Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Inapaswa kuwa makini sana katika wakati huu na pia sioni sababu ya kufanya hivi mambo kama haya bwana. lakini yote lazima watu tuyajue na tuchukue hatua haraka sana
 


Mkuu wao ndio wameanza kuja hapa jf,wao ndio hawakufuata taratibu ,kwanini hawakumuita zitti huko kwenye ze said utaratibu wa chama na kumweleza hayo mambo yake ya kifisadi??

Rudi nyuma kidogo kasome post kuanzia mwanzo Zitto amemtaja memba humu na kusema anamfahamu kuwa ni nani huko chadema ,ndipo zitto naye akanza kushusha bakola.

Waambie kwanza hao chadema wafuate utaratibu.Mkuu nimekuuliza kosa la zitto ni kutumia humu jina lake halisi.?
 
Hata kama angetimia jina la vichochoroni But the way uandishi wake ulivyo tungejua kabisa kuwa ni yeye. Hivyo Mimi kikubwa nasema kuwa yeye ni kiongozi mkubwa ndani ya CHADEMa na hivyo wanavyoboronga wote wanashiriki na mambo yaliyoandika hapa angepaswa kuyasema ndani na sio kuyamwaga hapa. Sisi hutuwezi kushuhudia CHADEMa ikipelekwa kama hivi wanavyotaka kwenda na kuomba huruma toka wa watu
 

Dah! jamani? si tulisema? mkafikiri tuna chuki,sasa hiyo ndo chadema chama m-badala.
Maelezo ya kamanda Zitto yanaeka wazi kuwa chadema :
- Rushwa- kwenye uchaguzi na inaonekana na hata chaguzi za nyuma.

- Democras- Zitto kaenguliwa,kafulia ndo huyo hapewi ushindi wake tena kwa mara ya pili.

- Ufisadi- hapo Zitto alipowaonya kuwa ukimaliza uchaguzi kuna ukaguzi wa mahesabu tena unafanywa na CAG.

- Udicteta- Kiongozi anatoa maaumuzi peke yake,kwa mfano hapo imeonesha dr slaa,na kulazimishana kujiondoa ktk chaguzi,kunyimwa ushindi.

- Makundi- hapo tumeona watu wanavotuhumiana hadharani kabisa,sasa haya ya juu,jee ya ndani.

- Maslahi binafsi- Hapo tumeona jinsi kila moja anavojitetea kwa maslahi yake badala ya chama,na wengine kusema wanang'ara zaidi kuliko wengine

- Siri- Chama hakina siri,watu wanaropoka tu,utafikiri hakuna uongozi ndani ya chama au hakuna kanuni madhubuti.

- Katiba- Katiba haifuatwi kabisa,kila mmoja anaamua vile ambavyo wanaona bora kwao,na hasa hili kundi la kina Nyere wa pili,kina Mtei..

- Majungu- chama kimejaa majungu mpaka viongozi wa juu,inaonesha wazi viongozi ni dhaifu mno na kunaonesha kama viongozi hawajakomaa kielimu kutokana na hili.

JAMANI,JAMANI CHADEMA NDO HII. Sijui wapi tunakwenda. Naona Lwakatare simsikii?
 
 

hoja yangu mbona hao walioanza hawakuyapeleka huko ndani ya chama,na huyo mzee mtei kapanda public ama hilo nalo ni gumu kuliona.?

jf ni chombo cha habari kama kilivyo chombo chochote ambacho mtei alipanda nacho hewani, na afterall sio zito alianza kuleta haya mambo hapa jf na badala yake unamshauri ayapeleke huko kwa ambao wao ndio hao walioanza kuyaleta hapa jf.

Mkuu sikuelewi una maanisha nini,naomba ufafanuzi zaidi.
 
hawa jamaa kwa kweli wako poa sana,ni chama ambacho kwa kweli hata wengine ambao tunaona siasa ni chafu tunaweza tukajiunga nao.
Kuweni makini chadema,jiepusheni na mamluki.

wish you all the best chadema
 
tutataka wakaee ndani na waongee na sio kuja hapa kuandika kama hivi
 

Nadhani wazee wa chadema waliliona hili. Kijana bado hajakomaa na hivyo wasingeweza kumwamini kumpa chama akiongoze (hata kama ana umaarufu!).
 

Kaka kama mambo ndiyo haya, kama ndivyo mnavyojibizana kwenye vyombo vya habari, nasikia harufu ya ile NCCR ya Lyatonga Mrema! Panapofuka moshi pana moto kaka, hapo kwenu mkichelewachelewa yatakuwa masizi!
 
Nadhani wazee wa chadema waliliona hili. Kijana bado hajakomaa na hivyo wasingeweza kumwamini kumpa chama akiongoze (hata kama ana umaarufu!).
Mimi Nasema kuwa Zitto ni mwanasiasa mzuri but sasa amelewa sifa na bado kuongoza CHADEMA ila huko mbele kama akijirekebisha basi itakuwa neema kwake,
 

Kaka Zitto nakata tamaa sasa! Hata wewe ulishiriki kumtenda Chacha Wangwe? Na ungamo hili limekutoka katika mwezi huu mtukufu nina uhakika ni kweli umeshiriki kumfanyia ubaya Chacha kama ulivyokiri mwenyewe. Kama ulivyokiri mwenyewe, Mwenyezi Mungu akujalie msamaha kwa toba yako katika mwezi huu mtukufu.

Lakini nimekata tamaa kabisa na CHADEMA yenu.
 
Mama Zitto afyatuka, uchaguzi Chadema wafutwa

Mwiba naomba ukiwa una quote gazeti basi tuletee na jina la gazeti ili tuchambue ni gazeti la nani tafadhali. Samahani ingawa wewe humu ni mzoefu ila ni angalizo.
 
Zitto, acha kuandika uongo na kuaminisha umma juu ya matokeo ya vijana .
Matokeo na ambayo ulikuwa nayo wewe kwani ulikuwa meza kuu na mimi sikuwepo meza kuu ni haya;
David Kafulila = 99
John Heche =83
Dady Igogo= 11
Julieth Rushuli= 11.

jumla zilikuwa kura 204.

Idadi ya wajumbe halali walikuwa ni 164.

Naomba uweke rekodi sahihi na ukijua kuwa kusema ukweli daima ndio njia ya kuweza kujenga, umelaumu sana Mrema na Mnyika hata unafikia mahali pa kudanganya.

Waseminari wana kauli moja kuwa ukweli ni mmoja na haugawanyiki.

naomba niishie hapo kwa leo na nitakujua kujibu mengine yote dhidi yangu siku zijazo .

Nawatakia mjadala mwema.
 
Ndio maana mimi napata shida sana kuona hali kama hii kutoka kwa Zitto na Kundi lake. Hivyo yeye badala ya kusimamia na kufanya kuwa makini na karibu sana na viongozi wake wa karibu na kufanya mambo ya ndani ya chama na siyo humo ndani JF. sisi kama Wasau hali hii inatuudhi sana na kutufanya kuchanganyikiwa hata kumuumiza roho zetu
 
uchoma kisu, uchaguzi vijana waahirishwa

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Dkt Willibrod Slaa akizungumza na waandishi wa habari akiwa pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe kuhusu muelekeo wa uchaguzi wa baraza la vijana Taifa.
Na Waandishi Wetu
HALI ya kisiasa ndani ya Chadema imezidi kuchafuka baada ya uchaguzi wa Baraza la Vijana Taifa (Bavicha) kuahirishwa kwa miezi sita, huku mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo (jina tunalo) akitishia kumchoma kisu mwanachama anayeaminika kuwa kambi ya naibu katibu mkuu, Zitto Kabwe.

Wakati hatma ya uchaguzi huo ikiwa bado njia panda, mizengwe imezidi kutikisa uchaguzi wa Jumuiya ya Wanawake baada ya mmoja wa wagombea anayeaminika kuwa upande wa Zitto kunusuruka kung'olewa.

Joto zaidi linaloonyesha hali tete ndani ya Chadema, lilipandishwa na hatua iliyotangazwa jana mchana na katibu mkuu, Dk Wilbrod Slaa ya kuahirisha uchaguzi huo hatua ambayo ilipingwa na Zitto na msemaji wa chama hicho David Kafulila ambao wanataka kutangazwa kwanza kwa matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika juzi na kuitishwa kikao cha dharura cha Kamati Kuu (CC), ambacho inasemekana kinafanyika leo.

Wagombea waliokuwa wakiwania nafasi ya uenyekiti wa Bavicha ni John Heche, Dadi Igogo na David Kafulila ambaye licha ya kuwa ofisa habari wa chama hicho, anatarajiwa kuwania ubunge Jimbo la Kigoma Kusini mwaka 2010.

Akitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi huo jana, Dk Willibrod Slaa alisema uchaguzi huo utafanyika ndani ya miezi sita ijayo.

“Mimi kama katibu nimeshauriana na kamati ya wazee ya chama nikiongozwa na Mzee (Edwin) Mtei, Bob Makani na Balozi (Christopher) Ngaiza tumeubatilisha uchaguzi huo, hivyo utafanyika ndani ya miezi sita ijayo,” alisema Slaa.

“Tumeamua hivi kwa sababu kwanza kufanya uchaguzi ni gharama, tunatumia karibia Sh50 milioni ambazo zinaweza kujenga zahanati moja. Jamani hapa tutawaeleza nini Watanzania.

“Wajumbe walidai kuwa uchaguzi ulijaa rushwa, lakini niliwambia waandike malalamiko kwa maandishi na ujumbe mfupi na wamenipatia nitayafanyia kazi na yatatolewa maamuzi na vyombo husika.”

Lakini Zitto alipinga uamuzi huo akisema katibu mkuu hana mamlaka ya kutoa tangazo hilo na kwamba nanlaka hayo ni Kamati Kuu (CC).

"Lakini pia, chombo pekee chenye uwezo wa kufanya uamuzi huo ni Kamati Kuu, sasa inakuaje chombo kingine kichukue uamuzi tena bila matokeo kutangazwa wala mgombea kukata rufaa," alisema Zitto.

Alifafanua kuwa uamuzi huo umetokana na baadhi ya watu kukataa matokeo hayo baada ya kuweka mbele maslahi binafsi badala ya maslahi ya chama kwa kuwa jambo la msingi katika suala hilo ni matokeo hayo kutangazwa kwanza kabla ya kuahirisha uchaguzi.

"Jambo la kwanza ni kutangaza matokeo na baadaye kama kuna mgombea alikuwa akipinga, anaweza kukata rufaa, lakini matokeo hayajatangazwa wala hakuna aliyekata rufaa," alifafanua Zitto.

Kutokana na utashi wa katiba, Zitto alisema tayari amemwomba katibu mkuu kuitisha mkutano wa CC kujadili suala hilo.

"Nimemwomba Dk Slaa aitishe kikao cha Kamati Kuu tujadili hii hali maana kama viongozi hatutakuwa na busara na chama kitavurugika," alionya.

Alipoulizwa nini mustakabali wa Chadema kutokana na matukio hayo ya vurugu yanayotikisa chama, alijibu: "Viongozi tusipotumia busara chama kitavurugika, lakini tukitumia busara na kuweka maslahi ya chama mbele, tutaweza kutatua haya mambo kwa urahisi."

Zitto alihoji: "Kwanini wazee wasitumie busara kama walizotumia kuniomba mimi nijitoe kwa kutaka wagombea wengine wajitoe au wakubali matokeo kwa kumwachia Kafulila?

"Tukiwa na busara; tukiheshimu demokrasia, tutaweza kuvuka salama. Naamini hilo tu ndiyo suluhisho la kukivusha chama salama."

Naye Kafulila alipinga uamuzi wa kuahirisha uchaguzi kabla ya kutangaza matokeo akisema anataka kutangazwa kwanza kwa matokeo ambayo anaamini, yalimpa ushindi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kafulila alisema haoni sababu ya kutotangazwa kwa matokeo hayo ambayo anaamini alishinda licha ya kutokubalika na sehemu kubwa ya wajumbe wa sekretarieti na wabunge wa viti maalum.

"Ukiangalia hata hayo mambo ya karatasi kuongezeka, utaona labda ulikuwa ni mpango maalumu wa kumwangusha mtu fulani, lakini imeshindikana," aliongeza.

"Kwa kifupi, sikubaliani na uamuzi huo ninachotaka kwanza matokeo yatangazwe na pia baraza halina mamlaka hayo. Hiyo ni kazi ya Kamati Kuu."

Habari zinadai kuwa tangu John Mnyika kuondoka kwenye wadhifa wa uenyekiti wa vijana wa Chadema, kumekuwa na mkakati wa kumdhibiti Kafulila unaofanywa na baadhi ya vigogo wa Chadema kutokana na mgombea huyo kuonekana mwiba kwao.

Kafulila anasemekana kuwa ni mtu anayepinga waziwazi mambo yanayoendeshwa kinyume na taratibu na amekuwa hahofii viongozi wa juu yake kueleza msimamo wake.

Wakati hayo yakiendelea, vurugu zaidi zimezidi kutikisa chama hicho na jana zilifikia katika hatua ya mgombea mmoja wa nafasi ya uenyekiti wa vijana kutaka kumchoma kisu mwanachama ambaye alikuwa akimtetea Zitto Kabwe asitukanwe na mgombea huyo.

Kabla ya kufikia hatua ya kutishiana visu, mgombea huyo alikuwa akibishana na baadhi ya wafuasi wa Kafulila kwenye ofisi za makao makuu ya Chadema zilizo Kinondoni jijini Dar es salaam.

Wakati Mwananchi inafika kwenye ofisi hizo majira ya saa 7:00, vurugu zilikuwa zimeshapoa tangu saa 5:00, lakini wanachama walikuwa wamekaa kwenye vikundi wakijadili matukio mbalimbali ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mgombea huyo na mwanachama mmoja anayedaiwa kuwa anamuunga mkono Kafulila, walirushiana ngumi kwanza na baadaye ndipo mgombea huyo alipotoa kisu na kumtishia.

Mashuhuda hao walidai kwamba mara baada ya mgombea huyo kutoa kisu, wanachama wengine waliokuwa karibu waliingilia kati na kumtoa eneo hilo.

Mwanachama anayedaiwa kutishiwa kisu aliiambia Mwananchi kuwa alikuwa akimsihi mgombea huyo kuacha kumsema vibaya Zitto kwa kuwa malalamiko yote ya uchaguzi wa juzi yako ngazi za juu za chama hicho.

Mwanachama huyo alifafanua kwamba baada ya kumwambia mgombea huyo maneno hayo, alipandisha ghadhabu zaidi na kuanza kutukana.

“Sasa mimi nilivyoona anamtukana Zitto, nilimwambia aache lakini hakusikia; alikuwa anasema Zitto wako na Kafulila walishirikiana kumwibia kura. Kutokana na kuendelea kuongea ovyo, tulishikana na alivyoona muziki ni mnene alinitolea kisu na kutaka kunichoma,” alidai.

Katika hatua nyingine, Dk Slaa juzi alilazimika kurudi katika ukumbi wa uchaguzi wa Bavicha mnamo saa 6:20 usiku ili kutuliza ghasia zilizoibuliwa na wajumbe mara baada ya kupata habari kuwa kura 20 ziliongezeka katika nafasi ya mwenyekiti.

Wajumbe hao ambao walionekana kuwa upande wa mgombea wa nafasi hiyo, John Heche ambaye ni diwani wa Tarime Mjini, walipinga matokeo kabla hayajatangazwa hali iliyomlazimu msimamizi wa uchaguzi huo, Charles Mwera, ambaye pia ni mbunge wa Tarime, kutoyatangaza.

Dk Slaa, ambaye aliondoka kwenye ukumbi huo juzi saa 7:00 mchana, alirejea kwa mara ya pili saa 6:20 usiku, vurugu zikiendelea baada ya Heche kumpiga ngumi mbili ofisa wa kurugenzi ya uchaguzi ya Chadema, Ali Chitandana na kumlazimu kufanya kazi kubwa kuzituliza.

“Jamani wajumbe nawaomba muwe watulivu kila kitu kilichotokea nimepewa taarifa na Mnyika, kwa hiyo kama kuna mtu ana malalamiko ayaandike na kuyawasilisha makao makuu ya chama kesho (jana) asubuhi ili niyafanyie kazi,” alisema Dk Slaa.

Katika hatua nyingine, wajumbe hao walimweleza wazi Dk Slaa kuwa hawajalipwa fedha zao za posho hali iliyomlazimu katibu huyo mkuu kumwagiza Mtunza Fedha kuwalipa wajumbe hao kutoka mikoa mbalimbali nchini usiku huohuo.

“Wewe Mtunza Fedha walipe wajumbe posho zao; jamani nimeshamwagiza atawalipa wote ila wale ambao wameshakata tiketi kwa ajili ya kusafiri watarudishiwa fedha zao kesho (jana) kwa sababu hamuwezi kuondoka kwa kuwa uchaguzi huu unaweza kurudiwa, lakini yote yatajulikana mara baada ya viongozi kukutana,” alisema Dk Slaa.

“Kwa kweli, nimesikitika sana hiki kitendo kilichotokea leo ni aibu kwa chama. Hapa wapinzani na magazeti yatapata pa kusemea.

Hiki chama ni cha demokrasia; nahitaji kujua kila kitu kilichotokea ili vifanyiwe maamuzi na yeyote atakayebainika kuhusika kwa namna moja au nyingine atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa katiba ya chama.”

Habari hii imeandikwa na Ramadhan Semtawa, Fidelis Butahe, Musa Mkama na Fred Azzah

Hapani shindwa kumuelewa Dr.Slaa uchaguzi unapoalishwa lazima kuwe na sababu na ili sababu ziwepo ni kutaja matokeo ili kutoa nafasi kwa wale wasiokubaliana na matokeo kukata rufaa.Nashindwa kuelewa Mh.Dr.Slaa anaposemo uchaguzi utafanyika katika kipindi cha miezi 6 kwa sababu gharama za uchaguzi ni kubwa 50millioni wananchi hawatatuelewa nikwanini katika kipindi hiki ambapo wajumbe wote wamekusanyika usitafutwe utaratibu wa kurudia uchaguzi huo hii itakua rahisi na kubana matumizi au upepo wa uchaguzi kwa hivi sasa hauko katika muelekeo wa kudi fulani na hilo kundi linategemea ktk kipindi cha miezi 6 litaweza kujipanga.INASIKITISHA MUNGU IBARIKI TANZANIA
 

Kaka haya mambo yanaoneka ni makubwa sana,na yapo ndani kwa ndani,na inaonekana ilikuwa inasubiri siku tu ifike,na ninavoona bado kuna moto mkubwa uwaka ndani kwa ndani,nakumbuka siku moja kuna mdau mmoja humu aliwahi kuongea kuwa kuna moto mkubwa chini kwa chini ktk chadema lkn mmoja mimi nikamdharau,sasa nauona kumbe ni kweli na kwa hali hii hichi chama sasa kinanitia wasi wasi sana kama kipo kweli kwa ajili ya wananchi
 

Haya matokeo mgeyatangaza siku hiyo ,na si kuja kuyatangazia jf.

Mliyatangaza haya matokeo siku hiyo?? hapo ndipo tutaanza kushika mwongo.

Hatudanganyiki tena kauli mbiu kuelekea 2010
 

Nisichoelewa ni kwamba kwanini pale mtu anapokuwa na "siri" za maovu ya serikali au CCM hapa JF tumekuwa na tabia ya kushabikia kwamba hizo sio siri na ni lazima ziwekwe wazi maana hapa we dare to talk openly! Lakini all of the sudden imekuwa opposite kwa sababu Zitto kaleta uozo wa Chadema hapa, tunashabikia kuwa nin siri za chama hatupaswi kujua! It sounds like double standard to me!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…