Kuendelea kuwavuruga vijana ni kujiharibia kwa CCM na Serikali yake

Kuendelea kuwavuruga vijana ni kujiharibia kwa CCM na Serikali yake

Matongee

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2023
Posts
1,056
Reaction score
2,729
Kwanza kabisa niseme wazi mimi ni mwanachama wa kawaida wa CCM nisiye na cheo chochote ndani ya chama. Wala siko kwenye kundi la kiongozi yeyote. Kwa hiyo huu uzi naandika bila kujali niko CCM. Nimeamua kwa makusudi kuwakumbusha viongozi wa serikali na chama kuacha kuendelea kuwavuruga vijana wa nchi hii ambayo kwa miaka yote wameonyesha utulivu na kuipenda nchi yao.

Kumekuwa na matamko mbalimbali ya kuwabeza vijana ila wanavumilia. Kwa mfano kiongozi anaposimama na kusema "vijana mjiajiri" huku akijua kabisa kuna sheria nyingi hasa za kodi zinazombana kijana kwenye mchakato wa kujiajiri ni sawa na tusi. Au kiongozi anaambiwa bei ya bando ni kubwa anaishia kujitetea kwa kutaja nchi ambazo zina bei ghali kuliko sisi... INATIA SANA HASIRA. Kimsingi mambo ni mengi mno ya kumvuruga kijana wa Tanzania.

Lakini hili la kufungia mitandao ya kijamii linaenda kupunguza kwa asilimia kubwa sana uvumilivu wa vijana wengi. Mitandao imekuwa chanzo cha ajira kwa vijana wengi mno. Binafsi mitandao ina mchango mkubwa kwenye kipato changu. Viongozi wa dini waliojitokeza na kusema mtandao wa X ufungiwe ni wapuuzi wasiojua lolote kuhusu mitandao. UVCCM nao ni kikundi tu cha watoto wa vigogo wasiojua maisha magumu mtaani yakoje kwenye maisha yao yote. Hichi kikundi hakifai kuwasemea vijana wa nchi hii. Kuanzia chipukizi hadi vijana wakubwa ndani ya UVCCM ni watoto wa mboga saba wasiojua shida. Mkoani kwetu Arusha tuna mwenyekiti wa UVCCM ambaye ni mtoto wa Meya wa jiji. UVCCM waendelee kula keki ya taifa kimyakimya bila kuwavuruga vijana wenzao walioamua kujitafutia riziki kihalali.
 
Back
Top Bottom