Pre GE2025 Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025: Kwanini Serikali inaonekana kuwajali Walimu zaidi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Siku za hivi karibuni kumekuwa na matamko mengi sana kutoka Kwa viongozi wa Serikali wakiji bebisha Kwa Walimu.

Tamko la hivi punde ni la Waziri Mchengerwa akidai kwamba Walimu ni watu muhimu sana Kwa Taifa hivyo hatokubali wachezewe.

Inaelekea Walimu Huwa Wana play vital role kwenye uchaguzi kuliko Watumishi wengine ndio maana Serikali inajibebisha kwao.kwa Kauli na matendo.

-Imepiga marufuku kuwatoa Walimu kwenye kamati za Ujenzi na kutaka walimu ndio wasimamie ujenzi wa miradi kwenye maeneo Yao.
-Imeahidi Kuajiri zaidi ya walimu 13,000
-Imeahidi kuwapandishia madaraja wote na wengine wameshapandishwa
-Imeahidi Kuwajengea nyumba Kwa Kasi zaidi kuanzia mwaka wa 2024/2024.

Hapo awali ujenzi unafanyika ila sio Kwa speed ya mwakani maana Rais mwenyewe aliwapigia simu eti kuwasalimie wakiwa kwenye kongamano lao.

Tamisemi.PNG

Swali: Je, Walimu ndio Watumishi pekee muhimu Kwa Serikali kushinda Maaskari,Manesi,Watendaji wa Vijiji/Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji kwenye harakati za ushindi wa Chama mwaka 2025?
 
Wawapigie kura
Sasa mbona Kuna makundi ya muhimu zaidi kwenye kupiga kura kuliko hao walimu wachache? Mfano wakulima.

Au wanaamini walimu wanaweza ku influence Watoto wao na Watoto wakawasemea vizuri makwao?

Au walimu wanaweza shawishi jamii? Mbona Mimi siwezi shawishiwa na mtu bila kuamua Kwa utashi wangu?

Labda Kuna la ziada
 
Itakuwa Kuna la ziada kaka
 
View attachment 2866067

Swali: Je, Walimu ndio Watumishi pekee muhimu Kwa Serikali kushinda Maaskari,Manesi,Watendaji wa Vijiji/Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji kwenye harakati za ushindi wa Chama mwaka 2025?
Hoja zako zote hazina mashiko. Au unataka kutuambia hao watumishi wa kada nyingine wamekuja kukulalamikia ya kwamba serikali haiwathamini? Na badala yake imeanza kuwathamini walimu tu?

Kwani kupanda si ni haki ya mtumishi? Na hizo ajira zilizotangazwa ni za walimu pekee? Mbona hujaitaja kada ya afya? Juzi kati tu hapa TRA wametoka kuajiri mamia ya wafanyakazi wake! Na wenyewe ni walimu wale?
 
Swali: Je, Walimu ndio Watumishi pekee muhimu Kwa Serikali kushinda Maaskari,Manesi,Watendaji wa Vijiji/Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji kwenye harakati za ushindi wa Chama mwaka 2025?
Askari manesi na watendaji wengine wanatokana na walimu na ndiyo maana kwa nchi kama Ujerumani wanawalipa vizuri kuliko watumishi wengine

Ila kwa hili la huyu waziri huenda wameikamata pabaya serikali yao kwa sasa
 
Sasa mbona Kuna makundi ya muhimu zaidi kwenye kupiga kura kuliko hao walimu wachache? Mfano wakulima.

Au wanaamini walimu wanaweza ku influence Watoto wao na Watoto wakawasemea vizuri makwao?

Au walimu wanaweza shawishi jamii? Mbona Mimi siwezi shawishiwa na mtu bila kuamua Kwa utashi wangu?

Labda Kuna la ziada
Kwa hiyo unataka kutuaminisha hapa wakulima hawathaminiwi, au!! Isipokuwa walimu pekee ndiyo wameanza kuthaminiwa!!

Halafu wewe jamaa ni mnafiki sana!! Wakitokea watu kuiokosoa serikali yako ya CCM kuhusu sera zake mbovu dhidi ya wakulima, wafanyakazi, na wafanyabiashara wa nchi hii; huwa unajifanya kuitetea.
 
Umemsikia nani anawazungumzia wakulima?
 
Umemsikia nani anawazungumzia wakulima?
Mchengerwa amewazungumzia walimu kwa sababu yupo ndani ya Wizara husika.

Vipi kuhusu Waziri wa kilimo Hussein Bashe miaka miwili iliyopita pale bei ya chakula mfano mchele, maharage, nk ilipopanda mara dufu; mbona alikuwa upande wa wakulima!! Na hata tulipolalamika humu jukwaani, mliishia tu kututukana na kutukejeli!!
 
Ukiona mfugaji anahangaika kuwapatia chakula kuku wake wanenepe, siyo kuwa anawapenda sana hao kuku bali mfugaji anajitengenezea kitoweo safi.

Hivyo waalimu wanapaswa kustukia mtama mwingi wanaomwagiwa na CCM
 
Back
Top Bottom