Kuelekea Mpambano wa Watani wa Jadi 'TPL' Simba SC dhidi ya Yanga SC, Tayari ameshafungwa

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Kuelekea pambano la kukata na shoka Jumamosi Februari 16, 2019 la watani wa Jadi (Kariakoo Derby) katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Tanzania 'TPL' Simba SC Mnyama, Wekundu wa Msimbazi dhidi ya Yanga SC Vijana wa Jangwani, ni kama kusema tayari Yanga ameshafungwa, yaani wamekwishapoteza mchezo huo wa TPL.

Wa kimataifa Original Simba SC Taifa Kubwa

Ni kutokana na ubora wa kikosi cha Simba SC, na thamani yake pamoja na safu hatari ya ushambuliaji ikiongozwa na Streika Matata uwanjani Meddie Kagere MK 14, akiunda Muunganiko wa Emmanuel Okwi, John Bocco na kiungo mshambuliaji ambaye anaudambwi mwingi mpaka anakuwa Kero uwanjani Cleoutus Chota Chama 'Triple C'

Mwana Kulitaka Mwana Kulipewa

Kocha Patrick Aussems baada ya ushindi dhidi ya Al Ahly SC katika Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) amesema umewaongezea morali Vijana wake kabla ya kuwavaa Vijana wa Yanga akiweka wazi mipango ya kumaliza kazi ya kuwasambaratisha watani hao mapema kabisa.

Simba iliitambia Al Ahly ya Misri kwa kuifunga bao 1-0 na kurudia ilichokifanya timu hiyo katika michuano ya CAFCL miaka 33 iliyopita katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kwa muktadha huo 'ikiwa mwarabu amefungwa basi Vijana wa Jangwani watatepeta kama mate ya mlevi, Simba imechapwa Klabu bora inatakuwa Vijana wa Jangwani bhana' na hasa ukizingatia Septemba 30 ilikuwa tia tia maji mwana ukome kufuata wakubwa. Ushindi ndo lengo letu la kwanza iwe Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) au Tanzania Premier League TPL..

Tukutane National Stadium kwa MCHINA kama unaweza kuzuia kipigo cha kufedhehesha.

Update•••••••••

Naaaaaaaam mpira umekwisha uwanja wa Taifa ambapo Simba SC imeibuka na ushindi wa bao moja bila (1-0) bao lililofungwa na Meddie Kagere MK 14 kunako dakika ya 71 ya mchezo

Yanga SC 0-1 Simba SC

IMG_20190214_072947_741.jpeg
IMG_20190214_072837_009.jpeg
IMG_20190214_072912_010.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DOOOH. Wacha yangu yawe macho na masikio tu maana kwenye huu uzi nitayaona mengi hasa kutoka kwa Watani zangu hali ya kuwa hata mpira haujachezwa bado. Teh

Haya Mujitahidi Mujae Uwanjani basi msiishie hapa.

"DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"
 
Kuelekea pambano la kukata na shoka Jumamosi Februari 16, 2019 la watani wa Jadi (Kariakoo Derby) katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Tanzania 'TPL' Simba SC Mnyama, Wekundu wa Msimbazi dhidi ya Yanga SC Vijana wa Jangwani, ni kama kusema tayari Yanga ameshafungwa, yaani wamekwishapoteza mchezo huo wa TPL.

Wa kimataifa Original Simba SC Taifa Kubwa

Ni kutokana na ubora wa kikosi cha Simba SC, na thamani yake pamoja na safu hatari ya ushambuliaji ikiongozwa na Streika Matata uwanjani Meddie Kagere MK 14, akiunda Muunganiko wa Emmanuel Okwi, John Bocco na kiungo mshambuliaji ambaye anaudambwi mwingi mpaka anakuwa Kero uwanjani Cleoutus Chota Chama 'Triple C'

Mwana Kulitaka Mwana Kulipewa

Kocha Patrick Aussems baada ya ushindi dhidi ya Al Ahly SC katika Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) amesema umewaongezea morali Vijana wake kabla ya kuwavaa Vijana wa Yanga akiweka wazi mipango ya kumaliza kazi ya kuwasambaratisha watani hao mapema kabisa.

Simba iliitambia Al Ahly ya Misri kwa kuifunga bao 1-0 na kurudia ilichokifanya timu hiyo katika michuano ya CAFCL miaka 33 iliyopita katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kwa muktadha huo 'ikiwa mwarabu amefungwa basi Vijana wa Jangwani watatepeta kama mate ya mlevi, Simba imechapwa Klabu bora inatakuwa Vijana wa Jangwani bhana' na hasa ukizingatia Septemba 30 ilikuwa tia tia maji mwana ukome kufuata wakubwa. Ushindi ndo lengo letu la kwanza iwe Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) au Tanzania Premier League TPL..

Tukutane National Stadium kwa MCHINA kama unaweza kuzuia kipigo cha kufedhehesha.View attachment 1022213View attachment 1022214View attachment 1022215

Sent using Jamii Forums mobile app
mbumbumbu FC aka mikia.
 
Juzi hapa Manu wakajidai kumfunga PSG wamekiona cha moto ,ngoja simba waingia na kujiamini kwao kama walivyoenda misri kikawakuta,Yanga wana wa zoom tu ,huo ni mpira sio bongo fleva.Hao yanga wenyewe walishamfunga Al ahly cha ajabu nini hapa mjini.tukutane kwa mchina
 
Back
Top Bottom