Kuelekea mkutano mkuu wa CCM; Je, wajumbe wa Mkutano huo ni akina nani? Tuwajue hapa...

Kuelekea mkutano mkuu wa CCM; Je, wajumbe wa Mkutano huo ni akina nani? Tuwajue hapa...

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Na Bwanku M Bwanku.

Kama tunavyofahamu, Ijumaa hii Aprili Mosi 2022, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitafanya Mkutano Mkuu wake Maalum pale Jijini Dodoma kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre ambao pamoja na mambo mengine utafanya marekebisho ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977, Toleo la 2020.

Je, kwasasa zikiwa zimebaki takribani siku 2 kuelekea Mkutano Mkuu huo Maalum, nani ni Wahusika (Wajumbe) wa Mkutano Mkuu wa CCM ambao ndio watakaoshiriki Mkutano huo? Je kila Mwanachama wa CCM anashiriki Mkutano huo mkubwa kabisa na wenye madaraka ya mwisho ndani ya CCM?

Kwa Mujibu wa Katiba ya CCM ya Mwaka 1977, Toleo la Mwaka 2017, Fungu la 7, Ibara ya 99 (2) imeeleza wazi kwamba Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa utakuwa ndio Kikao Kikuu cha CCM kupita vyote na ndicho kitakachokuwa na madaraka ya mwisho. Kwa lugha rahisi, Mkutano Mkuu wa CCM ndicho Chombo Kikuu cha maamuzi yoyote makubwa yanayoathiri Chama kizima Kitaifa.

Sasa, turudi kwenye Mjadala wetu? Nani Washiriki, Wahusika au Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM? Je Kila Mwanachama wa CCM ni Mjumbe au anaweza kushiriki Mkutano huu? Jibu ni hapana, si kila Mwanachama wa CCM ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu au anaweza kushiriki Mkutano Mkuu huu wa juu kabisa wa Chama bali wanaoweza kushiriki ni wale Wanachama wa CCM waliotajwa kwenye Katiba ndiyo Washiriki wa Mkutano Mkuu huu.

Kwa Mujibu wa Katiba ya CCM ya Mwaka 1977, Toleo la 2017, Fungu la VII, Ibara ya 99 (1) imeainisha wazi Wajumbe wa Mkutano Mkuu na si kila Mwanachama anaweza kushiriki Mkutano Mkuu wa CCM.

Ibara hii ya 99 (1), Fungu la VII kuanzia Ukurasa wa 102 hadi 104 imeeleza, Mkutano Mkuu wa CCM Taifa utakuwa na Wajumbe wafuatao:-

(a) Mwenyekiti wa CCM Taifa.
(b) Makamu Wawili wa CCM kutoka Tanzania Bara na Tanzania Visiwani (Zanzibar).
(c) Katibu Mkuu wa CCM Taifa.
(d) Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotokana na CCM.
(e) Manaibu wa Katibu Mkuu wa CCM wote wawili kutoka Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.
(f) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Zanzibar, wote wanaotokana na CCM.
(g) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizesheni
(h) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi.
(i) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI).
(j) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha.
(k) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Kila Jumuiya ya CCM kwa maana Jumuiya zote 3 kuanzia Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) na Jumuiya ya Umoja wa Wazazi.
(l) Katibu Mkuu na Manaibu wa Katibu Mkuu wa Kila Jumuiya ya CCM.
(m) Wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
(n) Mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM.
(o) Mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM.
(p) Wenyeviti wote wa CCM wa Mikoa.
(q) Makatibu wote wa CCM wa Mikoa.
(r) Makatibu wote Siasa na Uenezi wa Mikoa.
(s) Mwenyekiti, Katibu wa Mkoa na Mjumbe mwingine mmoja aliyechaguliwa kutoka kila Mkoa wa Tanzania Bara na Zanzibar kwa kila Jumuiya ya CCM.
(t) Wenyeviti wote wa CCM wa Wilaya.
(u) Makatibu wote wa CCM wa Wilaya.
(v) Makatibu wote wa Siasa na Uenezi wa Wilaya.
(w) Wabunge wote wanaotokana na CCM au kama Bunge limevunjwa wale Wanachama wote waliokuwa Wabunge mara kabla ya kuvunjwa Bunge na Wabunge wote wa Afrika Mashariki wanaotokana na CCM.
(x) Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi wanaotokana na CCM au kama Baraza hilo limevunjwa basi wale Wanachama wote waliokuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi mara kabla ya kuvunjwa kwa Baraza hilo.
(y) Wajumbe watatu waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa CCM wa kila Wilaya.

Kikatiba ya CCM kama nilivyotaja vifungu pale juu, hao hapo juu kuanzia (a) hadi (y) ndio Wajumbe halali wa Mkutano Mkuu wa CCM na wanaoshiriki Mkutano Mkuu wa CCM.

Ibara ya 99 (7) ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 inaeleza pia kwamba Kikao hiki cha juu kabisa ndani ya CCM na chenye nguvu kubwa kuliko Kikao chochote kile kitaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu ama asipohudhuria basi mmoja wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa awe wa Bara au Visiwani basi ataongoza Kikao hicho na ikitokea wote watatu hawapo ama hawawezi kuhudhuria basi Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itamchagua Mjumbe mwingine miongoni mwao kuwa Mwenyekiti wa muda wa kuongoza Mkutano Mkuu.

Bwanku M Bwanku.
bwanku55@gmail.com

IMG-20220329-WA0033.jpg

IMG-20220329-WA0032.jpg

IMG-20220329-WA0031.jpg

IMG-20220327-WA0009.jpg
 

Attachments

  • ccmtanzania~tv~CbrkVQ2KwMa~1.mp4
    28.6 MB
  • VID-20220326-WA0024.mp4
    9.1 MB
Itakua ni siku ya wajinga.
Alafu kuna jamaa alizaliwa tarehe kama hiyo na mama yake akafariki, chaajabu huyu jamaa hua ikifika hiyo siku anafanya sherehe. Sasa sijui anafanya sherehe ya kuzaliwa ama anasherehekea siku mamake alifariki...!!??
 
Back
Top Bottom