Kuelekea Valentines day nimeamua kuonyesha 'love' kwa hawa

Lol!
Nilikuwa sijasoma hili...
Mimi hata iweje siwezi kuwatumia salamu mapopoma haya GENTAMYCINE idawa DuppyConqueror Carbondioxide el nino The bold kilimbamula

Naogopa kuweka list ya marafiki ninaowatumia salaam maana ni wengi nikisahau wengine itakuwa lawama.
 
Hapo umekosea mkuu....
Halafu umesahau alivyokuwa anajiita mchungaji Illovo?
Hahahahahaa nikikumbuka vimbwanga vyake nacheka sana,hasa alivyokuwa anatafuta mchumba sijui mke.

daah kweli nimemsahau Illovo na Barbarosa
 
Anayejua ID ya lara1 kwa sasa plz aweke kwa hewa, micng sna huyu lady
 
Juan Roman Requelme Aka La Brujita

Inawezekana labda umesahau ila Mchezaji aliyekuwa akiitwa na Waargentina La Brujita hakuwa Juan Roman Requelme bali alikuwa ni Kiungo aliyenisababisha na Mimi kula Hela za Ndondo wakati nikisoma Uganda baada ya kucheza kama yeye katika midfield hadi Waganda wakata nibadili Uraia ili nichezee timu yao ya Taifa ya Vijana mwaka 1999 ( wakati huo najua ulikuwa ndiyo kwanza upo katika beseni unaogeshwa ) lakini nikawaambia kuwa naipenda mno nchi yangu ya Tanzania na nikawakatalia. Huyu Kiungo anaitwa JUAN SEBASTIAN VERON. Ningesema niendelee na kucheza mpira nina uhakika ningeshindana sana na akina Pirlo, Xavi na Deco kwani nilikuwa na uwezo nao sawa ila basi tu Mfumo nao uliniathiri kuchanganya na njaa na mikwara ya Wazee kutaka nijali Masomo. Najua hii kitu Nifah atanibishia. Mkuu nilikuwa nafanya vitu ambavyo si Niyonzima au Kamusoko au Mkude au Ndemla wanaweza kufanya hasa sehemu ya Kiungo hasa cha chini na ndiyo maana nikiwaona vijana leo wanambwelambwela tu uwanjani huwa napatwa na hasira mno.
 
Hahahahahaa aiseee wewe jamaa ni kiboko!
Kumbe na wewe unaipenda Tanzania?Nilifikiri wewe ni Mtusti na unaipenda Rwanda KULIKOTUKUKA!
Sina cha kubisha kuhusu kiwango chako cha kusakata kabumbu ila hapo kwenye kushindana na Pirlo na Xavi?
πŸ™„πŸ™„
 

Najua huwezi kuamini kuwa nilikuwa na uwezo sawa na akina Pirlo na Xavi kwakuwa wao wapo Italy na Spain huku humu nikipigika zangu Tandale Tanzania. Ila amini usiamini Watanzania niliosoma nao Bugema na Kabojja nchini Uganda miaka ya 1996 hadi 2001 na hasa wale tuliokuwa tukikutana katika UMISETTA za Uganda watakuambia shughuli yangu. Nilikuwa napigishwa dimba la chini au la juu halafu siku zingine namaliza mwenyewe au natupwa shavu la kulia na kushoto. Dada umenikumbusha mbali sana na laiti Wazazi wangu wasingenilazimisha nishike Masomo leo ningewaleteeni sana TUZO kama hizi za Mbwana Ally Samatta nyingi sana na kinachoniuma sasa ni kwamba nimeishika hiyo Elimu lakini sina UTAJIRI wowote japo nina hako Ka Degree kangu na kama mambo yakienda poa naweza mwaka huu au hata mwakani nikamaliza M.A. lakini najuta kuwa Msomi na kuachana na Mpira ambao ndiyo naamini UNGENITOA mno KIMAISHA. Huwa nasikia Uchungu mtu kama Ngassa au Samatta japo hawana ELIMU kama yangu lakini KIMAISHA na KIPESA wamenipiga GEPU kubwa sana na Mimi UTAJIRI wangu ni hivi VYETI tu vya UNIVERSITY lakini MFUKONI ni bonge la NGUMBARU. Kungekuwa kuna dawa ya kurudisha UMRI nyuma hakika ningeinunua ilia nirudishe kidogo tu mpaka miaka 17 kisha Watanzania muwe kila siku mnakuja kunipokea JNIA nikiwa na MATUZO mengi tu. Kiwango changu na Kipaji changu unaweza kukikuta kwa Ferminho au Viera au Gaucho. Naomba nitumie pia FURSA hii kuwaasa WAZAZI ambao naamini wengi mpo humu kuwa jaribuni basi KUHESHIMU interests za WATOTO wenu na muwape sapoti ili wafikie huko watakako. Watanzania leo mnalalamika kuwa ni Mbwana Samatta tu ndiyo kawatoa KIMASOMASO ila kama Washua zangu wangeniruhusu niendelee na KUCHEZA MPIRA na kwa Kiwango kile KIKUBWA nilichokuwa nacho Tanzania mngekuwa mnakula KUKU kwa MRIJA sasa. Na ulivyo mbishi kama SHIPA wewe Mwanamke najua na hii nayo UTANIBISHIA tu.
 
Hahahahahaa hapana!
Kiukweli umeniumiza sana jinsi ulivyoongelea hili kwa uchungu.
Wazazi wengi wanaamini elimu ndiyo itakayowatoa vijana wao kuliko vipaji walivyojaaliwa.
Hata hivyo bado hujachelewa popoma,pigana tu huenda ikawa FAINALI UZEENI!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…