado haijaruhusu goli akiwa nyumbani katika michuano ya klabu bingwa msimu huu. Na amekuwa na Clean sheets kwenye michezo yao mitano ya mashindano hayo, na hii ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo kwenye mashindano hayo.
 
Uchambuzi mzuri mkuu Dortmund atakufa bila shaka na kunipa hela pia
 
Back
Top Bottom