Mkuu wewe ulipoenda Kyela na jina lako lilipokuwa likitajwa sisi tulikutetea na haikutosha uikaingia Mwenyewe kujibu hoja mbali mbali.
Zitto alidhalilishwa na watu wa Mbowe kwa kuleta habari ya uongo,majungu,dharau na uzushi juu ya ushiriki wa Zitto na Mama yake kwenye uchaguzi wa vijana.maneno yale bila ya Zitto kuja kuyakanusha yangezidi kuvuruga jina lake. unataka akae kimya hadi lini. tarehe 26 mwezi huu KIBANDA kaandika makala chafu kwenye gazeti la MBOWE TANZANIA DAIMA. jumapili hii tarehe 30 akaja NGURUMO kutia msumari kupitia gazeti hilo hilo. Zitto akawa kimya tu.
leo hii wamekuja kwa kumuingiza mama yake mzazi.Zitto sio Mtume au malaika ana kiwango cha kuvumilia. wewe mbona unamchafua Mwakyembe kwanini usinyamaze? mie nilifungiwa kwa kukutetea wewe wiki nzima ulipokuja hata kunipa pole umeshindwa.
Kweli binadamu hatujioni.
Zitto jibu kadri inavyowezekana. wao wamewatumia KIBANDA,KWAYYU NA NGURUMO kukuchafua kwa wajumbe wa mkutano mkuu, sasa wameumbuka pamoja na yote hayo Kafulilla kapiga bao.
- Inachekesha sana kwa mtumzima kama wewe kuleta habari za Malecela, wakati
Zitto anaongelea habari za jinsi alivyoshirikiana na wenziwe huko Chadema kumuuua Wangwe,
- unajaribu kutetea Zitto kuenguliwa nje ya vikao vya chama badala ya kugombea il, ashindwe kwenye uchaguzi, unasema ni jambo la kawaida huku ukiwa unajua kabisa kwamba ni tabia mbaya sana ya CCM iliyotufikisha hapa tulipo yaani taifa la Banana Republic, unajaribu kwa nguvu zote kutetea huku ukitumia mifano ya upuuzi wa CCM, and you think you are making a sense,
- Hivi ni lini umesikia rais wa US ameondolewa nje ya uchaguzi wa kidemokrasia, mmelichemsha sasa mlinywe wenyewe CCM has nothing to do with it hili kama la wangwe ni lenu wenyewe na ni aibu sana, demokrasia inadai Zitto aruhusiwe kugombea kama kushindwa akashindwe kwenye kura za wananchi sio busara za wazee wanaogawana ruzuku za chama,
- Kama kweli Chadema mnajali demokrais makini basi mpeni nafasi Zitto agombee, hili halina mjadala wala compromise, na hamtaweza ku-recover from this ugly political mistake, sasa tumeelewa kwamba hicho ni cahma cha wachache sana ambao kugombea kwa Zitto kumetishia mlo wao yale yale ya kina Karamagi, sasa mnajionyesha rangi zenu rasmi kwamba hamna cha demokrasia wala umakini, ni wababaishaji tu kama yale mafisadi ya ndani ya CCM,
Kama kweli mnajali demokrasia basi waaambieni viongozi wenu wamruhusu Zitto kugombea kama hamuwezi acheni na hizi spin za kitoto za kulinganisha Zitto na Malecela, kwa sababu ni aibu sana kwa watuwazima, JF hatujawahi kuogopa mtu wala jina au chama, licha ya baba wa mtu yoyote hapa huwa tunapiga mawe tu mmelichemsha sasa mlinywe kama ni spin Zitto atawachafua sana na hamumuwezi, si unaona so far anayoyafanya mamluki wa demokrasia, mnafikiri mnaweza kutudanganya hapa watuwazima, mmelikoroga sasa mlinywe la moto!
Kama kweli nyinyi ni demokrasia makini mruhusuni Zitto agombee, kama hamuwezi basi nyamazeni kama mafisadi wa ndani ya CCM, wao huwa hawasemi sana huwa wana vitendo tu, Chadema mmetuabisha sana na kutukatisha tamaa wananchi ulio wengi, kumbe mko sawa na CCM tu!
Respect.
FMEs!
Nafikiri Malecela hakuondolewa jina lake ila mafisadi walipiga kampeni za kifisadi akatolewa kwa kura ktk round ya mwanzo.Habari ndiyo hiyo.
Haya sasa unaingia na gear nyingine kabisa ktk kuspin issue tunayozungumzia.Inachekesha sana kwa mtumzima kama wewe kuleta habari za Malecela, wakati Zitto anaongelea habari za jinsi alivyoshirikiana na wenziwe huko Chadema kumuuua Wangwe,
Mkuu, kwani wewe hujui hilo?kwa hiyo ccm ndio model ya chadema?
Zitto Amelewa sifa na hivyo itakuwa vigumu sana kubaki kama alivyokuwa awali. Kuna kila dalili kuwa nguvu fulani ya kutaka kudhoofisha CHADEMA na huku mwenyewe ameshiriki kujenga kwa miaka mingi. Huyu Siyo Zitto tunammjua toka akiwa na Makala Zake akiwa anaandika gazeti la RAI kwa wakati ule. Jamani anapaswa kushauriwa haraka sana na sasa kama ana majeraha mengi. Siwezi amani kama kweli anafanya hivi kwa manufaa ya CHAma chake, Hapana, Sifa zimemlevya tena sana. Zitto badilika Haraka sana la Svyo utaweza kuwa kama Kabour wa Kigoma. Naanza kupata shida na mawazo mengi toka kichwani kwangu.Field Marshall Es,
Haya sasa unaingia na gear nyingine kabisa ktk kuspin issue tunayozungumzia.
Wapi Zitto kasema alishiriki ktk mbinu ya kumuua Wangwe?...hivi kweli wewe unamtendea haki au unamchulia zaidi!
Mimi ndo nimemuuliza Zitto atuambie kilichotokea haswa ikiwa yeye ameamua kusema ukweli wote na sikumaanisha kwamba Chadema na Zitto walifanya mbinu ya kumuua Wangwe. Nimetaka kujua ukweli wote maadam yeye kaamua kuanika kila kitu hapa JF.
Pili, unapotumia mtazamo wangu ni bora zaidi upinge hoja yangu kwa hoja siii swala la CCM na upuuzi wake. Nimesema vyama vyote duniani vinaweza kuengua jina la mtu hii haina maana Zitto alienguliwa kwa sababu hizo hizo. Ila nachosema Demokrasia ni pamoja na mgombea kukubali kutopitishwa jina lake la wazee wa baraza kutokana na katiba ya chama husika..Mtu yeyote anaweza chukua form ya kugombea Urais iwe Marekani, UK, Caanda na hata Uchina lakini jina lake linaweza enguliwa ikiwa mtu huyo hana sifa, hakutimiza masharti au amekiuka baadhi ya kanuni na sheria za uandikishaji.
Ni jambo la kawaida kabisa, na mtu kama Zitto alitakiwa kuwa mvumilivu, kuheshimu na kukubali matokeo au kufuatilia swala zima kwa kutumia misingi ya sheria inayoambatana na kukata rufaa au kutoa lawama zake. Mzee Malecela alifanya hivyo na heshima yangu kwake nitampa pale aliposindwa kukipaka chama kizima kwa sababu yeye kaenguliwa. Sikuandika kitu chochote kinachohusiana na ubabe wa CCM ila hekima alotumia Mzee Malecela na hata Mzee Sitta kuonyesha kukomaa kwa wanasiasa hao. Chama ni mjumuiko wa watu wa kila aina hivyo issue sio chama hapa ila mhusika anaweza vipi ku handle issues kama kiongozi alokomaa kifikra.
Mkuu wangu hapa tunazungumzia MTU na maamuzi yake na sio chama..Napinga sana yaliyomkuta mzee malecela kwa sababu naelewa kilichofanyika. Na napinga kuenguliwa kwa Zitto ktk kugombea Uenyekiti lakini maadam yeye alikubali kuondoa jina lake ina maana alikubali kujitoa kwa mujibu wa sheria au ushauri wa baadhi ya watu. Kitendo cha yeye kujitoa wakati bado akiwa na hasira inaonyesha wazi hakuwa mkweli.
Tofauti na Wangwe on the otherside alihakikisha haki yake anapewa na nadhani hata Zitto mwenyewe aliwahi kupinga kuwepo kwa njama dhidi ya Marehemu.. leo hii ndio kwanza tunajua ukweli wa mambo yote baada ya mkuu Zitto kupandisha mashetani yake.
Tatizo sii kuupata ukweli ila nashangaa tena kwamba huyu mtu siku zote alikuwa kimya wakati Wangwe akifanyiwa unyama wote na yeye mwenyewe anakiri kuwa mshirika, leo inatokea kwake ndio ukweli tunakuja upata akiwa mshirika wa mbinu chafu against Marehemu.
Ni mchanganyiko wa mambo yote haya ndipo napohoji dhumuni la mheshimiwa
Zitto kama kweli ni kwa maslahi ya chama au yake mwenyewe binafsi. Mandingo wanasema - Chicken has come home to roost! Ukiwa ktk mbinu ya kumuengua mtu ktk kiti cha makamu mwenyekiti, kumbuka malipo yake yanaweza kuwa hapa hapa duniani na hivyo kulalamika kwa Mheshimiwa Zitto hakuwezi kumsafisha hata kidogo ila kinaharibu jina zima la chama.
Wewe kama mwana CCM unafurahia haya yanayotokea na utasema sana kumwita Zitto a hero kwa sababu unataka Chadema wanakwisha..Siku zote wewe mwenyewe husema Siasa ni mchezo mchafu. Unaelewa fika rafu ambazo CCM hutumia na mara zote umekuwa nyuma ya rafu hizo ukiwaambia Chadema wao wanshindwa kipi kucheza rafu mpira wa mchangani usokuwa na refa.
Mimi sii mwanasiasa na nitasema ukweli kwamba ndio sababu kubwa inayonifanya nisiwe mwanasiasa kwa sababu Siasa ni UONGO unaokubalika. Ukiwa mkweli siku zote ktk siasa U will fail na hakuna kitu kibaya ktk makundi haya ya siasa kama Panya (rat) ambaye ni mwepesi wa kuropoka na kusema siri za chama ukidhani ndio ukweli...
Mkuu wangu tunazungumza kila siku na tunafahamiana zaidi ya miaka 30 lakini hata siku moja sijakusikia uki lalamika kuhusu mkeo au familia yako. Hii haina maana ndoa yako ni shwari lakini unajua fika kuwa mimi sii solution pamoja na kuwa mshikaji wako. Swala la ndoa yako ni nje ya ufahamu wangu kabisa isipokuwa tu pale panapojenga urafiki wetu na ndoa yako. Sitakiwi wala sipaswi kuelewa kitu kama kuna matatizo mazito, wapo watu na vyombo ambavyo vitaweza ku solve matatizo ya ndoa yako sii mimi..
Na kibaya zaidi ni pale utakapo nieleza ubaya wa mkeo tu ktk kila janga bila kutoa nafasi sawa kwa mkeo kujieleza. hapo utakuwa unaivunja ndoa wewe mwenyewe, njia nzuri na yenye suluhu ni pale pande mbili zitakapo shiriki ktk mazungumzo au upanisho wowote ule.
Zitto anapokuja hapa JF na kukipaka chama anategemea ku accomplish kitu gani?.. sisi tutamsaidia kipi haswa kama sii kuongeza chunvi ktk kidonda!..Mkuu wangu utu uzima ni pamoja na kuwa nahekima ya kupima uzito wa issue na ukaweza kuziwakilisha ipaswavyo. Uwezo huu Zitto hana na hakika ni moja ya sababu ambayo binafsi nisingempa nafasi ya kuongoza chama. Tabia hii pekee ni liability kwa chama na inaruhusiwa kabisa kumuengua mgombea pamoja na kwamba anweza kuwa na umaarufu kwani siri za Vatican hubakia Vatican..That is leadership hakuna unafiki.
Mkuu, kwani wewe hujui hilo?
Kwa kweli hata mimi siamaini kwamba CHADEMA ni wale wale...AKINA Mkuchika na makamba......I dont want to believe!! Duh...sasa itabidi next year nisipige kura...
Friends..I might be wrong..ila mimi mpaka hapa sijaona kosa la Zitto. Kwa sababu kama alivyosema FMES sioni kwa nini CHADEMA waogope kuwapambanisha wananchama wake Zitto na MBOWE..WHY???????????????????
Jamani kama Zitto akikubalika..si ndo demokrasia yenyewe?? KWA NINI WAZEE WA CHADEMA WAOGOPE?
Inasikitisha na inauma sana.
Itawachukua muda mrefu sana katika kuzifuta hizi.. maana kuna watu wametulia na wanafutilia kwa makini yote haya Zitto ameyataka yeye mwenyewe ndio sababu ya yote haya.Mkuu, usiache kupiga kura. Maana usipopiga kura wewe, wenzako watakuchagulia viongozi na hutaweza kuwalaumu wakikosea. Nenda tu, kapige kura yako, labda matokeo yatakuwa nafuu.
Ni kweli kuwa Zitto hakuwa na kosa kutaka kugombea nafasi ya uwenyekiti wa CHADEMA. Alikuwa na haki kabisa ya kufanya hivyo. Kosa walilofanya viongozi wa CHADEMA kumuomba atoe jina lake kwenye kinyang'anyiro hicho, ndio kosa baya kidemokrasia. Walitakiwa wamuache aendelee tu. Kama angeshinda, basi CHADEMA ingehitaji kumpa msaada wowote ambao angehitaji ili kuweza kukifikisha chama mahali ambapo wote wangetamani kifike. Kwani chama kinaendeshwa na mtu mmoja? Sijui owoga wao ulisababishwa na nini hasa. Anyway, hali imekuwa kama ilivyokuwa sasa.
Tatizo ninaloliona ni kauli za Zitto Kabwe baada ya yote hayo kutokea. Kauli za kuvujisha siri ambazo zinaweza kukigharimu chama kwa kiasa ambacho yeye na wengi ndani ya chama watatumia muda mwingi na propaganda kubwa kuzifuta. Hizo ndizo tatizo Mkuu wangu.
Chadema yachafuka,mgombea atishia kuchoma kisu, uchaguzi vijana waahirishwaNa Waandishi Wetu
Source: Gazeti la Mwananchi
nashindwa kuanmini kwamba hata Dr. Slaa mpiganai mwingine amewekwa ktk kundi baya halafu mtetezi mkubwa wa Mh. Zitto ktk kikao cha chama ametokea kuwa ni mama yake!.. Hii kweli inaingia akilini mkuu wangu?.. Kuna Ujinga unaendela na sii Zitto mwenyewe ila wapambe wake ndio wanaharibu kabisa!
Wapinzani wake watatumia haya kumbomoa kule Kigoma na hivyo labda anatafuta huruma toka kwa watu. Siwezi kuficha kuwa mambo ya Zitto yametumiza watu wengi. Siwezi kuficha kuwa labda naye anatumiwa katika hili.. huwezi kuja hapa na kutoa tuhuma kama hizi then unategemea nini?? Zitto hivi ndio wewe kweli?? umefikia hatua ya kutoa tuhuma mpaka kwa wakina Mnyika??Itawachukua muda mrefu sana katika kuzifuta hizi.. maana kuna watu wametulia na wanafutilia kwa makini yote haya Zitto ameyataka yeye mwenyewe ndio sababu ya yote haya.
Mkuu, usiache kupiga kura. Maana usipopiga kura wewe, wenzako watakuchagulia viongozi na hutaweza kuwalaumu wakikosea. Nenda tu, kapige kura yako, labda matokeo yatakuwa nafuu.
Ni kweli kuwa Zitto hakuwa na kosa kutaka kugombea nafasi ya uwenyekiti wa CHADEMA. Alikuwa na haki kabisa ya kufanya hivyo. Kosa walilofanya viongozi wa CHADEMA kumuomba atoe jina lake kwenye kinyang'anyiro hicho, ndio kosa baya kidemokrasia. Walitakiwa wamuache aendelee tu. Kama angeshinda, basi CHADEMA ingehitaji kumpa msaada wowote ambao angehitaji ili kuweza kukifikisha chama mahali ambapo wote wangetamani kifike. Kwani chama kinaendeshwa na mtu mmoja? Sijui owoga wao ulisababishwa na nini hasa. Anyway, hali imekuwa kama ilivyokuwa sasa.
Tatizo ninaloliona ni kauli za Zitto Kabwe baada ya yote hayo kutokea. Kauli za kuvujisha siri ambazo zinaweza kukigharimu chama kwa kiasa ambacho yeye na wengi ndani ya chama watatumia muda mwingi na propaganda kubwa kuzifuta. Hizo ndizo tatizo Mkuu wangu.
Kosa lake kubwa ni kuvujisha siri za Chama hata pale ambapo hakutakiwi.na tena inapaswa yeye ndie anajua mengi kuhusu Chadema sasa iweje atoe tuhuma kuhusu CHADEMA na pia ana haraka gani ua uongozi??Mkuu
Zitto hana kosa lolote.
ameweka siri bado ya kuona wenzake yani viongozi wajuu wameweka uhuni na kumwandama kwa shutuma zisizofaa.Kama wao hao viongozi wa juu wangeekuwa na siri ama kuheshimiana wasingesema waliyosema.
Tofauti yako na Zitto ni kuwa Zitto anawafahamu wenye nick names zao wanaomwandama hapa jf ,na wewe huwafahamu .
Labda nitakubaliana na wewe kama kosa la Zitto ni kutumia jina lake halisi na uzuri wa hao viongozi wa juu wanatumia majina ya bandia.
Kosa lake kubwa ni kuvujisha siri za Chama hata pale ambapo hakutakiwi.na tena inapaswa yeye ndie anajua mengi kuhusu Chadema sasa iweje atoe tuhuma kuhusu CHADEMA na pia ana haraka gani ua uongozi??
Wapi Bwana kama unakumbuka ya Chacha Wangwe na leo unasema utasahau baada ya uchaguzi, mimi naanza kukosa imani na wewe. maana si ya Wangwe yalikuwa yameshapita?Ni imani yangu kuwa chama kitakuwa kimoja baada ya uchaguzi. Kimaumbile sina grudges. Tutapiga mstari na kusahau yaliyopita ili kuanza upya.
Tatizo ndugu yangu ni kwamba kama una mambo au jambo la kujibu toka kwa wapinzani wako kuna taratibu fulani za kufuata na sio kama hivi za kuja hapa JF na kuongea na kuandika mambo ya jikoni na kutoa upenyo kwa Wapinzani wako kukusema na kukuadhibu mwakani. CHADEMA wao ndio wanasimamia. na tena kama kuna mtu amedhulumiwa haki yake kama hivi basi kuna mamlaka kamili ya kutoa hukumu na sio kuja na kusema huku JF. Sasa sisi tulikuwa tunamuona Zitto kama Mentor yetu, kweli tunazidi kupunguza imani na mambo yanatokea kwake ikiwa yeye ndio mdau mkuu wa CHAMA.Nani aliyeanza kurusha ma B52.? Ni principle za kidunia ukirushiwa mangumi na wewe una haki ya kujidefendi kwa kurusha ngumi na hata kutoa silaha.Hii ni natural haki inatambulika kote duniani na ktk mahakama zote.
Ukimuuwa jambazi kwa kombora wakati yeye amekuja na lungu kukuvamia nyumbani kwako hutokuwa na makosa mbele ya mahakama zote zilizo huru duniani.
Hii mnayoongea leo kuhusu Zitto labda muiingize leo rasmi ktk uso wa dunia.
Mmemshauri/shurutisha kuachana na uenyekiti ameacha lakini bado hamkuheshimu wakaendelea na griba na kurusha mishale sasa kashusha kombora mnalia lia .alichokifanya zitto ni sahihi kabisa.
- Yale yale aliyoyasema Obama kule Ghana, Africans tuache tabia ya kuwekeza kwenye majina ya viongozi, tujifunze kuwekeza kwenye sound policies hii thread na yaliyojiri ni mfano mkubwa sana wa maneno ya Obama.
In the 21st century, capable, reliable and transparent institutions are the key to success - strong parliaments and honest police forces; independent judges and journalists; a vibrant private sector and civil society. Those are the things that give life to democracy, because that is what matters in peoples' lives... Africa doesn't need strongmen, it needs strong institutions.
Accra speech full text...