Kuelekea michuano ya CAF: Yanga SC malengo yenu michuano ya CAF ni kufika hatua gani?

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Kufuatia gazeti la michezo la Mwanaspoti la leo Mei 6,2022 kuandika kuwa sare ya Simba SC dhidi ya Namungo FC na Azam FC kupoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Yanga SC yatanguliza kwenye michuano ya CAF.

Kwa kuwa kila timu inaposhiriki michuano yoyote, lazima wajiwekee malengo kwa kile ambacho wanakiamini kuwa wanaweza, baada ya kupata maandalizi ya kutosha.

Kwa kuwa Mwanaspoti wamesema hivyo mapema kabisa..Je katika malengo matano haya, Yanga safari hii malengo yenu kwenye michuano ya CAF ni kufika hatua gani?

1. Makundi.
2. Robo Fainali.
3. Nusu Fainali.
4. Fainali.
5. Kombe la CAF.

Wenu: Ghazwat, Ekuweme
 
Kipaumbele Cha Yanga kiwe kuimarisha timu Kwa kuongeza wachezaji wenye uzoefu wa mashindano na uwezo mkubwa na kuondoa wachezaji wenye viwango vya wastani.

Wakumbuke Yanga inahitaji matokeo isiwe kituo Cha kukuza vipaji waje wachezaji watakao ingia first eleven mojakwamoja na kwenda kwenye mashindano ya Caf na kufikia hatua za nusu au final.
 
Okay.. Majibu yatapatikana Kimataifa
 
Nyie mnapoulizia mambo ya Uwanja wa Simba SC mnataka maendeleo yake siyo..!?

Au lengo lenu muambiwe ili iweje hapo..?! Ukipita jibu ndo jibu la hapa.
Kawaulize viongozi wa yanga watakupa majibu, Na yanga watawauliza kina mangungu juu ya michango ya uwanja
 
Hili swali tuulize mara baada ya kukabidhiwa ubingwa wa Ligi kuu na pia ule wa kombe la Shirikisho la Azam.

Kwa sasa akili zetu zote tumezielekeza huko.
 
Simple tu,kama malengo ya msimu huu ambayo yalikuwa kuingia makundi ya CL hayajatimia.basi wataanzia hapo,Kisha kama watafika hapo ndo yataanza hayo ya robo fainali.
 
CAF pekee munayoweza kufika nusu ni ile CUF ya Lipumba [emoji23][emoji23]
 
Namba 5πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Yanga huwa wakiona Simba hii hii inavyochanua inaona ni kazi rahisi subiri kimbembe sana. Wakitaka kuingia hata makundi tu inabidi wasajili upya.
Kabisa, wakiona kuna Ahly, Chiefs, RS Berkane, ASEC Mimosas wanaona hata wao wanamudu...! Ngoja Tuone labda waishie round ya awali kama mwaka uliopita.
 
Malengo yao ni kwenda kutetema kwenye Preliminary round then Warudi jangwani kufuga vyura waanze kuandika makala za kuitukana Simba waseme ni ya Peter Banda.
Peter Banda?

Mkuu kuweka kumbukumbu sawa, nadhani ulikusudia kusema ni Abdi Banda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…