Jensen salamone
JF-Expert Member
- Sep 28, 2019
- 320
- 641
Zikiwa zimesalia siku chache kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi(mei mosi), walimu tunakuomba mheshimiwa Rais uunde tume ya elimu kukichunguza chama cha walimu (CWT) kwakuwa kimeshindwa kutimiza wajibu wake wa kututetea na kutuhudumia.
Mbali na kushindwa kutimiza wajibu wake wa msingi wa kutulinda na kututetea, chama hiki ni mwiba kwa walimu kwani kimejaa uozo na uzandiki wa kila aina. Miongoni mwa uozo huo ni pamoja na haya yafuatayo:
CWT kinafanya biashara kupitia kampuni ya TEACHERS DEVELOPMENT COMPANY LIMITED ambayo inaendeshwa kwa michango yetu wanayotukana kila mwezi lakini faida inayopatikana kupitia kampuni hiyo hatujui inamnufaisha nani.
CWT wanatukata pesa ya kuchangia mfuko kila mwezi wakati vyama vya watumishi wengine vinachukua michango kwa mwaka.
CWT kupitia michango wanayotukata kila mwezi wamejenga benki ya mwalimu (MCB) lakini sisi kama wanachama ambao tulipaswa tuwe wanufaika wa kwanza hatuelewi chochote kuhusu benki hiyo wala mapato yanayopatikana huko hatuelewi yanakoelekea.
Kila mwezi walimu tunakatwa kuchangia hiki chama lakini uwazi na matumizi ya pesa tunazochangia hakuna na hivyo sisi kama walimu tuna wasi wasi kwamba huenda michango tunayokatwa inaishia kwenye mifuko ya wachache.
CWT kupitia michango wanayotukata kila mwezi, wametengeneza vitega uchumi karibia kila mkoa ikiwemo mwalimu house lakini sisi kama wachangiaji hivi vitega uchumi havitunufaishi kwa chochote.
CWT pamoja na kwamba tunawafikishia vilio vyetu huwa hawatusikilizi na mbaya zaidi wametunyima uhuru wa kufanya vikao kwenye vituo vyetu vya kazi kujadiliana shida mbali mbali zinazotuandama.
Wito wetu kwako mheshimiwa Rais
Tunakuomba uunde tume ya kukichunguza hiki chama na tuhuma zote zinazokikabili ili utusaidie kututua huu mzigo mzito tuliotwishwa na watu wasiotutakia mema sisi walimu.
Mheshimiwa Rais, sisi kama walimu tunaomba tukutoe wasi wasi kwamba hautakuwa wa kwanza kukifuta hiki chama. Kwani uamuzi kama huu uliwahi kufanywa na mwl Nyerere mwaka 1982. Katika kuweka kumbukumbu sawa naomba nikukumbushe kidogo ilivyokuwa.
Katika miaka ya 80 kuliibuka na vilio kama tulivyonavyo sisi walimu leo. Sasa baada ya madai na malalamiko ya walimu kuwa mengi, Rais Nyerere aliunda tume maalum ya elimu kuchunguza madai hayo.
Tume ilipofanya uchunguzi ilibaini kuwa Unified Teachers Service(UTS) ambacho kilikuwa ndicho chama cha walimu kwa wakati huo kwamba kilishindwa kuwahudumia walimu kikamilifu, hivyo tume ikapendekeza kuundwa kwa chama kingine kitakachohudumia na kuwatetea walimu ndipo Rais Nyerere akakivunja na chama kingine kikaundwa.