Uchaguzi 2020 Kuelekea Uchaguzi Mkuu, tunawaomba wazee wetu wastaafu wapumzike, msiwatumie kwenye kampeni zenu

Uchaguzi 2020 Kuelekea Uchaguzi Mkuu, tunawaomba wazee wetu wastaafu wapumzike, msiwatumie kwenye kampeni zenu

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,102
Reaction score
1,919
Nimekumbuka Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015 wazee wetu walivyotutahadharisha kukisaidia chama tawala, sipendezwi binafsi kuwatumia wazee wetu kwenye kampeni kwa ajili ya kuokoa jahazi mkifanikiwa mnawatelekeza hata mafao yao yanakuwa Ni hisani yenu Wala siyo sheria.

Nakumbuka jinsi Mama Maria Nyerere alivyotengenezewa video kumnadi mgombea uraisi kupitia CCM, jiulize, Bibi Kama yule anaingia kwenye shooting, akikosea anarudia, najua watu wa video production mnajua ugumu wa shooting ulivyo, Jamani safari hii mjinadi wenyewe, waacheni wazee wetu.

Ukilikologa lazima ulinywe. Mzee Mwinyi, Kikwete, Pinda, Maaskofu, Pius Msekwa, etal tunaomba muwe wafuatiliaji tu CCM mwaka huu ipo vizuri kuliko awamu za nyuma, tuwaacheni wajikampeni wenyewe.

#fair and free election
 
Waache tu. Wazee hufurahia kushangiliwa. Inawaongezea mda wa kuishi. Hawana "impact" yeyote kwa "rational voter".
 
Kwanini umkatalie Mtanzania mwenzako kutoa mawazo yake kuhusu mtu wa kumchagua atuongoze Watanzania wakati wewe unatoa mawazo yako? Mstaafu anabakia kuwa Mtanzania tu sawa na wewe na anabaki na haki yake ya kutoa mawazo yake sawa na yako. Usinyanyase Mtanzania mwenzako kwa kuogopa tu maoni yake yanaweza kueleweka zaidi kuliko yako.
 
Mzee Mwinyi atattamani kumpigia debe mtoto wake
 
Back
Top Bottom