Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
tatizo sio kutoa siri za chama ....tatizo ni namna alivyozitoa.
ametaja habari ya chacha wangwe baada ya kuonekana na yeye amefanyiwa spinning kama zile .....kwa maana hiyo hakuwa na nia ya kuzisema kama yasingemkuta na yeye.
amesema kuhusu habari ya mahesabu ya chama kwa sababu anataka kuwakomoa wengine ndani ya chama, baada ya yeye kuguswa na vitendo vyao
motive ya zitto ya kuanika siri za chama ndio inatutia wasiwasi.....na sio siri zenyewe
 
 


Kwa yaliyojili mpaka sasa inatosha kutambua kuwa Chadema si chama cha siasa, bali mkusanyiko wa wasanii na wahuni wenye malengo binafsi. I'm sorry to say sioni tofauti kati yake na CCM, in that sense sio chama mbadala! Kama Zitto kakiri kushiriki kumchongea shutuma Chacha Wangwe ni imani yangu kwamba kulikuwa na baraka za viongozi wenzie wa juu including wazee waasisi, kwa maana hiyo sidhani kama kuna msafi hapo! Kumtoa Zitto hakutasaidia kwa sababu uozo unaonekana haujaanzia kwake, ni wengi wameoza na tushukuru conflict zao zimeweza kutufumbua macho na kuona kwamba Chadema ni chama cha aina gani? Na kwanini unaita uozo kama huo siri za chama?Ooh My God, nani atatutoa kwenye utumwa wa CCM?
 

Umesema sawia kabisa! watu wanataka Zitto awe kama punching bag kwa kupokea mashumbulizi tu bila kujibu. Hapa Kaja anaejiita Asha Abdallah na Mpaka Kieleweke ( mmoja mbunge na mwingine kiongozi mwandamizi wa Chadema) wamemtukana Zitto pamoja na mama yake. Zitto kaitwa fisadi mtoa na mpokea rushwa, mrokokaji nk hawa sio na wanachama wa kawaida bali viongozi wa chadema kubwa zaidi baba mkwe Mzee Mtei kanukuliwa na Nipashe akisema mafisadi wamepenyeza pesa kuharibu uchaguzi ( aki maanisha Zitto anatumiwa ) hayo yote yameanikwa hapa jamvini je mlitaka Zitto akawajibu wapi? je hao hawakuwa wanatoa siri?

Zitto yupo sahihi kwenye hili haya mambo ya kufuga ugonjwa mauti yatawafichua chama kinaendeshwa kibabe na kifamilia, watu wana shurutishwa kuondoa majina, bila haya Dr Slaa ( of all people ) anavunja uchaguzi wa vijana bila kufuata taratibu ( hana powers hizo ) halafu mnataka watu wakae kimya?

Hapa JF zimetungikwa nyaraka kadhaa wa kadhaa za siri za serikali na mikataba je watetezi wa siri mlikuwa wapi? vikao vya NEC na CC ya CCM viliivyo wajadili NAPE na SITTA taarifa zilikuwa zinamwagwa hapa wakati kikao kinaendelea watetezi wa usiri mlikuwa wapi?

Kumbe JF inakuwa nzuri pale inaposemwa na kukosolewa CCM tu na sio Chadema.
 


Ndio maana sasa nimeamini kwamba Chadema ni mkusanyiko wa wasanii, wahuni na mafisadi wenye malengo binafsi. Wanapozidiana kete na conflict kuibuka kama sasa ndio sisi tulio nje tunajua what does Chadema mean! Hii ni kesi ya ukimwaga mboga namwaga ugali lakini timing ni muhimu! Damn! CCM part two!
 

Mara zote ukifanya tendo la kishetani ,tatizo la shetani ni lazima aliweke hilo tendo wazi ukiwa bado hai,huwa anakufichia kwa mda tu.
 

Mkuki kwa nguruwe mkuu wangu, kwa binadamu mchungu!
 
Wapi Bwana kama unakumbuka ya Chacha Wangwe na leo unasema utasahau baada ya uchaguzi, mimi naanza kukosa imani na wewe. maana si ya Wangwe yalikuwa yameshapita?
wewe hebu tupishe hapa.kwanza Chadema yenyewe huijui hata probation hujamaliza unajitia kimbele mbele au unafikiri cheo cha Zitto utapewa wewe?
UMESHINDWA KUISHI NA LIPUMBA utaweza hao wazee wa Machame? pole sana umeruka mkojo umekanyaga MAJITAKA.
 

MKANDARA KUMBUKA KUWA ZIITO HAKUONDOLEWA JINA LAKE NA VIKAO HALALI KIKATIBA NI WAZEE WANNE AMBAO HAWATAMBULIKI KISHERIA.MALECELA ALIZUILIWA NA KAMATI KUU CHOMBO KINACHOTAMBULIKA KISHERIA SIO KAMA HAWA WAZEE WA CHADEMA.

UNASEMA AWE MVULIVU HADI LINI? KAVUMILIA YEYE KUENGULIWA KINYUME NA KATIBA YA CHADEMA. AKALETA MGOMBEA UENYEKITI WA VIJANA AKASHINDA MATOKEO YAKE YAMEFICHWA NA HAO WAZEE SIO KAMATI KUU YA CHADEMA. BAADA YA HAPO ANAKUJA KUTUKANWA HUMU JF YEYE NA MZAZI WAKE. WEWE UNASEMA AWE MVUMILIVU.

NDUGU YANGU HUO UTAKUWA UZEZETA.ZITTO KAINGIA CHADEMA AKIWA NA MIAKA 16 HUKO BUSANDA KOTE KAPITA KUFANYA SHUGHULI YA CHAMA ANAKIJUA CHADEMA NDANI NJE.WEWE UTAKUWA UMEJIUNGA CHADEMA KUPITIA JF-INTERNET MWENZAKO YUKO KWENYE GROUNDS. NAOMBA MWACHE ACHA KUMSAKAMA.

UNASEMA OOH MBONA ALIKUBALI KUONDOA JINA LAKE, HAKUKUBALI KWA HIARI NI PALE TU ALIPOKUTANA NA HAWA WAZEE WANNE NA ZITTO ANAJUA KILICHOMTOKEA WANGWE BAADA YA KUWABISHIA HAO WAZEE WANNE. KWANINI ASICHUKUE TAHADHARI KWA KUONA BORA YA NUSU SHARI KULIKO SHARI KAMILI? AU ULITAKA ANG'ANG'ANIE YAMKUTE YA WANGWE? MAMA YAKE UNGEMLEA WEWE? mwache Zitto wetu.
 

Ndio maana nimemshauri Zitto ajiunge na chama chenu cha mafisadi cha CCM - maana inaonekana mafisadi mnampenda sana Zitto leo na sio siku ile alipofichua siri zenu za kuuza nchi (Buzwagi).
 
Haya matokeo mgeyatangaza siku hiyo ,na si kuja kuyatangazia jf.

Mliyatangaza haya matokeo siku hiyo?? hapo ndipo tutaanza kushika mwongo.

Hatudanganyiki tena kauli mbiu kuelekea 2010

Ha ha ha ha .... wanaccm hamdanganyiki?

Mtadaganyika mara ngapi?

IPTL, Richmond, Buzwagi, Meremeta, Tangold, EPA, BOT, nk
 

Kuandika kwa CAPS kunamaanisha unashout --- au ndiyo unataka kujilipua mabomu? Watu kama wewe huwa siwaamini kabisa. Wakati mmoja unaongea na before u know it - booooom (suicide bombing).
 
Mara zote ukifanya tendo la kishetani ,tatizo la shetani ni lazima aliweke hilo tendo wazi ukiwa bado hai,huwa anakufichia kwa mda tu.

Yeah, kama lile la kusomea porraaaandi IT na kisha kuja Tanzania na kujaribu kumchafua Mwakyembe.
 
Peasant, Mkuu mbona unazungumza wewe tuu na kuamini unayoandika kama ndicho tulichiookuwa tukisema?..
Mkuu wangu kuna namna mbili hapa ya Usiri tunaozungumzia. Ikiwa kuna mbinu za kumwangusha Zitto au madudu yanafanywa na Baadhi ya viongozi wa chama, wanachama na kadhalika ndani ya Chadema, Zitto ni msomi anaelewa wapi pa kwenda...Tatizo la issue hii nzima ni pale Zitto anapochukua sheria mkononi kama vile anamkamata kibaka Kariakoo na kuanza kumtwanga magumi.
Hii haina maana yule kibaka hana makosa ila kuchukua sheria mkononi kinyume cha taratibu za chama ndicho tunachokizungumzia.
Bila shaka hii ni siri ya wao viongozi wa Chadema na ni Uozo mkubwa isipokuwa kwa mtu anayegombea Uenyekiti, na hasa inapokuwa wewe pia ni mhusika..Kitendo kama hiki tayari kinakuondolea uaminifu achana na madudu ya watu wengine.
Kwa maana nyingine tena ikiwa wewe Peasant ni mkweli na umeshikiri ktk kuiba au kumwibia mtu mali yake na unataka kujisafisha sehemu ya kwanza kwenda ni Polisi au kwa mhusika ukiwa na mali yako mkononi na ukawataja wote waliohusika kuiba mali ya mtu huyo... Kisha sheria itachukua mkondo wake na utakuwa tayari kuadhibiwa.. Nipo sawa mkuu wangu?

Tunachokiona hapa ni Zitto akitangaza wizi wa watu wengine ktk gazeti, na pale alipohusika anasema alikwenda omba msamaha maiti ikiwa ktk jeneza au sijui mara kabla (wakati gani hakuna anayejua) ni jambo ambalo hakuna kati yetu anayeweza kuhakikisha ilitokea hivyo,au ndio katika kukipaka anataka kuhakikisha kwamba kama kuna anguko lake ataondoka na wengi.. Kifupi hakuna mtu anayefahamu nini kusudio la Mheshimiwa na anapofanya hivyo atakisaidia vipi chama ikiwa mkuu huyu ameshindwa kusubiri mkutano wa Baraza kuu au Kamati kuu kuwakilisha malalamiko yake yooote.
Tena basi kubwabwaja kwa huyo mwandishi wa Daima - Kibanda kungempa Ushahidi tosha kabisa kuwakilisha hoja yake na na kuhakikisha Pasingetosha! Zipo njia ambazoi Zitto alitakiwa kuzifuata lakini sii kuanika madudu haya hapa JF..trust me, binafsi kuelewa tu kwamba alihusika na mbinu za kumwangusha Wangwe yaani tayari imenitisha zaidi.. Halafu mtu huyu ndiye anatakuwa Mwenyekiti!.. noo jamani, Zitto bado hajakomaa kabisa kisiasa ni kama JK mwaka 1995, mwaka 2005 akawawekea vikwazo CCM na kina Mkapa kwamba asipochaguliwa ataanika madudu yote ya CCM.. na kwa woga wao wakampitisha.. Na upande wa wananchi tukampa a blackmailer kura asilimia 80.
NDIVYO TULIVYO...
 
Pamoja na yote yanayotokea ndani ya CHADEMA lakini ni njia mojawapo ya kukomazwa. hakuna chama duniani ambacho hakijawahi kukumbwa na dhoruba wakati wa kujipambanua kati ya wanasiasa na wadandia siasa.

Hilary Clinton alipokuwa anamkaribia Obama kwa kura wazee wa chama hicho (super Delegate) kwanza walimsihi ajitoe alipokaza shingo wakalamzimshisha,lakini wapambe wake walipomchochea kuwa asijitoe, Super delegate wengi zaidi wakatangaza kumuunga mkono Obama kwa faida ya Chama chao. Clinton alisalimu Amri

kama chama ni chama cha wachaga ni chama gani hakina wachaga? ndani ya miaka kumi CCM imewahi kuongozwa na watunza hazina wachaga wawili. kwanza Sifa Swai na Salome Mbatia. kama wachaga ni watu hatari kuwa wanasiasa ni kwa nini CCM iliwapa madaraka makubwa sana ndani ya Chama chao?

Hivi CCM Moshi inaongozwa na Waluguru?

Zitto hana uzito huo kisiasa kama wengi wenu mnavyotaka kuonyesha. ushahidi wa kimazingira unaonyesha jamaa anashawishiwa zaidi na Viongozi waandamizi wa CCM kuliko wa chama chake.
CHADEMA haitasambaratika!!
 
Ndio maana nimemshauri Zitto ajiunge na chama chenu cha mafisadi cha CCM - maana inaonekana mafisadi mnampenda sana Zitto leo na sio siku ile alipofichua siri zenu za kuuza nchi (Buzwagi).
Kuna mafisadi kuliko chadema? imekuwaje uchaguzi wa vijana kura zimezidi?
 
Balantanda, naomba utuweke sawa hii story yako tarehe yake inachanganya kwani inaonekana niya 4/9/09 tuweke sawa tafadhari.

Mods tunashukuru kwa marekebisho yote tunaenda sawa.
Unaweza kusoma gazeti la Mwananchi lina habari nyingi za uchafu wa Chadema.gazeti hili lilikuwa beneti na Chadema Busanda au una shaka nalo?
 
Kuna mafisadi kuliko chadema? imekuwaje uchaguzi wa vijana kura zimezidi?

Mafisadi waliofilisi nchi kupitia Buzwagi, IPTL, EPA, na mengine ni CCM (just in case umesahau). hayo ya chadema na kura zao unaweza kuwauliza viongozi wa chadema.
 
Unaweza kusoma gazeti la Mwananchi lina habari nyingi za uchafu wa Chadema.gazeti hili lilikuwa beneti na Chadema Busanda au una shaka nalo?

Angalau sasa umeacha kutumia CAPS kwenye maandishi yako (maana ulianza kutishia usalama wa wananchi hapa). Huo uchafu ni pamoja na kutaka kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya kiislam (Tanzanistan)?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…