Pre GE2025 Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025: Kwanini Serikali inaonekana kuwajali Walimu zaidi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hao na watendaji wa vijiji ndio hufanikisha wizi wa kura. Acha waanze kujibebisha wakati huu.
 
Wewe jamaa una wivu wa ajabu sana! Sasa hapo shida iko wapi? Hao ni watoa huduma muhimu katika jamii! Unaona ni sahihi kwao kuishi katika mazingira magumu?

Mbona wanajeshi na askari polisi wanajengewa majengo ya kisasa!! Maana ni kutokana na unyeti wa majukumu yao. Sasa wewe walimu na watumishi wa afya wakifanyiwa jambo dogo tu kama hilo, eti unaumia! Halafu wakitoa huduma mbovu kutoka na mazingira/maidha magumu wanayoishi; unalalamika tena!
 
mie naona si walimu tu hata WAKULIMA madaktari na actually waTanzania wote tu 🐒
 
Kwa asilimia kubw zoez huendeshw na walimu lakn mchengerwa ni hulka yake kuttetea maslai ya watumish chin ya Tamisemi , afya elimu kilmo n.k
 
Ni moja wapo wa kikosi cha waiba kura kwa ajili ya uchaguzi wa 2024 na 2025
Sasa hivi kuna mchakato wa kuanzisha Tume Huru ya Uchaguzi. Badala ya kulalamika tu! Tupaze sauti zetu kuhakikisha hiyo tume inakuwa huru kweli.
Yaani viongozi wake wasiteuliwe moja kwa moja na Rais, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama tawala!

Tuhakikishe Wakurugenzi wa Halmshauri, Miji, Manispaa na Majiji hawahusiki kuwa wasimamizi wa huo uchaguzi! Tuhakikishe pia watumishi wa umma wakiwemo hao walimu nao pia hawasimamii huo uchaguzi; ili mshindi apatikane kwa haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…