Mkuu, tatizo hapa ni kuwa, Zitto pia ni CHADEMA. Labda kama unataka kutuambia kuwa ameshaachana nao.
Kuhusiana na kosa la kutumia jina lake halisi, mimi nakiri kuwa hilo ndilo kosa kubwa kabisa alilolifanya. Angekuwa ametumia jina la bandia, habari, shutuma na kauli alizozitoa zisingekuwa na nguvu kama ambavyo zimekuwa na nguvu baada ya kutumia jina lake halisi.
Natamani kuamini kuwa alisahau kuwa aliingia JF na kuandika yote aliyoandika akidhani ametumia jina tofauti. Kwa kuwa madhara aliyosababishia chama chake kwa kauli hizi ni makubwa sana kuweza kuyarekebisha kwa kipindi kifupi. Yanarekebishika tu endapo CHADEMA itachukua uamuzi mgumu wa kumuomba awaachie chama chao na atafute chama kingine. Ila atakapotoka na kuingia chama hicho (kingine), jina lake litafifia kabisa kwenye duru za kisiasa nchini.
mkuu hatupo hapa kukuza jina tupo kufanya kweli tupu kama alivyofanya Zitto na hatimaye demokrasia ya kweli.
Haya yakulinda jina kwa kuogopa mafisadi hiyo ndo weakness kubwa, unalinda jina badala ya haki.
Ni heri kuishi kama simba kwa saa moja kuliko kuishi kama nyumbu miaka 90.