Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Uchaguzi ujao atolewe tu hana jipya
Tunaongozwa na mpuuzi asiyejua lolote ndiomaana wanaomuzunguka wanafanya wayatakaoyo, mtu alikuwa msambaza chai maofisini ataweza nini kwenye nafasi kubwa kama hiyo?
Tunaongozwa na mpuuzi asiyejua lolote ndiomaana wanaomuzunguka wanafanya wayatakaoyo, mtu alikuwa msambaza chai maofisini ataweza nini kwenye nafasi kubwa kama hiyo?
 
Wewe endelea na makala za kuelimisha vijana na mahusiano upo vizuri, huku tuache wenyewe huna upako huo.

Magufuli tutaendelea kumsema Kwa maovu aliyowatendea Watanzania tangu kuumbwa Kwa ulimwengu huu, udikteta na utawala wa mkono wa chuma tulikuwa tunausikia tu Kwa wenzetu na kusoma kwenye historia, lakini yule Mrundi wa Chato akaja kutuonesha dhahiri.

Hadithi kama hii usithubutu kwenda kuiogea kwenye familia ya Ben Saanane utakimbizwa na mashoka.

Hebu tuache, huyu tunaye liwe fundisho Kwa waovu wote kwamba ukiishi Kwa Ubaya utasemwa daima Kwa Mabaya yako na mema yako tutayasahau.

Imagine Profesa mzima Kabudi leo anatuambia eti yeye na Magufuli walitudanganya kuhusu pesa za Makinikia halafu unataka tukae kimya?
Mbona JK hamumsemi,chini ya utawala wake Mwandishi wa habari Channel ten Daud Mwangosi aliuwawa kinyama na Polisi bila kusahau Mabomu ya Mbagala yaliua watu kibao kwa uzembe wa utawala wa JK.Achilia mbali vijana waliofariki kwa madawa ya kulevya!
Au Aya kwenu ni mema?
 
Ingekuwa wewe ndiye uliyepigwa Risasi thealthini,Mtoto wako alipotezwa, Ndugu zako waliuawa(Baba au mama yako) ulibomolewa nyumba yako Morogoro Road bila kulipwa hata mia nazani ungekuwa unamlaani milele hata kama amekufa
Aya yote JK alifanya katika utawala wake mbona hamumsemi?
 
Anaandika, Robert Heriel

Sikuwa mshabiki wa Magufuli Kutokana na namna alivyokuwa anaongoza, sisemi Kuwa Magufuli hakuwa na mambo Mema aliyoyafanya, yapo mengi mazuri Sana hasa ya miundombinu, lakini pia yapo Mabaya ambayo aidha aliyafanya au kuyafumbia macho, ambayo ndio yalinifanya nimuone kama kiongozi asiyefaa.

Ninashangazwa na kile kinachoendelea hasa Kwa upande wa Upinzani kuendelea kumtaja taja MTU ambaye tayari anasiku nyingi ameshafariki.

Wabaya Waliohai wapo wengi, Kwa nini mhangaike na Watu waliokwisha Kufa wasio na chochote cha kuchangia katika Ulimwengu wa Waliohai? Wema Waliohai pia wapo wengi.

Hatuwezi kuongoza nchi Kwa kuangalia Wafu, na hatutataka nchi yetu iongozwe na watu wenye mawazo na Matendo ya Wafu.

Tunahitaji viongozi ambao wanaongoza nchi Kwa kuangalia Maisha ya kizazi kijacho kitaishije,
Nchi inaongozwa Kwa mahitaji yajayo sio mahitaji yaliyopita. Nchi inaongozwa Kwa maslahi ya Watu wa kesho sio Kwa maslahi ya Watu wa Jana na juzi waliokwisha Kufa.

Wanaoishi Wasiwe watumwa wa Wafu, Watu waliokwisha Kufa. Hivyo ndivyo taifa hili linapaswa kujengwa na kuongozwa. Kwa sababu tunaenda Mbele na sio Nyuma.

Sijui Fulani alikuwa Nani akasema nini, hiyo haina maana yoyote Kwa wakati au kizazi kijacho, kitakachoangaliwa ni manufaa ya kizazi kijacho.

Hata Mungu tunayemuabudu ni MUNGU aliyehai na Mungu wa Waliohai sio Mungu wa Wafu.

Wanasiasa mnaomtaja taja Magufuli Kwa ubaya mnayohaja ya kujitafakari, kama mnaagenda zenu za Siri Sawa lakini eleweni kuwa haitasaidia Jambo LOLOTE lile.

Acha nipumzike SASA.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Makanya, Same, Kilimanjaro.
Wewe ndo punguani kweli... kwani mbona tunasoma habari za kina Kinjekitile ngwale, chief mkwawa et al...hawafa? Vita vya dunia na kina Hitler, Mussolin tunawasoma na kuwajadili kwanini
Tuache kujifunza kutoka uovu wa huyu nduli relevant kabisa kwa kizazi hiki nawatu wajue katiba ni muhimu maana manduli bado wapo tena wengine wanajidai waumini wema.
Acha tumjadili na elimu isambae kama hupendi usisome habari zake lkn jua nifunzo kuuubwa tunalipata kwake. We pumzika kivyako
 
Kwahiyo umekubali hoja ya mleta mada kwamba mmeng'ang'ania kueleza maovu ya mtu aliyekufa kwa sababu ya hisia zenu tu ila hakuna faida kuzungumzia maovu ya mtu aliyekufa hayupo tena na kuacha kuzungumzia waovu waliyo hai ambao bado wanaendelea kutenda maovu?
Maovu mengine ya kuchonga eti alinyonga , alitesa na kuua ukiiliza aliua nani .anakuambia saane azory gwanda .kunzia kipindi cha nyerere hadi leo je amna aliyewahi kupotea huku nyumba kama akina jumbe
 
Aya yote JK alifanya katika utawala wake mbona hamumsemi?
Nchi hii nikama mbao inayotafunwa namchwa.Au chuma kinacholiwa na kutu huku tukishuhudia kwa macho Yetu Kama hatuoni kilichotokea au kinacho endelea nachojua tunawatawala wanao tawaliwa.
Dalali Mkuu February Ulisema tuonane
 
Back
Top Bottom