Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ushachelewa sana.
Wanakuambia gari iko 180kph hakuna u turn
CCM waliuasisi UFISADI miaka yote sasa wanapowaambia wanasema maovu yao.Huwezi kuzungumzia CCM bila kutaja UFISADI
Twende na Lowassa..hatuna imani na mwingine
Ufisadi mtu wa Kijijini huko anaujua ni nini? We ahidi nitatoa umaskini,nitawajengea nyumba ndo utaeleweka.Agenda ya ufisadi inaeleweka na werevu wachache watu wengi hawajui ufisadi ni nini.Ni bora kuwa na agenda zinazoeleweka
Wasomi wengi wanafeli kwenye siasa na huwa wanashindwa na watu wa darasa la saba kwa sababu ya kujiona wanajua na wanatoa facts,kumbe wapiga kura wanataka swaga za bomba litatoa maji na maziwa.ndo wale wanaoamini mabomba yatatoa maziwa kumbe!
Baada ya Edward Lowassa kusifiwa na rais Magufuli kuwa ni Superman, namdurufu kidogo Lowassa kwa kujikumbusha niliwahi kusema nini kuhusu mtu huyu.Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%, tena isiwe tuu ni ufisadi bali pia rais wa nchi yetu lazima awe ni mtu mwenye long expiriaence ya uzoefu wa muda mrefu kwenye ajenda hiyo, nikimaanisha ili kuweza kumkamata mwizi, sometimes one has to 'set a thief to catch a thief!', hivyo mgombea pekee wa CCM mwenye sifa hiyo ni one and only Edward Ngoyai Lowassa, ndiye pekee mwenye uwezo wa kupambana na ufisadi kwa sababu sio tuu anaujua, bali yeye mwenyewe anatuhumiwa kuwa fisadi, hivyo ndiye pekee mwenye uwezo wa kupambana na ufisadi!.
Mtu yoyote asiye lijua tatizo kamwe hawezi kupambana nalo!, ili mtu uweze kupambana na tatizo, ni kwanza yeye mwenyewe ulijue tatizo, chanzo chake, na jinsi ufisadi unavyotekelezwa, hivyo kuwa na uwezo wa kupambana kwa kuzijua mbinu zote!.
Mfano hai ni ufisadi wa iliyokuwa City Water, Lowassa akiwa ni waziri wa Maji, baada tuu ya kuujua ufisadi wao, aliwatimulia mbali, wakafungasha virago vyao na kukimbilia mahakama ya usuluhishi kule London, nako tukawatwangwa, sasa imebaki tuu historia ya utendaji uliotukuka wa Edward Lowassa!.
Hivyo Lowassa ndio mtu pekee anayeujua sio tuu anayeujua ufisadi wa Tanzania nje ndani!, bali pia ndio mwenye uwezo wa kukabiliana nao na kuukomesha!. Mfano mzuri ni kwenye ufisadi wa Richmond!, Lowassa alishuhudia jinsi ufisadi huo unavyolitafuna taifa hili na uko kwenye level gani!, kwa ushujaa wa ajabu, akaamua kujitoa mhanga, yeye mwenyewe, kwa nafsi yake, kuibeba dhambi ya ufisadi huo uliotaka kuliangamiza taifa ili yeye ndiye ateketee lakini taifa liokoke!.
Ni kweli aliibeba hiyo dhambi na akafa nayo, kama yule aliyekuja kuzibeba dhambi za ulimwengu huu, ambapo kwa kupigwa kwake, sisi tuliponywa!, alikubali kudhalilishwa, kuteswa hadi kifo msalabani, lakini siku ya tatu, alifufuka na kwenda kwenye uzima wa milele huku amekaa kulia kwenye kiti cha enzi!.
Vivyo hivyo ufisadi wa Richmond, bado uko vile vile, Lowassa aliubeba msalaba ule ili taifa liokoke!, tofauti na yule aliyebeba dhambi za Ulimwengu, dhambi ya Richmond haikuisha kwa kujiuzulu kwa Lowassa, bali baada ya Lowassa kukaa pembeni, wenye Richmond yao, ambayo waliibadili jina kuwa Dowans, wakaishitaki Tanzania kule London, wakashinda!, Tanzania ikajidai haitalipa tozo ya Dowans, ila tozo ile imelipwa 'kisiri siri', Dowans ikajibadili tena jina kuitwa Simbion!, ufisadi ule unaendelea hadi kesho, mitambo ni ile ile!, capacity charge ni ile ile!, ila jina sasa ni Simbion!, na wanaendelea kupiga hela kama kawa!.
Mtanzania gani mwingine mwenye guts za ku deal na ufisadi wa level hii?!. Ni Lowassa Pekee!, hivyo uchaguzi wa mwaka huu ndio ile siku ya tatu...
Pasco