Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.


mkuu hatupo hapa kukuza jina tupo kufanya kweli tupu kama alivyofanya Zitto na hatimaye demokrasia ya kweli.
Haya yakulinda jina kwa kuogopa mafisadi hiyo ndo weakness kubwa, unalinda jina badala ya haki.

Ni heri kuishi kama simba kwa saa moja kuliko kuishi kama nyumbu miaka 90.
 

Na habari za hujumu Wangwe na watoto wake wake wanahangaika ndizo zinatakiwa ziwe siri ya chama.
 
Mkuu, kama kawaida ya jamvi hili nadhani tunajitahidi kujenga kwa kadiri tuwezavyo na endapo kunatokea kubomoa kidogo, basi kunatokea kutokana na jitihada hizo (za kujenga).

Mkuu naheshimu mawazo na nia yako yoyote iwayo. Najua ni vyema kila mtu kuwa na haki ya kueleza anachotaka ili kutimiza mahitaji yake. Ila nia yoyote ya haya yanayofanywa hapa kuhusu Zitto na CHADEMA ni ya kukiua chama hicho. Usinielewe vibaya, chama hiki kikifa sitakonda. Vinakufa vyama vingi tu, na mimi wala si mwanasiasa kimaslahi.

Nawatakia kila la kheri katika ustaarabu huu mpya.
 

Bora ya chama kufa kuliko kuwa genge la kuwapoteza ktk uso wa dunia watetea haki.

Chama chochote kilicho na sura ya namna hii yapaswa kufa.
 

Kuna mstari kwenye biblia unaosema something to this effect: "watu wangu wanaangamia kwa kukosa hekima".
 
sheMkumbo ungefafanua zaidi ...
 
Last edited:
Kwa majibu yake hapa Zito kanichefua kupita kiasi! Au ndiyo njia ya kuondokea kama wengine wa huku kupinzani wanavyofanya. Kweli kaka Zito umetia aibu hakuna mfano. Kumbe wewe ni haramia kiasi hicho kaka, imeniuma sana! Chacha Wangwe alikukosea nini? Na hapo hukuwa mwenyekiti sasa! Ukiupata huo uwenyekiti kuna atakayepumua huko CHADEMA kweli? Nimeogopa leo kupita kiasi. Namshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kutuwekea huu mwezi mtukufu, watu wanapofunga anawasikiliza maombi yao, hebu ona tuliyoyajua leo kuhusu Zito, ambaye huko awali tulidhani ni mkombozi!
 
Kama hamjui ushawishi uliotumika kumfanya aondoe jina lake, kwa nini sasa awali unasema uamuazi huo ulifanyika kidemokrasia?
 


disgusting hatred comments...nausea..vommit!!!

.....mada ukishaingia kuchangia wewe na wale wenzako,,,...mswahili na nungu ...wote mnafanana mawazo.....mijadala yote serious inageuka kuwa ....kinyume chake!!!....sijui huwa unafikiria nini...
 

Zitto bado anaweza kuwa mkombozi kama akijirudi na kuwa yule Zitto wa kabla ya kuingia kwenye kamati ya madini ya Kikwete. Mambo yote ya Zitto yalianza kubadiliwa wakati huo.
 
Bora ya chama kufa kuliko kuwa genge la kuwapoteza ktk uso wa dunia watetea haki.

Chama chochote kilicho na sura ya namna hii yapaswa kufa.

CCM yako ya kifisadi itakufa kabla ya Chadema. Umeanza kuiombea Chadema kufa karibu mwaka sasa.

Huko poraandi wangekuwa wanafundisha uchawi nadhani ungekuwa umewaua viongozi wote wa chadema.
 
Wanajamvi,
Hatimaye nimebaini kuwa hapa jamvini watu wengi wanajiofanya wapinga ufisadi sio wa wakweli na kauli aliyoitoa Kadinali Pengo kuhusu wapinga ufisadi ni ya kweli. Kwamba watu wengi wanajidai kupinga ufisadi kwa maslahi yao.

Yaani kama mtu X anatuhumiwa kwa ufisadi lakini kwa vile mimi Y ni jamaa yangu au nina maslahi naye, basi nimtatetea X hata ikibidi kwa kuhalalisha huo ufisadi anaotuhumiwa nao. Mifano hai nilimeiona mingi tu kama juu ya utata wa urai wa Mhe. Mukasa, watu kuumunga mkono Mwakalinga (Kyela) ambaye ukweli kuwa anatumiwa na baadhi ya watuhumiwa ufisadi liko wazi kabisa. Pia nimeliona katika suala la Mhe. Zitto ambapo watu kadhaa wamekuwa wakimtetetea wakati ukweli upo peupe kabisa kuwa kitendo chake cha kugombea na kuamua kujitoa vyote vilikuwa well calculated chini ya usimamizi wa hao hao wenye kuhusishwa na ufisadi au wale wenye kukitakia mabaya CHADEMA.

Jambo moja ambalo wengi wameshindwa kulibaini ni kuwa hapa hesabu zote mbili zilipigwa mapema kabisa kuwa Zitto akichukua fomu na kwa vile umaarufu wake ni mkubwa na kwa vile wanachama na watu wengi (wakiwemo hata hapa JF) wanamuamnini sana hawatashtukia hii move kuwa anatumika.

Wapangaji wa mchezo huo wanajua kuwa kuwa kutokana na ufahamu mdogo wa wanachama au ushabiki uliopitiliza, jina la Zitto lingefika kwa wanachama (walalahoi) lazima angeshinda tu maana jina lake liko juu sana na wanachanma wengi hawamjui vizuri kiundani. Siwalaumu hao wanachama wa kawaida kwa kukosa ufahamu huo, endapo watu wasomi hata wenye shahada za uzamili na uzamivu hawajaweza kumjua vizuri Mhe Zitto vipi mwanachama anayetoka Ntambaswala au Mangaka au Ifwenkenya?

Bahati nzuri kwa CHADEMA ni kuwa viongozi wengine na wazee wa chama walishamfahamu hyu kijana kuwa anatumikia mabwana wawili wakaona hakuna njia isipokuwa kumfanya achomoe jina lake. Uamuzi wa kuamua kumshinikiza bila shaka ulikuwa mgumu lakini waliona njia hii ina maumivu kidogo kwa chama kuliko kumuachia kijana agombee

Zitto alijua kuwa akishindwa au jina lake likichomolewa kama ilivyotokea basi ataanzisha mizengwe yake ya kukichafua chama ili kikose sifa mbele ya watanzania, na ndilo analolifanya sasa. Kwa hiyo yote anayoongea sio jazba wala hasira ni jambo liliokuwa limeandaliwa vizuri sana.

Kimsingi Zitto anaelewa hata mwisho wake wa hili saga, kuna njia mbili moja atajitoa CHDEMA na kusema anapumzika siasa za vyama, na njia ya pili ambayo nasikia imeshika kasi ni kuondoka nchini kwenda kusoma kwani hata chuo naambiwa kipo tayari.

Inaaminika akirejea toka masomoni hatarudi CHADEMA. Jambo moja aliliosahau ni kuwa watanzania sio mabwege tena, watazipima kauli zake za kuanzia miezi 18 iliyopita na kulinganisha na tukio lilitokea sasa na kauli anazoendelea kuzitoa watambaini kuwa kuna mushkeli katika msimamo wake kisiasa.

Nadhani sasa hata wale waliokuwa wanamshabikia tangu wiki iliyopita, kwameanza kurudi nyuma kutoka na kauli alizozitoa siku mbili hizi. Katika thread hii au nyingine nilitoa mtihani huu kwa Zitto ambao ndio swali alilokuja kuulizwa kwenye kikao cha wazee na kushindwa kutoa jibu.

Anachofanya sasa ni kuwachokonoa CHADEMA na kutoa siri za chama chake ili hatimaye chama kishindwe kumvumilia na hatimaye kimuchukulie hatua kisha aanza kusema mnaoona..........ya Chacha Wangwe yamejirudia

Ushauri kwa Zitto:katika maisha sote huwa tunakosea kwa mawazo yetu au kwa influence ya watu wengine, Zitto toa kauli ya mwisho unusuru mageuzi nchini ili wananchi tuendelee kuwa na imani na upinzani. CHADEMA pia jaribuni kuwa na pamoja na Zitto anapitia kipindi kigumu, matamko anayotoa vumilieni tu, magazeti nayo kazi yake wakati fulani ni kuharibu zaidi kuliko kujenga au kuhabarisha.

Nawasilisha
 

- Bob nimekusikia maneno yako mengi sana, ninasema hivi Zitto ni kiongozi wa juu wa Chadema tena kwa siku nyingi sasa, haiwezekani leo akawa hafai kuwa mwenyekiti tena kwa uamuzi wa wazee wa busara wa Chadema ambao kikatiba hawatambuliwi.

- Kama kweli unataka kuzungumzia ya Malecela na CCM, fungua thread inayowahusu, lakini usichanganye mambo ndio ninaita utoto, CCM imetufikisha pabaya sana taifa kwa sababu kama hizi za busara za Spika, sasa haiwezekani na Chadema mrudie tena zile zile busara za Spika, tena kwa kutumia mifano ya CCM hiyo ninasema ni aibu ya mwaka na mnalimaliza taifa!

- Demokrasia makini inadai Zitto aruhusiwe kugombea now, na sio maneno ya foolishness ya busara za wazee, kama kweli Chadema ni demokrasia makini mpeni Zitto fomu ya kugombea uenyekiti, anything less ni upuuuzi ule ule wa mafisadi wa CCM.

- Chadema ndio mlianza kumchafua Zitto na yeye amewajibu, matokeo ni Chadema ndio mmeabika na mnazidi kushuka hadhi kwa kujaribu kuipindisha demokrasia, mnafikiri maneno mengi haya mnayoropoka yanaweza kuwasiaidia kumbe ni waste of time, kinachoweza kuwasaidia kwenye hilo shomi la uchafu mlilojiingiza ni kumpa Zitto fomu ya kugombea mwenyekiti wa chama waachieni wanachama wa Chadema waamue, otherwise mmejimaliza wenyewe na tamaa ya power kwa wachache huko Chadema,

- Ninarudia hivi JF hatujalala kama huko maporini, hizo ngonjera zenu pelekeni hukooo sio hapa, JF ni mahali pa ukweli sio filimbi na longo longo za mitaani, CCM wameharibu juzi tumewachambua hapa kama watoto sasa mlifikiri ikija Chadema wote hapa tutawapeni free pass maana hii ni forum ya Chadema, now you know hatuogpi wala kutishika, Zitto ni kiongozi wa Chadema, tena wa juu sana, sasa anataka kupeleka mawazo ya uongozi wake kwenye next level ya uenyekiti, sasa mpeni fomu now, msitupotezee muda hapa na hii nonsense, hivi nilipokuwa ninawatwanga CCM na Muungwana hapa na kina Kusila, mbona hukusema haya maneno ya mimi kufurahia kuharibika kwa Chadema?

- Mnaandika pumba hapa kutaka kututisha na maneno ya kitoto hapa wakati ishu iko wazi and very clear kwamba mmetumia nguvu na vitisho na kuvunja katiba ya chama chenu wenyewe kwa kumnyima kiongozi wenu kugombea kwa sababu mnaogopa mlo wa wachache huko utaharibika, sasa eti mnajaribu kulaumu CCM, what CCM has to do with it?

Ninasema tena na tena Chadema mpeni Zitto fomu ya kugombea uenyekiti tena now, msituletee ngonjera hapa JF sio mahali pa ngonjera ni mahali pa kumkoma nyani tu giladi! hatuwezi kushusha standard zetu hapa JF kuwa-commodate Chadema tu no way, mimi ninasimamia policies sio jina la mtu, Zitto is not an ishu hapa the ishu ni demokrasia makini ambayo hapa mmeibana na kuivuruga kwa visingizio ambavyo havi-make a sense at all, Zitto apewe fomu na aruhusiwe kugombea wanachama waamue kuwa hafai, ya kuchafuana kati yenu huko Chadema hapa JF we could care less sisi tunasimamia demokrasia makini that is all!

Respect.

Field Marshall Es!
 

kituo cha kugeukia (turning point) ya Zitto ilikuwa pale alipojiunga na kamati ya madini ya Kikwete (akipingana vikali na msimamo wa viongozi wa CHADEMA) na kuondoa momentum ya wapinzani kwenye issue ya Buzwagi.

Wafuatiliaji wa siasa za bongo walishangazwa sana na uamuzi wa haraka (bila kusubiria makubaliano ya vikao vya chama) yaliyofanywa na Zitto. Hapa JF, watu wengi walipinga sana uamuzi wa Zitto lakini yeye akasisitiza kuwa anajua anachokifanya.

Matokeo ya kamati ya madini ya Kikwete yanajulikana - hakuna kilichofanyika zaidi ya usanii juu ya usanii wa kamati kibao zilizokuwa zimeitangulia.

Baada ya hapo (na mapesa kibao ya posho za kamati), Zitto aligeuka sana kimtizamo na kisiasa - akaanza kuunga mkono Dowans na mengine mengi tu ya serikali ya Kikwete. Hayo mengine ni historia.

Katika hili, sitoshangaa kama Zitto atapewa uwaziri wa fedha au madini na serikali ya Kikwete katika siku chache zijazo.
 
Kwa logic ipi? futa tu thread yako wala haina maana. Tanzania haruhusiwi mtu kugombea Urais akiwa chini ya miaka 40. Zitto ana 33 sasa. Ni vema ukafuta thread yako.
imi


UMEMUAMBIA sawa katiba inasema ni miaka 40....,nadhani hata wadhamini wa chadema walitumia kigezo hicho kumuomba avumilie hata kwenye uwenyekiti agombee mwaka 2013 ,,,akimridhi mbowe...,na atakuwa na miaka 2 ya kujiandaa kugombea urais mwaka 2015 ikiwa kufikia wakati wa uchaguzi atakuwa ametimiza miaka 40.....ndio sababu kuu ya kumuomba asubiri.Wakijuwa wazi kuwa mwaka 2015 na mwaka 2020 ...ndio miaka hasa ya muheshimiwa zitti kambwe kufikia kilele za siasa za tanzania...

kwa umri wa miaka 33 alionao ...anahitaji bado kuongozwa na hata ikiwa kuna maoni aliyotoa humu ndani watu hawakupendwa ...basi tunahitaji kumuangalia kwa jicho la mdogo wetu,kaka,au mwanetu....wengi hapa tunao vijana wa umri huu nyumbani na bado ni kula kulala ....sasa hatuoni kuwa zitto kwa umri wake huu kapiga hatua....
nadhani ni busara kumuelewa kama na yeye ataliona hilo ....ikiwa anaweza kikiri kughafirika ...na kujutia matamshi yake hata kwa moyo tu[kimyakimya].Wengi hapa wanaomuambia ukweli ndio wanaompenda ....wanaomsifia na kumpa kichwa ..eti aendelee kuropoka ni watu wabaya,hawampendi.Ni kama wale watoto wanaoshinda nje ya vilabu vya pombe kusubiri walevi watoke na kuwafuata nyuma wakiwashangilia...pale wanaposema "nivue ,nisivue" watajibu "vuaaaaa""...lengo lao ni kumdhalilisha "mlevi"
akitokea rafiki au ndugu yake kumvika nguo basi ...wale waliokuwa wakisheherekea kudhalilika kwake ..wapo tayari hata kumpiga aliyekuja kumsitiri na kumtukana .....na hata yule "mlevi" atamuona aliyekuja msitiri kuwa ni mbaya ....lakini mara "pombe" au "hasira" zikiisha ....aliyekuwa mlevi atamuendea rafikiye aliyemsitiri na kumtaka radhi ...na kumshukuru ....na wale waliokuwa wakimshangilia aendelee kuharibu....atawaona ni wachawi na wabaya sana!!
 


Mhh hii kali kweli.

hiyo ninasema ni aibu ya mwaka na mnalimaliza taifa!

Mhh


- Demokrasia makini inadai Zitto aruhusiwe kugombea now, na sio maneno ya foolishness ya busara za wazee, kama kweli Chadema ni demokrasia makini mpeni Zitto fomu ya kugombea uenyekiti, anything less ni upuuuzi ule ule wa mafisadi wa CCM.


Unapingana na Zitto anayesema kuwa amejitoa kwenye kugombea?


Huyu ni the same Zitto ambaye ulimwita kuwa Zitto wa Dowans baada ya kumuita tingatinga kuwa ni Bajaji?


Sidhani kama wewe ndiye unatakiwa uwaamulie hao CHADEMA cha kufanya.


Ukiita wanachoandika wenzako kuwa ni pumba, je hiki ulichoandika wewe ni nini?


Respect.

Field Marshall Es!

Haya ni mawazo yako binafsi na sio tamko na JF au sio?
 
Kama ndivyo hivyo Mkuu,wavunje chama hakina maana wizi mtupu wa kutuzuga.

Pamoja na maoni mengi toka kwa wana JF dunia nzima;lkn kwangu ukweli unabaki palepale;SIUTAMBUI WALA SITAKUJA KUUKUBALI UCHAGUZI WENYE HILA WA CHEDEMA WA TAREHE 4 SEPTEMBA UTAKAOMRITHISHA MADARAKA MWENYEKITI MBOWE NA WENZAKE!

Ni uchaguzi wa kiimla mbao haufai hata kufikirika kama umewahi kutokea kwa chama kama CHADEMA ambako viongozi wake wamekuwa wakijinadi kama wao ndiyo "baba wa demokrasia nchini tz"

Je hiyo ndiyo demokrasia kutumia wazee kumuomba mgombea halali kisha kumlazimisha kujitoa?SIWEZI KUTAMBUA WALA KUYAKUBALI WALA KUMTII KIONGOZI ALIYESHINDA KWA MATOKEO YA KUPIKWA!

Natetea katiba,sitetei nguvu za wazee ndani ya CHADEMA akina Mtei!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…