Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Hapa kuna issue mbili na zinachanganywa baada ya Mods kuunganisha MADA husika

1. kuna issue ya Zitto na Kugombea Uenyekiti
2. kuna issue ya Uchaguzi BAVICHA

tuyazingatie hayo.........

1.Kwenye issue ya kwanza "Uenyekiti" CHADEMA Wamechemka
2.kwenye issue ya pili "Uchaguzi BAVICHA" Zitto "kafulia"......

Zitto acha Jazba,

Hivi kuondoa jina lako ili usigombee uenyekiti ndio umekiokoa chama? au ulitishiwa KIFO?

Pili, ni kuwa, kama matokeo kwenye uchaguzi wa BAVICHA hayakutangazwa kwa nini uje hapa kusema kuwa una hakika uliyekuwa unamkampenia alishinda....what are you trying to insinuate...........
 
Home
wanafunzi 2,500 zafungwa kwa kukosa vyoo Date::9/1/2009Mama mzazi amtetea mwanaye Zitto Kabwe kuwa ni safi,hahongeki, hanunuliki
broken-heart.jpg
Fidelis Butahe na Mussa Mkama

WAKATI hali ikiwa bado tete ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Shida Salum jana ameibuka katika Uchaguzi wa Baraza la Wanawake (Bawacha) na kudai kuwa mwanaye, Zitto Kabwe sio fisadi kama inavyoelezwa na wafuasi mbalimbali wa Chadema.

Akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilibroad Slaa, mama huyo ambaye ni mwenyekiti wa wanawake walemavu taifa, alitamka wazi kuwa mwanaye ni msafi, hanunuliki, hahongeki wala hatoi rushwa hivyo tuhuma hizo dhidi yake sio za kweli.

Alimtahadharisha Dk Slaa kuwa makini na viongozi wa makao makuu ya Chama hicho akituhumu kwamba baadhi yao ni mafisadi.

"Mheshimwa Katibu mkuu nimeshakufuata sana nikakumabia iangalie ofisi yako ya makao makuu itakuharibia chama na uliniahidi kuwa utalishughulikia lakini matokeo yake ndio haya,"alisema Shida na kuongeza;

"Magazeti yanamtukana Zitto kuwa ni fisadi lakini mimi ninasema kuwa Zitto hawezi kupokea wala kutoa rushwa kwa sababu anajua nini maana ya demokrasia, Katibu inayokuangusha ni ofisi yako ya makao makuu ichunguze."

Akijibu hoja ya mama Zitto, Dk Slaa alisema kuwa ni kweli suala hilo linawezekana lakini akasisitiza kuwa kama ni rushwa ndani ya ofisi yake hata Zitto naye anahusika kwa sababu ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama ambaye kikatiba ndiyo mtendaji mkubwa wa ofisi hiyo.

"Kwa kicheko, nimekuelewa mama Zitto lakini unapozungumza hivyo ina maana unamuweka na Zitto pia maana yeye ndio naibu wangu, Zitto ni mwanao mimi ni naibu wangu sasa sijui niamue vipi, lakini hayo yote tuyaache mimi kama Katibu nitayafanyia kazi kwani tuliahidiana kutooneana haya wala kulindana hata kama mhusika anazungumza sana Bungeni," alisema Slaa na kuongeza.

"Ninaposema kuwa chama kimeingiliwa na mafisadi sina maana kuwa Zitto ndiyo fisadi bali nawalenga wale wote wenye tabia ya kifisadi ndani ya chama pamoja na wale wanaotoka nje ya chama na kuleta ufisadi wao ndani ya chama."

Awali akifungua Mkutano huo wa (Bawacha), Slaa alisema kuwa amepata ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwa wajumbe kupitia simu yake ya mkononi kuwa kuna wagombea wamepenyeza rushwa kwa baadhi ya wajumbe ili waweze kuchaguliwa na kuwaonya kuwa wakigundulika watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.

"Kutokana na hili nitaleta maofisa kutoka Takukuru ili wapambane na vitendo hivi vya rushwa kwa sababu moja ya vita kubwa ya Chadema ni rushwa, nitafanya hivi kwa kulinda demokrasia ndani ya chama atakayeshikwa na Takukuru shauri yake" alisema Slaa na kuongeza

"Mimi pamoja na wenzangu tumewataja walaji rushwa ndani ya serikali hatuwezi kushindwa kuwataja na kuwachukulia hatua wale wote wanaoendekeza rushwa ndani ya chama chetu, lakini pia ninawaonya wale wote wanaosema Slaa na Mbowe wanakula rushwa asimame na asema tena akiwa na ushahidi."

Slaa akizungumza kwa jazba aliwataja maadui watatu wa Chadema kuwa ni Usalama wa taifa, Chama cha Mapinduzi(CCM) pamoja na vyombo vya habari vinavyotumiwa na mafisadi.
"Usalama wa taifa kuna gazeti moja wanalitumia kwa ajili ya kuichafua Chadema tunalijua, lakini pia lipo gazeti ambalo mimi mwenyewe nilimtaja mmiliki wa gazeti hilo kuwa ni fisadi Septemba 15 mwaka 2007 kwa hiyo sikushangaa lilivyoanza kuniandika vibaya kwa hiyo na hili linatumiwa," alisema Slaa na kuongeza

Mkuu wewe ulipoenda Kyela na jina lako lilipokuwa likitajwa sisi tulikutetea na haikutosha uikaingia Mwenyewe kujibu hoja mbali mbali.

Zitto alidhalilishwa na watu wa Mbowe kwa kuleta habari ya uongo,majungu,dharau na uzushi juu ya ushiriki wa Zitto na Mama yake kwenye uchaguzi wa vijana.maneno yale bila ya Zitto kuja kuyakanusha yangezidi kuvuruga jina lake. unataka akae kimya hadi lini. tarehe 26 mwezi huu KIBANDA kaandika makala chafu kwenye gazeti la MBOWE TANZANIA DAIMA. jumapili hii tarehe 30 akaja NGURUMO kutia msumari kupitia gazeti hilo hilo. Zitto akawa kimya tu.

leo hii wamekuja kwa kumuingiza mama yake mzazi.Zitto sio Mtume au malaika ana kiwango cha kuvumilia. wewe mbona unamchafua Mwakyembe kwanini usinyamaze? mie nilifungiwa kwa kukutetea wewe wiki nzima ulipokuja hata kunipa pole umeshindwa.

Kweli binadamu hatujioni.

Zitto jibu kadri inavyowezekana. wao wamewatumia KIBANDA,KWAYYU NA NGURUMO kukuchafua kwa wajumbe wa mkutano mkuu, sasa wameumbuka pamoja na yote hayo Kafulilla kapiga bao.

Umenifurahisha thats why I like JF!

Wakati naona wana JF wengi wakitapatapa na kuzika hadhi ya jamvi ya kukos kufikiria in 3D naona bado JF imesimama palepale, hivyo kuwaacha baadhi ya watu kuwa SIO GREAT THINKERS na wanabaki kubonya keyboard, hawana msaada!

Kama material basi Zito alianza kwenye elastic kaenda kwenye plastic na sasa ame-collapse

kama ulivyosema kila kitu wamemzuishia Zito!

1. Kuwa anatumiwa na CCM, hii wamesema wengi wakiongozwa na babu mtei
2. Hao akina kibanda na akna Ngurumo(maskini nime-mdevalue huyu)

3. Leo wanangiza familia yake

mnataka yoooote hayo akae kimya kana kwamba yeye ni CHUMA

HAWA WASIOPENDA MABADILIKO YA KWELI WAKIFANYA HIVI KESHO WATARARUA FAMILIA YA SLAA na kubaki ona sasa, kesho wataenda kwa MKJJ, na wale wapiganaji wooote, ikifika mda JF IKAKOSA KUWAZA KWA NAMNA HII (japo pengine siko sahihi) nachelea kuwa vita hii bado sana!

adui anaweza kuja kwa namna yeyote akigusa familia cha bwana, mama yake yuko CHADEMA tangu 1992, hakuwahi kuwa na tuhuma za ufisadi na kurubuni wapiga kura, ila hii imetokea leo wakati Zito alitaka kugombea uenyekiti??

Jamani ebu tuamke, tuache ushabiki usiotufikisha katika lengo!

- Inachekesha sana kwa mtumzima kama wewe kuleta habari za Malecela, wakati
Zitto anaongelea habari za jinsi alivyoshirikiana na wenziwe huko Chadema kumuuua Wangwe,

- unajaribu kutetea Zitto kuenguliwa nje ya vikao vya chama badala ya kugombea il, ashindwe kwenye uchaguzi, unasema ni jambo la kawaida huku ukiwa unajua kabisa kwamba ni tabia mbaya sana ya CCM iliyotufikisha hapa tulipo yaani taifa la Banana Republic, unajaribu kwa nguvu zote kutetea huku ukitumia mifano ya upuuzi wa CCM, and you think you are making a sense,

- Hivi ni lini umesikia rais wa US ameondolewa nje ya uchaguzi wa kidemokrasia, mmelichemsha sasa mlinywe wenyewe CCM has nothing to do with it hili kama la wangwe ni lenu wenyewe na ni aibu sana, demokrasia inadai Zitto aruhusiwe kugombea kama kushindwa akashindwe kwenye kura za wananchi sio busara za wazee wanaogawana ruzuku za chama,

- Kama kweli Chadema mnajali demokrais makini basi mpeni nafasi Zitto agombee, hili halina mjadala wala compromise, na hamtaweza ku-recover from this ugly political mistake, sasa tumeelewa kwamba hicho ni cahma cha wachache sana ambao kugombea kwa Zitto kumetishia mlo wao yale yale ya kina Karamagi, sasa mnajionyesha rangi zenu rasmi kwamba hamna cha demokrasia wala umakini, ni wababaishaji tu kama yale mafisadi ya ndani ya CCM,

Kama kweli mnajali demokrasia basi waaambieni viongozi wenu wamruhusu Zitto kugombea kama hamuwezi acheni na hizi spin za kitoto za kulinganisha Zitto na Malecela, kwa sababu ni aibu sana kwa watuwazima, JF hatujawahi kuogopa mtu wala jina au chama, licha ya baba wa mtu yoyote hapa huwa tunapiga mawe tu mmelichemsha sasa mlinywe kama ni spin Zitto atawachafua sana na hamumuwezi, si unaona so far anayoyafanya mamluki wa demokrasia, mnafikiri mnaweza kutudanganya hapa watuwazima, mmelikoroga sasa mlinywe la moto!

Kama kweli nyinyi ni demokrasia makini mruhusuni Zitto agombee, kama hamuwezi basi nyamazeni kama mafisadi wa ndani ya CCM, wao huwa hawasemi sana huwa wana vitendo tu, Chadema mmetuabisha sana na kutukatisha tamaa wananchi ulio wengi, kumbe mko sawa na CCM tu!

Respect.

FMEs!

Respect, umebeba JF we need people like you, however Zito alimaanisha kumsingizia Wangwe kuwa ni fisadi na sio KUMUUA! najua ulikuwa safari
 
Nafikiri Malecela hakuondolewa jina lake ila mafisadi walipiga kampeni za kifisadi akatolewa kwa kura ktk round ya mwanzo.Habari ndiyo hiyo.

Mwaka 1995 Mzee Malecela alijitoa kwenye uchaguzi. Inasemekana ni baada ya kuambiwa atoe jina lake na mwalimu Nyerere.
 
Field Marshall Es,
Inachekesha sana kwa mtumzima kama wewe kuleta habari za Malecela, wakati Zitto anaongelea habari za jinsi alivyoshirikiana na wenziwe huko Chadema kumuuua Wangwe,
Haya sasa unaingia na gear nyingine kabisa ktk kuspin issue tunayozungumzia.
Wapi Zitto kasema alishiriki ktk mbinu ya kumuua Wangwe?...hivi kweli wewe unamtendea haki au unamchulia zaidi!
Mimi ndo nimemuuliza Zitto atuambie kilichotokea haswa ikiwa yeye ameamua kusema ukweli wote na sikumaanisha kwamba Chadema na Zitto walifanya mbinu ya kumuua Wangwe. Nimetaka kujua ukweli wote maadam yeye kaamua kuanika kila kitu hapa JF.

Pili, unapotumia mtazamo wangu ni bora zaidi upinge hoja yangu kwa hoja siii swala la CCM na upuuzi wake. Nimesema vyama vyote duniani vinaweza kuengua jina la mtu hii haina maana Zitto alienguliwa kwa sababu hizo hizo. Ila nachosema Demokrasia ni pamoja na mgombea kukubali kutopitishwa jina lake la wazee wa baraza kutokana na katiba ya chama husika..Mtu yeyote anaweza chukua form ya kugombea Urais iwe Marekani, UK, Caanda na hata Uchina lakini jina lake linaweza enguliwa ikiwa mtu huyo hana sifa, hakutimiza masharti au amekiuka baadhi ya kanuni na sheria za uandikishaji.

Ni jambo la kawaida kabisa, na mtu kama Zitto alitakiwa kuwa mvumilivu, kuheshimu na kukubali matokeo au kufuatilia swala zima kwa kutumia misingi ya sheria inayoambatana na kukata rufaa au kutoa lawama zake. Mzee Malecela alifanya hivyo na heshima yangu kwake nitampa pale aliposindwa kukipaka chama kizima kwa sababu yeye kaenguliwa. Sikuandika kitu chochote kinachohusiana na ubabe wa CCM ila hekima alotumia Mzee Malecela na hata Mzee Sitta kuonyesha kukomaa kwa wanasiasa hao. Chama ni mjumuiko wa watu wa kila aina hivyo issue sio chama hapa ila mhusika anaweza vipi ku handle issues kama kiongozi alokomaa kifikra.

Mkuu wangu hapa tunazungumzia MTU na maamuzi yake na sio chama..Napinga sana yaliyomkuta mzee malecela kwa sababu naelewa kilichofanyika. Na napinga kuenguliwa kwa Zitto ktk kugombea Uenyekiti lakini maadam yeye alikubali kuondoa jina lake ina maana alikubali kujitoa kwa mujibu wa sheria au ushauri wa baadhi ya watu. Kitendo cha yeye kujitoa wakati bado akiwa na hasira inaonyesha wazi hakuwa mkweli.

Tofauti na Wangwe on the otherside alihakikisha haki yake anapewa na nadhani hata Zitto mwenyewe aliwahi kupinga kuwepo kwa njama dhidi ya Marehemu.. leo hii ndio kwanza tunajua ukweli wa mambo yote baada ya mkuu Zitto kupandisha mashetani yake.

Tatizo sii kuupata ukweli ila nashangaa tena kwamba huyu mtu siku zote alikuwa kimya wakati Wangwe akifanyiwa unyama wote na yeye mwenyewe anakiri kuwa mshirika, leo inatokea kwake ndio ukweli tunakuja upata akiwa mshirika wa mbinu chafu against Marehemu.
Ni mchanganyiko wa mambo yote haya ndipo napohoji dhumuni la mheshimiwa
Zitto kama kweli ni kwa maslahi ya chama au yake mwenyewe binafsi. Mandingo wanasema - Chicken has come home to roost! Ukiwa ktk mbinu ya kumuengua mtu ktk kiti cha makamu mwenyekiti, kumbuka malipo yake yanaweza kuwa hapa hapa duniani na hivyo kulalamika kwa Mheshimiwa Zitto hakuwezi kumsafisha hata kidogo ila kinaharibu jina zima la chama.

Wewe kama mwana CCM unafurahia haya yanayotokea na utasema sana kumwita Zitto a hero kwa sababu unataka Chadema wanakwisha..Siku zote wewe mwenyewe husema Siasa ni mchezo mchafu. Unaelewa fika rafu ambazo CCM hutumia na mara zote umekuwa nyuma ya rafu hizo ukiwaambia Chadema wao wanshindwa kipi kucheza rafu mpira wa mchangani usokuwa na refa.
Mimi sii mwanasiasa na nitasema ukweli kwamba ndio sababu kubwa inayonifanya nisiwe mwanasiasa kwa sababu Siasa ni UONGO unaokubalika. Ukiwa mkweli siku zote ktk siasa U will fail na hakuna kitu kibaya ktk makundi haya ya siasa kama Panya (rat) ambaye ni mwepesi wa kuropoka na kusema siri za chama ukidhani ndio ukweli...

Mkuu wangu tunazungumza kila siku na tunafahamiana zaidi ya miaka 30 lakini hata siku moja sijakusikia uki lalamika kuhusu mkeo au familia yako. Hii haina maana ndoa yako ni shwari lakini unajua fika kuwa mimi sii solution pamoja na kuwa mshikaji wako. Swala la ndoa yako ni nje ya ufahamu wangu kabisa isipokuwa tu pale panapojenga urafiki wetu na ndoa yako. Sitakiwi wala sipaswi kuelewa kitu kama kuna matatizo mazito, wapo watu na vyombo ambavyo vitaweza ku solve matatizo ya ndoa yako sii mimi..

Na kibaya zaidi ni pale utakapo nieleza ubaya wa mkeo tu ktk kila janga bila kutoa nafasi sawa kwa mkeo kujieleza. hapo utakuwa unaivunja ndoa wewe mwenyewe, njia nzuri na yenye suluhu ni pale pande mbili zitakapo shiriki ktk mazungumzo au upanisho wowote ule.

Zitto anapokuja hapa JF na kukipaka chama anategemea ku accomplish kitu gani?.. sisi tutamsaidia kipi haswa kama sii kuongeza chunvi ktk kidonda!..Mkuu wangu utu uzima ni pamoja na kuwa nahekima ya kupima uzito wa issue na ukaweza kuziwakilisha ipaswavyo. Uwezo huu Zitto hana na hakika ni moja ya sababu ambayo binafsi nisingempa nafasi ya kuongoza chama. Tabia hii pekee ni liability kwa chama na inaruhusiwa kabisa kumuengua mgombea pamoja na kwamba anweza kuwa na umaarufu kwani siri za Vatican hubakia Vatican..That is leadership hakuna unafiki.
 
Last edited:

Zitto Amelewa sifa na hivyo itakuwa vigumu sana kubaki kama alivyokuwa awali. Kuna kila dalili kuwa nguvu fulani ya kutaka kudhoofisha CHADEMA na huku mwenyewe ameshiriki kujenga kwa miaka mingi. Huyu Siyo Zitto tunammjua toka akiwa na Makala Zake akiwa anaandika gazeti la RAI kwa wakati ule. Jamani anapaswa kushauriwa haraka sana na sasa kama ana majeraha mengi. Siwezi amani kama kweli anafanya hivi kwa manufaa ya CHAma chake, Hapana, Sifa zimemlevya tena sana. Zitto badilika Haraka sana la Svyo utaweza kuwa kama Kabour wa Kigoma. Naanza kupata shida na mawazo mengi toka kichwani kwangu.
 
Kwa kweli hata mimi siamaini kwamba CHADEMA ni wale wale...AKINA Mkuchika na makamba......I dont want to believe!! Duh...sasa itabidi next year nisipige kura...

Mkuu, usiache kupiga kura. Maana usipopiga kura wewe, wenzako watakuchagulia viongozi na hutaweza kuwalaumu wakikosea. Nenda tu, kapige kura yako, labda matokeo yatakuwa nafuu.

Friends..I might be wrong..ila mimi mpaka hapa sijaona kosa la Zitto. Kwa sababu kama alivyosema FMES sioni kwa nini CHADEMA waogope kuwapambanisha wananchama wake Zitto na MBOWE..WHY???????????????????

Jamani kama Zitto akikubalika..si ndo demokrasia yenyewe?? KWA NINI WAZEE WA CHADEMA WAOGOPE?

Inasikitisha na inauma sana.

Ni kweli kuwa Zitto hakuwa na kosa kutaka kugombea nafasi ya uwenyekiti wa CHADEMA. Alikuwa na haki kabisa ya kufanya hivyo. Kosa walilofanya viongozi wa CHADEMA kumuomba atoe jina lake kwenye kinyang'anyiro hicho, ndio kosa baya kidemokrasia. Walitakiwa wamuache aendelee tu. Kama angeshinda, basi CHADEMA ingehitaji kumpa msaada wowote ambao angehitaji ili kuweza kukifikisha chama mahali ambapo wote wangetamani kifike. Kwani chama kinaendeshwa na mtu mmoja? Sijui owoga wao ulisababishwa na nini hasa. Anyway, hali imekuwa kama ilivyokuwa sasa.

Tatizo ninaloliona ni kauli za Zitto Kabwe baada ya yote hayo kutokea. Kauli za kuvujisha siri ambazo zinaweza kukigharimu chama kwa kiasa ambacho yeye na wengi ndani ya chama watatumia muda mwingi na propaganda kubwa kuzifuta. Hizo ndizo tatizo Mkuu wangu.
 
Mkuu, usiache kupiga kura. Maana usipopiga kura wewe, wenzako watakuchagulia viongozi na hutaweza kuwalaumu wakikosea. Nenda tu, kapige kura yako, labda matokeo yatakuwa nafuu.

Ni kweli kuwa Zitto hakuwa na kosa kutaka kugombea nafasi ya uwenyekiti wa CHADEMA. Alikuwa na haki kabisa ya kufanya hivyo. Kosa walilofanya viongozi wa CHADEMA kumuomba atoe jina lake kwenye kinyang'anyiro hicho, ndio kosa baya kidemokrasia. Walitakiwa wamuache aendelee tu. Kama angeshinda, basi CHADEMA ingehitaji kumpa msaada wowote ambao angehitaji ili kuweza kukifikisha chama mahali ambapo wote wangetamani kifike. Kwani chama kinaendeshwa na mtu mmoja? Sijui owoga wao ulisababishwa na nini hasa. Anyway, hali imekuwa kama ilivyokuwa sasa.

Tatizo ninaloliona ni kauli za Zitto Kabwe baada ya yote hayo kutokea. Kauli za kuvujisha siri ambazo zinaweza kukigharimu chama kwa kiasa ambacho yeye na wengi ndani ya chama watatumia muda mwingi na propaganda kubwa kuzifuta. Hizo ndizo tatizo Mkuu wangu.
Itawachukua muda mrefu sana katika kuzifuta hizi.. maana kuna watu wametulia na wanafutilia kwa makini yote haya Zitto ameyataka yeye mwenyewe ndio sababu ya yote haya.
 
Chadema yachafuka,mgombea atishia kuchoma kisu, uchaguzi vijana waahirishwa
broken-heart.jpg
Na Waandishi Wetu

Source: Gazeti la Mwananchi

Balantanda, naomba utuweke sawa hii story yako tarehe yake inachanganya kwani inaonekana niya 4/9/09 tuweke sawa tafadhari.

Mods tunashukuru kwa marekebisho yote tunaenda sawa.
 
nashindwa kuanmini kwamba hata Dr. Slaa mpiganai mwingine amewekwa ktk kundi baya halafu mtetezi mkubwa wa Mh. Zitto ktk kikao cha chama ametokea kuwa ni mama yake!.. Hii kweli inaingia akilini mkuu wangu?.. Kuna Ujinga unaendela na sii Zitto mwenyewe ila wapambe wake ndio wanaharibu kabisa!

Mkuu, nadhani hali ilivyo ndani ya CHADEMA kwa sasa, inahitaji busara na utulivu mkubwa sana kuweka mambo sawa. Naamini Dr. Slaa ameona mambo yakienda "dangerously too fast" kuingilia.

Inabidi kwa kweli awe makini sana kuamua jinsi ya kuchukua hatua ambazo wewe na sisi wengine tungependa azichukue. Busara zake pekee ndizo zinazohitajika kwa sasa. Maana inaelekea, hata Baraza la wazee haliaminiwi tena, na Mwenyekiti Mbowe nae hawezi kuaminiwa katika hili. Kwa kifupi, hakuna mtu ndani ya CHADEMA Anaeweza kufanya lolote zaidi ya Dr. Slaa.

Dr. Slaa anatakiwa aangalie kwa makini angle anayoweza kuingilia kwenye sakata hili. Akikosea tu anaharibu mambo moja kwa moja. Nadhani atakuwa anafahamu hivyo kwa sasa.
 
Itawachukua muda mrefu sana katika kuzifuta hizi.. maana kuna watu wametulia na wanafutilia kwa makini yote haya Zitto ameyataka yeye mwenyewe ndio sababu ya yote haya.
Wapinzani wake watatumia haya kumbomoa kule Kigoma na hivyo labda anatafuta huruma toka kwa watu. Siwezi kuficha kuwa mambo ya Zitto yametumiza watu wengi. Siwezi kuficha kuwa labda naye anatumiwa katika hili.. huwezi kuja hapa na kutoa tuhuma kama hizi then unategemea nini?? Zitto hivi ndio wewe kweli?? umefikia hatua ya kutoa tuhuma mpaka kwa wakina Mnyika??
 
Mkuu, usiache kupiga kura. Maana usipopiga kura wewe, wenzako watakuchagulia viongozi na hutaweza kuwalaumu wakikosea. Nenda tu, kapige kura yako, labda matokeo yatakuwa nafuu.

Ni kweli kuwa Zitto hakuwa na kosa kutaka kugombea nafasi ya uwenyekiti wa CHADEMA. Alikuwa na haki kabisa ya kufanya hivyo. Kosa walilofanya viongozi wa CHADEMA kumuomba atoe jina lake kwenye kinyang'anyiro hicho, ndio kosa baya kidemokrasia. Walitakiwa wamuache aendelee tu. Kama angeshinda, basi CHADEMA ingehitaji kumpa msaada wowote ambao angehitaji ili kuweza kukifikisha chama mahali ambapo wote wangetamani kifike. Kwani chama kinaendeshwa na mtu mmoja? Sijui owoga wao ulisababishwa na nini hasa. Anyway, hali imekuwa kama ilivyokuwa sasa.

Tatizo ninaloliona ni kauli za Zitto Kabwe baada ya yote hayo kutokea. Kauli za kuvujisha siri ambazo zinaweza kukigharimu chama kwa kiasa ambacho yeye na wengi ndani ya chama watatumia muda mwingi na propaganda kubwa kuzifuta. Hizo ndizo tatizo Mkuu wangu.

Mkuu
Zitto hana kosa lolote.
ameweka siri bado ya kuona wenzake yani viongozi wajuu wameweka uhuni na kumwandama kwa shutuma zisizofaa.Kama wao hao viongozi wa juu wangeekuwa na siri ama kuheshimiana wasingesema waliyosema.

Tofauti yako na Zitto ni kuwa Zitto anawafahamu wenye nick names zao wanaomwandama hapa jf ,na wewe huwafahamu .

Labda nitakubaliana na wewe kama kosa la Zitto ni kutumia jina lake halisi na uzuri wa hao viongozi wa juu wanatumia majina ya bandia.
 
Kosa lake kubwa ni kuvujisha siri za Chama hata pale ambapo hakutakiwi.na tena inapaswa yeye ndie anajua mengi kuhusu Chadema sasa iweje atoe tuhuma kuhusu CHADEMA na pia ana haraka gani ua uongozi??
 
Kosa lake kubwa ni kuvujisha siri za Chama hata pale ambapo hakutakiwi.na tena inapaswa yeye ndie anajua mengi kuhusu Chadema sasa iweje atoe tuhuma kuhusu CHADEMA na pia ana haraka gani ua uongozi??

Nani aliyeanza kurusha ma B52.? Ni principle za kidunia ukirushiwa mangumi na wewe una haki ya kujidefendi kwa kurusha ngumi na hata kutoa silaha.Hii ni natural haki inatambulika kote duniani na ktk mahakama zote.

Ukimuuwa jambazi kwa kombora wakati yeye amekuja na lungu kukuvamia nyumbani kwako hutokuwa na makosa mbele ya mahakama zote zilizo huru duniani.

Hii mnayoongea leo kuhusu Zitto labda muiingize leo rasmi ktk uso wa dunia.

Mmemshauri/shurutisha kuachana na uenyekiti ameacha lakini bado hamkuheshimu wakaendelea na griba na kurusha mishale sasa kashusha kombora mnalia lia .alichokifanya zitto ni sahihi kabisa.
 
Ni imani yangu kuwa chama kitakuwa kimoja baada ya uchaguzi. Kimaumbile sina grudges. Tutapiga mstari na kusahau yaliyopita ili kuanza upya.
Wapi Bwana kama unakumbuka ya Chacha Wangwe na leo unasema utasahau baada ya uchaguzi, mimi naanza kukosa imani na wewe. maana si ya Wangwe yalikuwa yameshapita?
 
Nani aliyeanza kurusha ma B52.? Ni principle za kidunia ukirushiwa mangumi na wewe una haki ya kujidefendi kwa kurusha ngumi na hata kutoa silaha.Hii ni natural haki inatambulika kote duniani na ktk mahakama zote.

Ukimuuwa jambazi kwa kombora wakati yeye amekuja na lungu kukuvamia nyumbani kwako hutokuwa na makosa mbele ya mahakama zote zilizo huru duniani.

Hii mnayoongea leo kuhusu Zitto labda muiingize leo rasmi ktk uso wa dunia.

Mmemshauri/shurutisha kuachana na uenyekiti ameacha lakini bado hamkuheshimu wakaendelea na griba na kurusha mishale sasa kashusha kombora mnalia lia .alichokifanya zitto ni sahihi kabisa.
Tatizo ndugu yangu ni kwamba kama una mambo au jambo la kujibu toka kwa wapinzani wako kuna taratibu fulani za kufuata na sio kama hivi za kuja hapa JF na kuongea na kuandika mambo ya jikoni na kutoa upenyo kwa Wapinzani wako kukusema na kukuadhibu mwakani. CHADEMA wao ndio wanasimamia. na tena kama kuna mtu amedhulumiwa haki yake kama hivi basi kuna mamlaka kamili ya kutoa hukumu na sio kuja na kusema huku JF. Sasa sisi tulikuwa tunamuona Zitto kama Mentor yetu, kweli tunazidi kupunguza imani na mambo yanatokea kwake ikiwa yeye ndio mdau mkuu wa CHAMA.
 
- Yale yale aliyoyasema Obama kule Ghana, Africans tuache tabia ya kuwekeza kwenye majina ya viongozi, tujifunze kuwekeza kwenye sound policies hii thread na yaliyojiri ni mfano mkubwa sana wa maneno ya Obama.

Kweli Mkuu, CHADEMA wameharibu mambo kweli kweli safari hii, ila tuelekezane kidogo hapo Mkubwa: Obama hakusema tujifunze kuwekeza kwenye "siasa safi." Obama alisema tuwekeze kwenye kujenga "taasisi imara."

Akimaanisha - na aliorodhesha na kuanisha anachomaanisha - mabunge huru, vyombo vya dola vilivyo safi (polisi wasiokula rushwa, akatoa mfano), mahakama na vyombo vya habari huru, asasi za kiraia zenye nguvu; kifupi taasisi zilizojengwa katika misingi ya, na zinazodumisha, demokrasia.

Kinachofanyika CHADEMA kwa sasa sio kwamba ni kuwekeza katika watu, bali kinaweza kuwa ndio hiyo struggle ya kujenga taasisi za kidemokrasia. Dr. Slaa (Mb.) anapobatilisha matokeo ya uchaguzi, Zitto K. (Mb) anamwambia mbona ni Kamati Kuu ndio ina mamlaka hayo na si wewe? Mbona katibu umejiamulia kutotangaza matokeo kivyako, kwani katiba inasemaje? Kwa hiyo Zitto yuko sawa kwa hilo ( japo anakosea anapolumbana na kunyosheana vidole na wenzake bila tact, akiwemo mwenyekiti wake) alichojaribu kukifanya kinaendana na alivyoshauri rais wa Marekani akiwa Accra, tuwekeze kwenye misingi ya taasisi za kidemokrasia, kufuata utawala wa sheria, Katiba, sio fikra za Katibu wala "siasa safi" za mwenyekiti!

In the 21st century, capable, reliable and transparent institutions are the key to success - strong parliaments and honest police forces; independent judges and journalists; a vibrant private sector and civil society. Those are the things that give life to democracy, because that is what matters in peoples' lives... Africa doesn't need strongmen, it needs strong institutions.

Accra speech full text
...
 
Hii katuni (Babatau) nadhani inatoa ujumbe mzito kwa Chadema:​

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom