Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Ni imani yangu kuwa chama kitakuwa kimoja baada ya uchaguzi. Kimaumbile sina grudges. Tutapiga mstari na kusahau yaliyopita ili kuanza upya.
 


Mimi sasa naanza kupata wasiwasi na watu kama akina Ado waliojisajili juzijuzi. Maana mnavyochangamkia issue za Chadema wakati wa kashfa za NEC ya CCM ambayo issue zake zinatuathiri wengi lakini hatukuwa notice. Sasa leo mnapokuja kutuletea habari za jikoni za Chedema tena bado za motomoto inatufanya tuwe na wasiwasi na nyie. Maana humu tulikuwa na akina Mugongomugngo, Mchunguzi na Tafiti wakapiga propanganda zao na kutetea pande flani then wakaishia kimya kimya. Sasa msije mkawa ndiyo design hizo hizo!!!!
 
Kama imefika hatua ya kuanza kunyoosheana vidole hadharani, naona future ya chama na baadhi ya wanasiasa inaenda mrama. Kutofautiana kimawazo inakubalika katika ngazi yoyote ama jumuiya yoyote lakini inapofikia hatua ya kushindwa kuelewana ama kuvumiliana na kuanza kusema ovyo ama kuomba msaada/support kwa watu ambao unajua fika hawalitakii mema kundi lako ama wewe binafsi, kitakachofuatia ni kilio na kuchekwa tu bila kuonewa huruma.

Kama vijana wenye kuelewa, hayo matatizo mlitakiwa myamalize kimya kimya bila hata nyumba ya jirani kujua kinachoendelea kati yenu. Ni vyema mkaelewa kuwa; "VITA VYA PANZI FURAHA YA KUNGURU"
 


Kwa mujibu wa mambo ulivyotueleza inaonekana kuna harakati za makundi humo nyumbani mwenu. Sasa sisi tulio nje tungependa tujue utachukuwa hatuwa gani kuondosha makundi hayo? Kwa sisi wengine tunaunga mkono hatuwa yako ya kuweka wazi hali halisi ndani ya Chama chako lakini tunataka kuona hatuwa zipi zitakazoondowa hilo tatizo?
 
Ni imani yangu kuwa chama kitakuwa kimoja baada ya uchaguzi. Kimaumbile sina grudges. Tutapiga mstari na kusahau yaliyopita ili kuanza upya.

will never be the same again, and the trust we had on CHADEMA will never be the same. Hapa mmeonyesha kuwa si chama mbadala wa CCM, bali kundi la wapenda vyeo. I'm sorry, but you should know that we trusted much on CHADEMA sasa mnaturudisha nyuma sana.

Also, i advice you keep silent because your words as for now heals nothing, zaidi yanaweza kuharibu zaidi. Poor us Tanzanians nani wa kutuokoa?
 
niliombwa kujitoa na nikajitoa kama ilivyotangazwa.

Ikiwa na maana ya kwamba ulikubaliana na hoja zilizotolewa na Kikao cha Wazee as to kwa nini wewe usigombee hiyo nafasi ya Uenyekiti wa Chama? Na ukaridhia hoja zao?
 

ulijuaje kama Kafulila kashinda?....unaweza kutupa HINT kidogo?
 
Kwanza Pole Mh. Zitto kwa kashikashi zote hizo,

Hivi ukiwa kama Kiongozi Mkuu kwenye Ukatibu Mkuu Makamu hivi huoni kuwa umeingilia huo uchaguzi kwa kusema wewe mwenyewe kuwa ulifanya kampeni wazi wazi kwa vijana hawa wadogo huoni kuwa ukutenda kosa??

Mh Zitto! kwenye kipindi kama hiki kizito kwa chama kwanini usiwe na moyo kama wa mwenyekiti wako Mbowe ukakaa kimya kwa masrahi ya chama kwanza, unapoanza kusema mambo ya Fedha (CAG) huoni kuwa hapo kuna mushkeli,

Pia kuja hapa kwenye JF forum kumwaga razi lote hilo ambalo kuna utitiri wa wanaCCM kibao, huoni kuwa unavujisha siri??

Mimi sina chama ila picha unayoonyesha ni ile ya mapindikizi ya CCM tuliyozoea kuona!!!
 
Ni imani yangu kuwa chama kitakuwa kimoja baada ya uchaguzi. Kimaumbile sina grudges. Tutapiga mstari na kusahau yaliyopita ili kuanza upya.

Zitto,
Kupiga mstari na kusahau yaliyopita haitakuwa determined na wewe tu! Kama unaendeleza maneno unadhani wewe pekee ndiye utakayeamua mambo kuwa mazuri! Au unaamini ni wewe tu ndiye unatakiwa kusamehe. Katika haya malumbano lazima kuna watu wengi wanajeruhiwa na actions/omissions zako. Act now before things are out of hands! Zitto, sitaki kuamini you dont see the effects of the damage that you are part in its making!

Guys!
 
Ikiwa na maana ya kwamba ulikubaliana na hoja zilizotolewa na Kikao cha Wazee as to kwa nini wewe usigombee hiyo nafasi ya Uenyekiti wa Chama? Na ukaridhia hoja zao?

Good questions zinazohitaji majibu ya kina
 
mh,mimi chokaa kabisa,CHADEMA?mwenyekiti MBOWE huyu mmemuweka agombee upresident?hivi mko serious na hayo mageuzi?mbowe mimi simkubali hata kwa virungu kwanza ni dikteta waulize waliofanya nae kazi pale club,na ana historia chafu sana hata yeye anajijua leo iweje agombee urais?pili yeye,baba mkwe wake,wajomba na wanafamilia wao ndio viongozi wa hicho chama,haya na leo napata kali zaidi zitto nae na mamaake ndani,hiki chama nadhani ni saccos kama nnavyokumbuka kuna mtu alisema humu,na angalia sasa nilianza kushawishika kama zitto angegombea uenyekiti nimpe kura yangu lakini sasa mmh!inabidi nijikalie tuu niendelee na shida zangu bongo hakuna mageuzi wala demokrasia,nyie endeleeni na majungu wenzenu nyumba ya pili wanachekelea tu,kwani mvurugano wenu ndo unaowapa wao uhakika wa kututawala maisha.chao
 
Wala siasa siamini kama ni mchezo mchafu , kampeni na kuzidiana yes ndiyo mana ya ushindani na ushabiki muda wote .Kutofautiana mawazo yes ni jambo ka kaaida hata mtu na mzazi wake lakini huwa wanatafuta point ya kukutana.

Vijana Chadema kuwa na siasa za maji taka si mahala pake ni aibu kukimbilia forum kila mara .Yes kuna wengu wanasoma na wanaweza kutoa ushauri ila si kila jambo mnaletana hapa.halisaidii chochote ni kujiabisha tu .

Naamini bado kwamba mkishindwa katika kambi yenu basi mnakubali mnaendelea .Why uwe desparate hadi uje na news za aina hii hapa ? Kwani lazima uwe na madaraka si unaweza kuwa mwana chadema wa kawaida tu ? Unaweza toka makao makuu ukagombea huko mtaani tawini ama mkoani na wilayani ?

Aibu hii .Lakini ndiyo kukomaa pia .Chadema inakuwa na hakika uchaguzi utaonyesha nani kapi na maslahi tumbo na nani kichwa na maslahi Tanzania .

Poleni sana ila mshindane kwa hoja na vioja .
 
Unajua nilikuwa sijakusoma mkuu Zitto sasa nimekuelewa wabaya wenu wanao vuruga chama wamo humo humo ndani ya chama kwa nini msiwatupie vilago na kuwaambia ukweli waende wakapike majungu vyama vingine vipo vingi wanaweza kwenda kwenye NGO ya CCM au kwa mzee Kilacha pale au kwa ngosha UDP.
 

Mkuu,Zitto hajawahi kujigamba kuwa ana magari 5, alichofanya ni kuweka wazi kuwa ana magari 5, sasa kwa level ya Mbunge hiyo haitutishi, hata mimi mwanafunzi najibana hapa ulaya na nina magari 2! acha kueleza vitu in childish way, Zitto amefungua njia kuwa hawa viongozi ni vizuri wawe wanasema mali zao, Magezi hapa hukuwa wewe!



Anasema ukweli na hiki wengi hatutaki na tunamuandama kwa kuwa mkweli


Asante, kwanza Pole sana kwa kumuhusisha mama katika haya, jamani ndugu haya mambo ukijiweka kuwa ndiye wewe anything that includes your parents and spouses negatively hurts, kama htuna uwezo wa kujua kuwa unaweza kuumiza feelings za watu wengine, we are far away from having truly dream leaders.


Kumbe una hakika,kwa post hii tu au una source nyingine, kama kwa post hii tu , una hakika pole, be careful usije acha mke

Ni imani yangu kuwa chama kitakuwa kimoja baada ya uchaguzi. Kimaumbile sina grudges. Tutapiga mstari na kusahau yaliyopita ili kuanza upya.

Zitto divisions are everywhere, we can not avoid it, we need strong leaders who will stand in their beliefs, tatizo la migawanyiko bado ni kutokana na uongozi wa juu ni dhaifum we need to work in this, lakini kuna watu hata UFANYE NINI WATAWEKA MAKUNDI LEAVE THEM STAY FOCUS .Masiha mwenyewe walimuaa very same people aliokuwa anawaponya, binadamu tuna dogo?? watu wasiojua kitu siku zote hawajui, unless wawe wewe

Keep up, stay focus
 

maneno mazito Mkuu Lunyungu.........yaani hivi sasa nina maswali meengi sana najiuliza sipati majibu
 
watanzania bwana tushageuzwa fikra sasa tumesahau madhambi ya NEC na Chichiem tunapambana na kina chadema,well it proves ni namna gani tnalack intelligency sisi watanzania,inasikitisha sana sana,kwani ipo waziwazi kuwa wameshapandikizwa watu Chadema kuvuruga na kuleta mpasuko,Wangwe kauliwa na wazee wa system leo hii kitabu,hapa Zitto ghafla anataka uenyekiti,ghafla anajitoa,hapa uchaguzi wa vijana mihela inamwagwa,cant we be sensible a little bit?ebu tuyadharau haya ya mafisadi tujadili great ideas,hizi zimekaa kimajungu majungu tuu!!hazitusaidii,humu ndani ni usalama wa taifa kibao,na wanaccm wanataka kutuvuruga hakuna lolote!!idumu democracy ya kwel!!
 


Nafikiri ungepaswa kuvaa viatu alivyonavyo Kabwe sasa na kuona jee amefanya uamuzi sahihi au la badala ya kuangalia upande mmoja wa shilingi.
Ni huyu huyu Kabwe alinyamaza wakati kundi fulani ndani ya Chama chake walipomshambulia kwa maoni yake kuhusu kununuliwa mitambo ya DOWANS, walimwita kila aina ya majina ili kumfanya kuwa hafai kuwa mmoja wao. Wakati Zitto alipochukuwa fomu kugombania nafasi ya uenyekiti ni hao hao waliompakaza na kumshambulia ilihali ilikuwa ni nafasi nzuri ya kumuondowa katika umaarufu kwa kumwacha aangushwe kenye uchaguzi.
Pengine umuhimu wake na sapoti yake iliwafanya wamzuie kwa staili ya kumuomba na hata baada ya kuachia bado wanamtupia madongo. Hivyo kwa ajili ya kunusuru umoja wa CHADEMA si wasingelimuhusisha na kashfa ya uchaguzi wa Vijana? SI lingekuwa jambo la Busara kwa wakati huu, muda mfupi tu baada ya kuondosha tofauti zao.
HAPANA! ALICHOFANYA ZITTO NI SAHIHI KABISA KWANI BILA YA KUANIKWA HAWA WANGEEMDELEA KUKUZAMISHA CHAMA KWA KUMUANDAMA MOMOJA MMOJA< PENGINE ANGEFUATA SLAA BAADA YA KUWAMALIZA WANGWE(marehemu) NA ZITTO,
Sasa mambo yapo hadharani umma utakuwa shahidi kwa matendo ya kila mmoja.
 

Hakuna cha ku keep kwayati

Sema ili wananchi tujue tunapoenda ktk uchaguzi tuna deal na watu wa namna gani.

Hizi the said sili ndiyo ttunazipinga kila siku.
 


Nakuunga mkono mkuu .

Kuna wabaya ambao wanaleta shida kwenye Chama na wanaleta issues kati ya Zitto na Chadema .Mbowe utakuwa mwenyekiti make sure you clean the mess .Chuck them out watu hawa si wazuri kwa chama.Ni wahujumu wa maisha ya Watanzania .Uongo ni simu zaidi ya sumu yenyewe .

Slaa Mzee baada ya uchaguzi fanyeni mageuzi makubwa kuanzia kurugenzi na mambo ya Pesa .Ni wakati sasa wa Chadema kuwa na Accountant wa kuajiriwa na si mwanasiasa ambaye mwisho wa siku tena naye anapanda jukwaani .Chama kiwe na watu wa kazi wabakie nakazi na wana siasa jukwaani .Kuna vitengo vina shida hapo .Nitakuandikieni barua mjue kwamba tunajua na mfanye marekebisho .
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…