This is part of spinning. Uwongo, uzushi nk. Tatizo wanaopanga haya wanasahau kuwa tuliyapanga wote dhidi ya marehemu Chacha Wangwe. Unatengeneza uwongo, unausambaza, na hatimaye wewe mwenyewe unauamini kuwa ni kweli.
Kama kuna kitu kilimuuma marehemu wangwe na alikufa nacho ni kile cha kumsema kuwa alikuwa anatumiwa na mafisadi. Namshukuru Mungu kuwa nilimwomba radhi Chacha kabla na baada ya kifo chake siku ya postmorterm kwa kumzushia uwongo.
Asha ni mmoja wa wenzangu tulioshiriki kumtenda Chacha. Wanatumia mtindo ule ule na wanapita njia zile zile. Rashidi wa Kuli alisema, YANA MWISHO HAYA!
Asha, (ninakujua wewe ni nani) kuwa mkweli wa nafsi yako! Utalipwa hapa hapa duniani kwa uzushi wako na wenzako.
To put record clear - Kasisiko sio ndugu yangu wa damu. Ni mwenyekiti wangu tu wa Mkoa Kigoma. Pili, Baregu hajahudhuria kikao hata kimoja cha wazee toka ajue ukweli wa mambo.
Tatu, chama jana kimechagua rasmi Baraza la Wazee na mgombea aliyekuwa ananiunga mkono waziwazi ameshinda. Inakuwaje bado vikao vya wazee vya chama vinaendeshwa na Mtei na Ndesamburo?
Pili, vyombo vyote vya habari vilikuwapo katika hotuba ya Mtei. Imekuwaje NIPASHE peke yake ndio ione alisema kuna ufisadi kwenye chaguzi za chama? Mhariri mtendaji wa Nipashe ni jesse kwayu kutoka Machame. Mmiliki wa Nipashe ni Reginald Mengi kutoka Machame.
Spinns sio sustainable. Acheni tujenge chama chetu.
Mkuu Zitto, hakika hii inakuondolea sifa ya Kugombea Uenyekiti automatic yaani hufai!..maelezo yako ni dhahiri yanaonyesha wazi huna Hekima wala Busara kuongoza chama, kifupi hujakomaa kisiasa kabisaaa. Una papara, mwenye hasira na mwepesi kuropoka..Mkuu hukutakiwa kabisa kubwabwaja ovyo hapa kijiweni maneno haya kwani yanazidi kukufunga wewe ikiwa umeshakubali kujitoa ktk kugombea.
Maneno haya yalitakiwa kutangulia na hasa siku ya kikao cha chama. Na nakuomba sana ktk mkutano mkuu wa chama hii September, zungumza yote yaliyoko moyoni mwako, kuwa muwazi, mkweli na bayana tuhoji utendaji kazi wa hao wazee ama watu ambao unawafahamu kuhusika na mbinu hizi chafu za kupakaza.
Kulitumia jina la wangwe na uchafu wote mlofanya dhidi yake hakika umenichefua kichizi yaani kumbe kweli Zitto mlimfanyia Wangwe roho mbaya makusudi?..Hukuona ubaya wa kutenda ulotenda Ukajisafisha hadharani hadi siku ambayo umetendewa wewe ndipo unakuja na habari hizi za Wangwe tena ktk gazeti!..
Well itakuwa vizuri ukimalizia kabisa kutufahamisha maanake hakuna kitu ambacho sisi wananchi tunataka kuelewa zaidi ya Kifo CHA WANGWE kama kuna mkono wa mtu..Ikiwa wewe mkweli na unataka tukuamini basi tueleze yote mlomtendea Marehemu Wangwe ambayo wewe mwenyewe unakiri na ulikwenda simama mbele ya maiti na Kutubu..What real happen? wewe mwenyewe pamoja na Bi Asha ,mlifanya nini au mlicheza part gani mkuu come clean leo hii hapa hapa JF.
Duh, ama kweli mkuu wangu najua ulikuwa na haki ya kugombea kiti hicho lakini leo hii na maelezo haya yaonyesha wazi kwamba hufai kabisa... Na wala usije fikiria kuwa Wangwe alikuwa mtu mzuri vile vile..ila kwa walalahoi wasojua kwamba a sneetch ni Liability ktk taasisi yoyote na hafai kabisa..isipokuwa kwetu sisi Ndivyo Tulivyo (Watumwa wa akili), kumbe ktk jumuiya kama zetu nchi za nje watu hawa hamalizwa vibaya vibaya na hawapokelewi mahala popote.
Kifupi Zitto hakuna sifa hata kidogo unapokipaka chama chako na sidhani hata ukiondoka ama kwenda chama chochote utapokelewa kwa mikono miwili, laa utatumiwa tu na hakuna mtu wala chama kitakachokuamini. Watu kama Wangwe na wewe ni wa kuogopwa na kukaliwa mbali sana na sii kwa sababu unasema ukweli wako ila Mropokaji ni Liabiility ktk chama..Usifikirie unajenga mkuu wangu yaani duh! ama kweli Umri ni moja ya kigezo kikubwa sana ktk CV ya mtu..