Mada inahusika.
Licha ya ahadi za kufanyika uchaguzi huru na wa haki kutoka kwa Rais JPM na serikali yake ukweli uko wazi. Hakuna dalili na ni kama mchezo umeisha kwenye hii hatua ya uteuzi na mapingamizi.
Jiulizeni yale mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi hayakulenga kitu kweli? Kwamba ratiba ya NEC inaonesha uteuzi utafanyika siku moja ya tarehe 26 na mapingamizi yatakuwa masaa 24 ilikuwa bure?
Hapo ndipo kazi ya CCM, NEC na washirika wao wa kidola walikusudia kuisaidia CCM baadae zianze kampeni na muda wa mapingamizi na ufuatiliaji iwe umeisha.
Tazama "Dillema" iliyopo kati ya kuendelea na kampeni kwa vyama na kufuatilia mapingamizi ya walioenguliwa kwa hila ulivyo. CCM inafaidi matunda ya mfumo Dola na haina habari kabisa na dhuluma iliyopo.
Jambo moja walilosahau CCM haya yanafanyika Umma ukijua wazi fitna hii. Bado wako kwenye imani ya matumizi ya Dola tu na wanaamini hao ndio wana uwezo wa kunyamazisha kudai haki za watu.
CCM wanasahau hatua za kuleta mageuzi kwenye jamii kwamba huanzia mbali. Kwa hatua ya sasa CCM imeamua ku-risk ili kujinusuru na hii ni hatua hatari.
Kuna "Suprise" moja ambayo vyanzo vinabainisha kuwachanganya CCM nayo ni Ujio wa Lissu na alivyobadilisha upepo huku wakijua kipindi hiki Tanzania inafuatiliwa sana lakini ndio hivyo hakuna zaidi ya ku- risk kama ndio "option" yao kwa sasa.
WAPINZANI
Kwenu sio kwamba ilikuwa hamjui kwamba kuna mazingira ya hatari kuelekea uchaguzi huu. Tunatambua jitihada zenu za kushauri kule bungeni, jitihada zenu za kutaka kuonana na JPM pale magogoni ili mustkbali wa Taifa uwekwe vizuri. Tunatambuwa jitihada zenu za kuwataka viongozi wa dini na wastaafu wakemee uvunjivu na kunyima haki za watu bila mafanikio. Tunatambuwa jitihada zenu za kuiomba Mahakama na bunge kuidhibiti serikali na kuilinda KATIBA na mligonga mwamba.
Si kwamba viashiria vya wazi havikuonekana kwenye chaguzi za marudio na ule uchaguzi wa mitaa wa 2019. Tunatambuwa kwamba mlikuwa mnaweka kumbukumbu sawa. Dunia imeona jitihada hizo, mmedharauliwa na kila taasisi na Dola na mchango wenu umewekwa kapuni.
CCM na dola hawataki kujifunza na kwa upevu wake hawana namna ya kufikiri zaidi ya kufuata zile zile njia vilivyopitia vyama vya ukombozi Afrika na kufanya makosa yale yale.
Tunafahamu mlivyosoma upepo na kuamua kushiriki uchaguzi wa 2020 bila KUSUSA na msithubutu kususa, lakini mlituahidi KUDAI TUME HURU KATIKATI YA UCHAGUZI HUU. Ndio WAKATI UMEFIKA.
Bado nini kitokee ili mjiridhishe kwamba CCM hawako tayari kwa uungwana na kutoa haki , hawako tayari kuweka mustakbali wa Taifa hili na hawako tayari kwa mabadiliko.
Mlijipa muda kusubiri wadau wa Taifa wakiwemo viongozi wa dini labda wangefanya nini, mlisubiri kuona Wazee na wastaafu watasema nini walau hao wachache akina Marehemu Mzee Mkapa na ametangulia, wakina Butiku japo kwa kuvizia na wengine wameamua kukaa kimya wakifaidi keki ya Taifa.
Kwa maelezo ya hapo juu nadhani wakati umefika wa kuwafahamisha CCM na Dola kwamba na nyinyi ni sehemu ya Watanzania. Wafahamisheni umuhimu wa kutoa haki na kupata fursa ya ushiriki sawa na wafahamisheni umuhimu wa Tume Huru ya Uchaguzi.
Tumieni njia zote za kisheria na taratibu zilizopo na tumieni fursa zilizopo.
HAKUNA KUSUSA , TAFUTENI HAKI ZENU KWA MAZINGIRA YALIYOPO.
Tumekufahamuni tunawaamini.
Kishada