PreGE2025 Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025: Watia nia CCM wabainika kugawa rushwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga kimesema kuwa jumla ya wagombea tisa wa nafasi za ubunge na udiwani wilayani humo wamebainika kujihusish na vitendo vya kugawa fedha kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa wilaya nyakati za usiku, kinyume na maadili ya chama.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kahama, Andrew Chatwanga, akizungumza na wanahabari amefichua kwamba wagombea hao wanatoka kwenye majimbo yote matatu ya wilaya hiyo: Kahama Mjini (watano), Ushetu (wawili) na Msalala (wawili).
GqiW7ocXUAEU6te.jpg
Amesema vitendo hivyo si tu vinakiuka taratibu za chama, bali pia vinadhihirisha dharau kwa wajumbe na kudhalilisha dhamira ya chama ya kuwa na viongozi wanaokubalika na wananchi kwa uwezo na si kwa fedha.

“Tumebaini baadhi ya watia nia wanazunguka usiku kwa kata mbalimbali kuwapa wajumbe fedha, wengine hadi Sh10,000 ili wawapitishe kwenye mchakato wa ndani. Hii ni aibu, ni udhalilishaji na ni kinyume cha maadili ya CCM. Chama hakiwezi kumvumilia mgombea wa aina hiyo,” amesema Chatwanga akizungumza na wanahabari.

Amesisitiza kuwa taarifa za wagombea waliobainika zimewasilishwa katika ngazi za juu za chama mkoani na makao makuu, na kuonya kuwa yeyote atakayebainika kuendelea na vitendo hivyo ataondolewa kwenye mchakato hata kabla ya kuchukua fomu.

Chatwanga amewaonya pia makatibu wa matawi wanaokumbatia wagombea na kudai kuwa ni “wagombea wao”, akisema chama hakiwezi kuvumilia viongozi wa aina hiyo wanaoeneza makundi na ushawishi wa kifisadi.

Chanzo: Jambo TV
 
HUWEZI TENGANISHA RUSHWA NA CCM.

HAO NDIO WANACCM .
 
Kwa vile wagombea wote wa CCM kila nafasi watatangazwa kuwa wameshinda kwa 99.9% hivyo nguvu kubwa inawekwa kwenye kupitishwa kura za maoni, baada ya hapo ni mserereko tu kwani dola ndiyo itafanya kazi ya kuwatangaza. Na pia kwa wapiga kura hakuna haja ya kwenda kupiga kura CCM imekwisha shinda. Siku ya kupiga kura ni kupumzika tu nyumbani.
 
Uchaguzi batili hautafanyika.

Bali baada ya reforms kufanyika ndipo patafanyika uchaguzi.
 
Back
Top Bottom