Kuendelea kushuka kwa Soko la hisa tangia 2015 inaashiria nini?

Kuendelea kushuka kwa Soko la hisa tangia 2015 inaashiria nini?

Mzalendo07

Member
Joined
Feb 24, 2014
Posts
71
Reaction score
120
Sijui kama niko sawa ninachokiona kwenye soko la hisa la Dar es salaam kwamba tangia mwaka 2015 soko hili limeenda likishukaa taratibu nikimaanisha bei za share za makumpuni karibia yote. Yaani share nyingi zilikuwa kwa kiwango cha juu mwaka 2014. Baada ya apo zimeenda zikiporomoka kila mwaka.

Mfano;
kampuniBei ya share moja mwaka 2014Bei ya share moja Mwaka 2021
swala1,900490
NMB4,7002,340
TBL18,00010,900
CRDB500205
TPCC4,5002,500

Hii inashiria nini kwenye uchumi unaosemwani wakati?

Kwa uwezo wangu mdogo nafikira ni kwamba watu wamekosa imani ya kuwekeza katika inchi, wewe jee?
 
Pia nadhan mfumo wa kununua hizo hisa sio rafiki na wenye mizinguko mingi..so waTz wengi Kama unavyojua..hawapendi/hatupendi kufuatilia fuatilia...plus kuzunguka mara njoo leo...njoo kesho..ndio ununue ama uuze hisa zako...kwa ufupi watu wa DsE teknolojia wameiweka pembeni
 
Back
Top Bottom