Kuelekea uzinduzi wa Album ya A boy from Tandale ya Diamond

jbernad2

Senior Member
Joined
Feb 7, 2017
Posts
112
Reaction score
86
Kwa Nini Diamond amechagua kwenda Kenya kuzindua na kusikilizwa kwa album yake kwa mara vya kwanza. Pia Wakenya wameitumia vema fursa hiyo kwa kampuni za biashara kujitokeza kwa issue za Biashara. Sisi watanzania bado Tunaendelea kulala. Hongera Diamond Piga kazi.
 
Nabii hakubariki kwao...wakenya wajanja sana kwenye fursa wao wameiona fursa safaricom na makampun mengine yameweka pesa nyingi kwenye hiyo event.

sisi watz tunapambana kuakikisha huyu jamaa anapotea mazima ata kama haitatunufaisha ila roho za kiswahili zimetujaa.
 
Kweli kabisa Mkuu kwani naona safar com wameishika hii event vilivyo na sasa naona kmpuni ya kitalii nayo imekuja kunogesha zaidi.
Hata hiyo Texas Cancer centre wanatumia fursa. Wacha sie tulale tukiamka tutaanza kulaumu wakenya kwa kupora rasilimali zetu kama mlima Kilimanjaro, Huyo Diamond nk. Hapa nakumbuka issue ya Mrisho mpoto huko London alivyowakilisha Kenya vema badala ya Tanzania.
 
Watanzania uzalendo hakuna,bora auze huko tu kwanza ndo wanamoyo wakununua,lakini bongo pirate kibao,unatoa Album cku moja tu washaanza kuiburn..tunasikitisha sana wabongo.
 
Watanzania uzalendo hakuna,bora auze huko tu kwanza ndo wanamoyo wakununua,lakini bongo pirate kibao,unatoa Album cku moja tu washaanza kuiburn..tunasikitisha sana wabongo.
Watanzani wana msubiria bekaboy aweke mp3 wakadownload na kukimbizana youtube waongeza view,zaidi ya hapo hamna support yoyote wanayotoa.
 
Bongo tuko busy mahakamani, subirini kwanza tuwafunge wanaomsema vibaya Msukuma na serikali yake wote.
 
wabongo wengi ni wachawi wanachokosa ni vifaa tu haswa vjana
 
Nimecheka hapo uliposema wanapambana kwa hali na mali kuhakikisha jamaa anapotea mazima hahaha
 
Jana kuna jamaa yangu Mkenya alivyokiwa anasifia diamond kuzindua album Kenya.. Diamond anapendwa sana Kenya..sisi wakina ruge wanataka kutuaminisha wasanii wao..mchawi wa kwanza ruge
 
Lakin jamaa hafanyi show za ndani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…