Nakupa bonusNimekupata vizuri kiongozi
Mwaka 2015 mara kura ziliponza kupigwa JF ilipotea kiaina. Mwaka huu ndiyo kabisaa, walivyo na hofu hakuna chombo huru kitakuwa hewani. Si ajabu hata Whatsup ikapotezwa kwa muda.Vema kukawa na mchakato wa kuwa na plan B in case of any emergency...
Jr[emoji769]
Mbona hata 2015 ilikuwa haipatikani? Hili ni jambo lililo wazi.Haya mambo kama yatatokea naamini JF itakuwa ya kwanza kufungwa kwa kweli
VPN haitasaidia kwenye hali kama hii. Uchaguzi wa 2015 nilikuwa nje ya nchi lakini JF ilikuwa haipatikani kabisa.Wana IT muanze kutoa shule ya namna ya kutumia VPN
🖕Acha kutosha watu wewe,Watumiaji wa mitandao ni wachache kuliko wapiga kura,bado hamjaweza kuitisha serikali kwa kutumia mtandao
Hii mbinu rahisi haiwezi kufanyiwa figisu ya maagizo toka juu. Wala hakuna kigogo anayeweza kuizuia bluetooth au memory card kufanya kazi. Hakuna polisi wa kukamata bluetooth wala tcra wa kukamata memory card nchi nzima. Hata Tv zote na radio na mitandao ikigoma bluetooth na memory card itafikisha ujumbe hata mahali pasipo na mtandao au hata radio.[emoji1752][emoji1534][emoji1548]Hilo jambo nadhani litatokea. Na tayari nimekuja na wazo. Soma hapa Wazo: Kutumia njia mbadala kufikisha ujumbe kwa wananchi
Nifikishieni ujumbe kwa wahusika.
Serikali hii itajichimbia kaburi ikijaribu kuzima mitandao, watu watachukua hatua nyingine mbadala zinazoweza kuwa na matokeo mabaya sana kwa watawala. Kwanza hadi sasa jumuiya ya kimataifa imeanza kuitazama serikali kwa jicho kali zaidi nimesikia kwenye vyombo vingi vya kimataifa kama DW, CNN, BBC jinsi wanavyozungumzia suala la kuzuiliwa kutangaza chochote Tz mpaka wapate ruhusa maalumu ya serikali. Yatakuja makubwa muda si muda. Najua dhambi humfunga mtu asione na kumwondolea hekima, na kupelekea kuanguka kwake, hayo ndio yanayoendelea kwasasa hapa.Wakuu ndani ya Jamii forums...Wageni kwa wenyeji...ni vema tukajiandaa kabisa kisaikolojiia na ikibidi kuweza kabisa kuanza mchakato wa kuwa na plan B.
Kadiri fukuto la uchaguzi mkuu linavyoanza kupanda kuna viashiria vya kila aina kwamba kuna mamlaka hazipendi baadhi ya habari kuwafikia wananchi wengi....habari zitakazotoka ni zile tu zilizochujwa na ama la kuhaririwa na mamlaka husika
Tayari vyombo vya ndani vimeshapewa onyo na karipio la kurusha habari kutoka vyombo washirika nje ya nchi ...pamoja na kuathirika kimapato kwa hatua hiyo ...wananchi wataigeukia mitandao ya kijamii yenye nguvu kuliko hata hivyo vyombo rasmi vya habari
Sambamba na hilo tutegemee wakati wowote toka sasa bei za vifurushi vya kuperuzi mitandaoni vikizidi kubadilika na kuwa ghali zaidi...kama mnakumbuka zoezi kama hili lilifanyika kuelekea uchaguzi mkuu 2015 na kamwe hatukuwahi tena kurudishiwa ule unafuu wa data.
Hizi online tv na radio pia zijiandae na haya maumivu...Ilishatolewa tahadhari kubwa kwamba kila unachokifanya mitandaoni kinafuatiliwa kwa karibu sana...watu kidogo wamekuwa makini kwenye hilo...lakini sasa hilo kilikuwa cha mtoto tuuu...maumivu makali yanakuja.
Wito wangu kwa mamlaka husika: kwa heshima kuu naomba muwe na tafakuri jadidi kwenye hili...uhuru wa kupashana habari ni hitaji muhimu na la msingi kwa watu wote...hili husaidia kuepusha hatari nyingi....Fanyeni yote lakini chondechonde msije mkazima mitandao ya kijamii.
Uchaguzi wenye changamoto za ushindi kama huu huwa na fukuto kila upande na kwa kila mmoja....njia pekee ya kupoza hili fukuto ni kutoa uhuru watu waseme lakini bila kuvunja sheria...watu wakisema hupata nafuu kubwa ndani ya miili yao
Kuwazuia kusema ama kuwazuia kupata habari ni sawa na kuruhusu maji kuingia kwenye nyumba isiyo walau na upenyo wa maji kutoka......Matokeo yake ni uharibifu mkubwa
Mungu ibariki Tanganyika na watu wake ili wote kwa umoja wetu tutambue kuna maisha baada ya uchaguzi..!!!![emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
Jr[emoji769]
Dooooh!VPN haitasaidia kwenye hali kama hii. Uchaguzi wa 2015 nilikuwa nje ya nchi lakini JF ilikuwa haipatikani kabisa.
HAKUNA aliyesalama, hata manyumbu hayako salama.Kuna MATAGA hapa huwa yanafurahia kutumia jamii forum, yanafikiri kuwa yapo salama!
Copy and paste. Hapa hujaelewesha wasiokuwa Wana IT.A virtual private network (VPN) gives you online privacy and anonymity by creating a private network from a public internet connection. VPNs mask your internet protocol (IP) address so your online actions are virtually untraceableView attachment 1533302
Jr[emoji769]
Naomba kama una weledi juu ya hili uwaeleweshe tafadhali ...nimefanya part yangu kwa mhusika na amenielewaCopy and paste. Hapa hujaelewesha wasiokuwa Wana IT.
Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Aliyekuwa Ana ujuzi na haya Mambo. Sasa Mimi numeona tu hayo maelezo sijui nayafanyaje.Naomba kama una weledi juu ya hili uwaeleweshe tafadhali ...nimefanya part yangu kwa mhusika na amenielewaView attachment 1533529