Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,290
- 2,468
Watu wanasema kuwa CHADEMA msirudie kosa kama kipindi kile cha Lowasa. Inawezekana kweli ikawa ni kamchezo kanachezwa tena na CCM lakini lolote laweza kutokea. Upepo hubadilikia hewani.
Mtazamo wangu ni kuwa, kwa kuwa Magufuli hiki ni kipindi chake cha pili anachotaka kuwania sasa, ni wakati mzuri sana wa kujaribu mbinu hatarishi hata kama zinatiliwa shaka. Kipindi hiki possibility ya Raisi aliyeko madarakani ni kubwa kuendelea hadi miaka yake kumi kukamilika.
Sasa ikifika 2025 CCM haitamsumamisha tena Magufuli bali atakuja mpya na hata ndani ya CCM kutakuwa na mtifuano kwenye ngazi ya urais kama tulivyoshuhudia kwenye ngazi ya ubunge.
Sasa hata kama leo CHADEMA wakiamua kushirikiana na ACT wakamsimamisha mgombea mmoja, ukweli utajulikana baada ya uchaguzi kuwa Membe alikuwa pandikizi au la, ili ikifika 2025 upinzani ujue kabisa kuwa CCM huwa wanapanga kuharibu mikakati ya upinzani kwa kuwapelekea watu ambao huja kuwa ni wagombea kisha wakagawa kura.
Kipindi hiki kwa asilimia kubwa yako mambo maatatu makuu:
1. Kuvuna majimbo ya kutosha kwa kuwekeza nguvu ya kutosha majimboni, bila kujali ni CHADEMA, ACT, NCCR au CUF
2. Kupata kubaini kama wagombea tokea CCM huwa ni mapandikizi au la. Pengine si mapandikizi ila mfumo huwalazimisha kurudi chamani
3. Kujipanga vyema kwa uchaguzi rasmi wa 2025. Hapa watakuwa wameshazijua mbinu za CCM vya kutosha. Hivyo kama kuna mapandikizi wajue hakuna tena kupokea walioachwa na CCM dakika za mwisho.
Hivyo nawahauri CHADEMA kuunganisha nguvu na ACT kumtumia vizuri Membe huku wakiwa makini kusoma trend