Kuelekea Uchaguzi Mkuu: Chama cha ACT-Wazalendo chapokea 21 waliokuwa Wabunge wa CUF

Wote Islamuic name
 
Napataje kadi ya ACT?
 
ACT Wazalendo kitakuwa Chama kikuu cha upinzani, naona kila dalili
 
Alkaida group wameanza mipango mapema,zenji mjihadhari Sana Aya tolah sio wakuamini cdm tulimuona mapema tukafyekelea mbali
 
Kura za wabunge wote wa ACT zanzibar hazifikii za majimbo ya Mdee na Mnyika hivyo CHADEMA wakipata hta wabunge 10 tu tegemea viti maalum kuwa wengi kuliko upinzani wote.

Kwahyo kma issue ni KUB sioni ikienda ACT kwa open play unless CHADEMA wasisimamishe wabunge kwenye majimbo makubwa.

Otherwise ACT haina nguvu bara hivyo solution washirikiane wawe na mgombea mmoja majimbo ya bara otherwise hawatoambulia jimbo hta moja bara
 
vyama vya upinzani huwa vinakuwa na mapungufu yanayowagharimu mara kwa mara.

Maswala ya Udini na ukabila wao wanayapa kipaumbele mno.

kujenga vyama katika misingi hiyo ni kutengeneza jamii inayotambuana kwa misingi hiyo.
 
Piga odds zote ACT- Wazalendo ndio kitakuwa chama kikuu cha upinzani Novemba 1. 2020. Aidha CCM ilijipanga vizuri kuvisambalatisha vyama viwili vikuu, CHADEMA na CUF. Na kazi hiyo wameifanya vizuri sana chini ya Pole Pole na Bashiru Ally. ACT-Wazalendo haikuwa katika ajenda Yao, kwani haingii akili utoe hata senti moja kwa chama chenye mbunge mmoja tu bara na visiwani.

Hivyo kuibuka kwa ACT- Wazalendo kukawaacha viongozi wa CCM mdomo wazi na kumtupia mpira Msajili wa vyama. Msajili akajaribu kuucheza lakini ngoma ilikuwa nzito sana na kuingia mtini bila taarifa. CCM walishindwa kwa muda mfupi kupanga mbinu za kuidhoofisha ACT kutokana na kutojua umaarufu Wake kwa Watanzania baada ya kumpata Maalim na wafuasi Wake hasa kwa kutojua hawa wabunge wa CUF watabaki CUF au watahamia ACT.

CCM wakihangaika kuendelea kuidhoofisha CHADEMA (kazi ambayo haijafanikiwa) na kugeuza mchoro kwa kuiimarisha CUF - Lipumba wakajikuta wana wakati mgumu sana. Walifikiri ingekuwa rahisi kuiimarisha CUF hasa kule Pemba, lakini wakajikuta hata Lipumba kupokelewa tu huko Pemba haikuwezekana licha ya majaribio mara kadhaa ya kutaka kudhuru visiwa hivyo. Mara ya mwisho ilibidi apate Company ya mkuu wa wilaya na polisi kutembelea Pemba kwa usalama huku akipokewa na wanchama wa CCM waliovalia nguo za CUF.

Sasa CCM wamefahamu nguvu ya ACT lakini muda si rafiki kwao kwa kukihujumu chama hiki kukiwa kumesalia takribani miezi mitatu mpaka uchaguzi mkuu. Magu hakupenda sana kutumia mbinu ya wizi wa kura wakati wa uchaguzi, lakini bila mbinu hiyo ACT - Wazalendo wataibuka kidedea. Na hivyo ndivyo itavyokuwa katika nafasi za wabunge na Urais Zanzibar oct 25.
 
Nimesoma kuwa wabunge wanaohama vyama kipindi hiki wanapewa fursa ya kugombea ubunge katika vyama vipya wanavyohamia. Kwa uelewa wangu kuna sheria mpya ilipitishwa kuwa ili mtu aruhusiwe kugombea lazima awe amedumu katika chama chake kwa miaka miwili mfululizo. Sasa hao wanaohamia sasa wakigombea ubunge au udiwani watawekewa pingamizi na wataondolewa hivyo chama kitapoteza fursa ya kugombea jimbo/kata husika na huo sutakuwa uzembe wa hali ya juu. Hivi vyama vinavyozungumzia kuwapa wahamiaji fursa za kugombea hawaijui hii sheria? Au ndio yale yale mgombea akienguliwa wanaanza kulalamika?
 
ACT ndo mbadala wa CUF ndo maana imevuna zaidi watu kutoka CUF.Cuf ilikua na nguvu sana maeneo ya pwani ambapo kwa sasa ACT imekita mizizi huko pwani.

Hata kama wakishirikiana ACT na CDM ZIto atapambana ili mgombea Urais atoke ACT ili awe na uhakika wa kupata wabunge wa kotosha na ACT iwe ya pili kwa kura uchaguzi wa october.ambapo ACT itatoa KUB kwenye bunge lijalo.

Zito yuko smart sana na anajua alifanyalo wala sina shaka nae.ni mtu wa mipango na mwenye maono.
Wanasiasa wakubwa wengi wakihama wanaamia vyama vingine.tofauti na Zito kaanzisha chama kakisimamia mpaka kinavuna wanasiasa wakubwa kama Maalim na Lissu kama akikaa sawa.
 
Yote kwa yote Zito Ni Mwanasiasa mwenye Akili na mipango kwa kizazi hiki

Anastahili kwakweli
 
Ni uzwazwa kufanya maandalizi ya harusi wakati unajua harusi haitafanyika.!
 
Story ya Ufipani sasa hahaha
Uganga wa kienyeji mwingiii
 
Hakuna jipya wamedili rangi ya nyumba tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…