Acha hizo,unawashwa nini this mornging? Nani kakwanbia nafundishwa mambo ya binadamu wote ni sawa huku marekani? We vipi mkuu? na wapi hapo nimeshindana? Wewe si unajuwa kila kitu,kuanzia kwenye mapenzi,mahusiano,michezo,kila jukwaa humu humo ndani,you know everything unajua,sasa nitashidana vipi na wewe? Ama kweli una muda! Duh!Sasa bwana Mangi baada ya kupata elimu zaidi huko ughaibuni bado unaamini kwa Mwalimu ndiye mwanzilishi wa hiyo falsafa?
Halafu acha ghadhabu Mangi. Tunajadiliana tu hapa. Hatushindani, okay?
Acha hizo,unawashwa nini this mornging? Nani kakwanbia nafundishwa mambo ya binadamu wote ni sawa huku marekani? We vipi mkuu? na wapi hapo nimeshindana? Wewe si unajuwa kila kitu,kuanzia kwenye mapenzi,mahusiano,michezo,kila jukwaa humu humo ndani,you know everything unajua,sasa nitashidana vipi na wewe? Ama kweli una muda! Duh!
For ya info sina muda kuwa kushindana.
Mwalimu yuko wazi kuhusu maana ya "watu wote ni sawa". Hapo anamaanisha wengine si "miungu" wanaostahili kuabudiwa au "nusu-nyani" wanaostahili kunyonywa. Pia anatafsiri utu/ubinadamu kama kiini (essence) cha kila mtu/mwanadamu hivyo hakuna mwanadamu/mtu mwenye stahili ya 'utu' au 'ubinadamu' kuliko mwingine. Ndio maana anauliza swali hili linalojijibu lenyewe "Kuna binadamu zaidi ya mwenziwe?"
Hivyo basi tunapoongelea wanadamu/watu wote kuwa sawa katika muktadha wa Ujamaa Mamboleo tunaamanisha wote tuna haki sawa ya kuishi maisha bora, kuwa na afya bora, kupata elimu bora, kufanya kazi bora na kupata kipato bora. Hii ni haki ya kila mwanadamu ni sio haki ya watu wachache ambao wao na watoto wao wamehodhi Haki zetu sote zilizoainishwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu.
Binadamu Wote ni Ndugu Zangu na Afrika ni Moja!
Hapana.
Hilo ongezeko la mashine lilitokana na nadharia za uchumi za Import Substitution Industrialization (ISI) ambazo tulizivaa kichwa kichwa na sio hizo nadharia zako za Benki ya Dunia iliyokuwa ikimwaga fedha kwenye miradi mikubwa ya Kidola iliyoweka Umma pembezoni.
Tulichotakiwa ni kuangalia uhusiano kati ya mapinduzi ya kilimo na mapinduzi ya viwanda hasa nadharia 'Lewisian Turning Point' ambayo aliiongelea Mkaribiani Arthur Lewis kuhusu namna ya kuingia kwenye sekta ya Viwanda bila kuathiri uzalishaji wa Sekta ya Kilimo.
Mimi hapa kwenye Ujamaa Mamboleo naongelea mchanganyiko wa nadharia za Uchumi wa Kiimla na Uchumi Huria yaani 'Uchumi Mchanganyiko' unaohakikisha kuwa tunawapa uhuru Umma kuzalisha bila kuingiliwa sana na Dola ilhali Dola inasimamia 'Mali ya Taifa' kama Madini.
Kwa Mwanafalsafa Aliyeianzisha.
Mwalimu yuko wazi kuhusu maana ya "watu wote ni sawa". Hapo anamaanisha wengine si "miungu" wanaostahili kuabudiwa au "nusu-nyani" wanaostahili kunyonywa. Pia anatafsiri utu/ubinadamu kama kiini (essence) cha kila mtu/mwanadamu hivyo hakuna mwanadamu/mtu mwenye stahili ya 'utu' au 'ubinadamu' kuliko mwingine. Ndio maana anauliza swali hili linalojijibu lenyewe "Kuna binadamu zaidi ya mwenziwe?"
Hivyo basi tunapoongelea wanadamu/watu wote kuwa sawa katika muktadha wa Ujamaa Mamboleo tunaamanisha wote tuna haki sawa ya kuishi maisha bora, kuwa na afya bora, kupata elimu bora, kufanya kazi bora na kupata kipato bora. Hii ni haki ya kila mwanadamu ni sio haki ya watu wachache ambao wao na watoto wao wamehodhi Haki zetu sote zilizoainishwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu.
Binadamu Wote ni Ndugu Zangu na Afrika ni Moja!
Kwanini unasema miradi hiyo iliweka umma pembezoni wakati wengi humu ndani wakiwemo: Mkandara, Mkjj, Kishoka etc bado wanadai kuwa viwanda vyao vimeuzwa kwa bei ya kutupwa.
Kuhusu mapinduzi ya kilimo sidhani kama viongozi watanzania wana hamu nayo. Kwa sababu tukirudi kwenye nadharia yangu ya kwanza, japokuwa sio valid, mapinduzi ya kilimo yatahitaji machinery. Na tukiongeza machinery kwenye kilimo, tutaongeza output per worker. Na ongezeko hili litasababisha watu wengi kukosa kazi vijijini.
Waliokosa cha kufanya vijijini itabidi wahamie mijini na kusababisha un-employments ambayo mpaka sasa hatujajifunza kukabiliana nayo.
Mpaka sasa tunajivunia amani, lakini kwa sehemu kubwa amani hii inaletwa na maisha ya vijijini. Sina imani kama ukipewa uongozi wa nchi utajaribu kuleta mapinduzi ya kilimo.
Au utatumia pesa zitokanazo na machimbo ya madini ku-spread wealth?
Mungu Muumba.
Acha kuweka maneno mdomoni kwangu. Sijasema kuwa hiyo miradi ya Benki ya Dunia na nduguze ilikuwa ni ya Viwanda. Naongelea miradi ya maranchi iliyoweka wafugaji pembezoni, miradi ya mashamba iliyoweka wakulima pembezoni na kadhalika. Kukua kwa sekta ya viwanda Tanzania enzi hizo sio kwa sababu ya Benki ya Dunia na washirika wake. Heri hata ungesema ni kwa sababu ya Wascandnavia na Wachina.
Nikipewa nchi hii jambo la kwanza litakuwa ni kuhakikisha kuwa watu wanashiba kwa kupata mlo kamili kwa kutumia gharama nafuu na muda mchache. Watakaposhiba na kukata kiu yao nitakuwa nimeokoa muda mwingi wanaopoteza kutafuta chakula na maji ili kukabiliana na njaa na utapiamlo. Kwangu hayo ndio mapinduzi ya Kilimo. Hayahitaji Mashine. Yanachohitaji ni kumpa uhuru mkulima na mfugaji azalishe kwa tija bila kumuingiliaingilia na kumsongasonga kwa nguvu za dola.
Mkuu, mbona sasa unakuwa naive. Nchi nyingi za wahisani zinafuata guidelines au nadharia zilizofanyiwa kazi na World Bank/IMF. Na siku zote misaada yao imeambatana na yale World Bank wanayopigia matarumbeta na data zipo. Hivyo sina sababu za kuwataja waScandinavia wakati wanachofanya kiko tayari mapped na WB/IMF. Kama wasingefanya hivyo basi tusingekuwa na Paris Club.
Kuhusu solution yako, kuna kipindi nilikuwa na project ya kutaka kumjibu Dr. Malima Bundara "Waafrika ndivyo tulivyo?" Na nilipata majibu kama yako. Lakini kwa sababu ya kubeba mabox, kazi yenyewe imekuwa nzito sana kuimaliza.
Ndio, unataka rejea(reference)?
Mkuu sasa hapo naive ni nani? Hivi hujui kwenye miaka ya mwisho ya 70 na mwanzoni mwa 80 kulikuwa na vuguvugu kubwa la kubadili uhodhi/ukiritimba wa Benki Kuu na IMF? Soma Development Dialogue 1980: 2 la Dag Hammarskjold uone jinsi ambavyo Waskandinavia walivyokuwa wakishirikiana na 'Nchi za Dunia ya Tatu' kutekeleza mambo nje ya mfumo huo wa Benki ya Dunia. Na je umaisahau Willie Brandt Commission na ile ripoti yake? Au hujui asili ya The South Commission iliyokuja kuwa chini ya Uenyekiti wa Mwalimu?
Naam itakuwa jambo jema ukimjibu Dk. Malima Bundara. Hicho kitabu pamoja na kingine cha 'The Coming Revolution' cha Mtanzania ambaye jina lake limenitoka kidogo nimewahi kuviandikia makala kuonesha kuwa vinajaribu kujenga hoja ya kutawaliwa upya tena na wakoloni kwa ridhaa yetu wenyewe. Hii ni hatari sana, kuamini kuwa Waafrika hatuwezi kujitawala wenyewe na kujiletea maendeleo yetu wenyewe kisa eti ndivyo walivyo tu! Mbona huko kwenye kubeba mabox tunaweza kutawala?