Kuendelea kuwekewa "mbinyo" na Jumuiya ya kimataifa, ndiyo njia pekee iliyobaki inayoweza kuiokoa nchi yetu katika anguko la kidemokrasia

Kuendelea kuwekewa "mbinyo" na Jumuiya ya kimataifa, ndiyo njia pekee iliyobaki inayoweza kuiokoa nchi yetu katika anguko la kidemokrasia

Hivi kipi bora !

Uumie juani unajitafutia ridhiki kwa jasho lako na baadaye ulie kivulini matunda ya jasho lako kwa kujitegemea bila masimango wala masharti yasiyotamkika kinywani au uumie ukiwa kivulini na kisha uanze kufurumishiwa mabomu utoke hapo kivulini na baadaye ulie juani matunda ya uzembe wako wa kushindwa kujitegemea huku ukisimangwa na kupewa masharti yasiyotamkika kinywani na kuyatekeleza kwa mijeredi kutoka kwa hao unaowaabudu!!

Yaani ninyi ihiii!!!
Matunda gani ambayo mtanzania anafaidi kwenye Nchi yake leo hii!!! Unazijua shule wanazoma watoto wa wanaoitwa wanyonge?!! Unajua gharama za matibabu za hawa wavuja jasho!! Unajua usumbufu wanaopata wakitaka kuchukua mafao yao mara wakistaafu?!! Unajua mazingira wanayofanyia kazi wavuja jasho wa nchi hii!! Mimi uwa nashangaa mtu anaeshabikia watawala wa nchi yetu!! Nchi ambayo haina vipaumbele!! Kila anaeingia anaingia na ujuaji wake!! Leo tunashangilia nchi maskini ina bunge lenye wabunge wa viti maalumu zaidi ya mia moja?!! Wakati kuna maelfu ya shule ambazo hazina madarasa, madawati, maabara, vitabu vya kiada na ziada!! Nyumba za walimu hakuna!!! Leo wabunge zaidi ya mia moja wa viti maalumu wanaenda kulipwa mamilioni ya shilingi kila mwezi, posho, usafiri na viinua mgongo vya kufuru!!! Halafu bado kuna watu wanajiita wazalendo wanashangilia?!!!
 
Ninesikia fununu watawala wetu watawekewa "mbinyo" mkubwa wao binafsi ya kutosafiri kwenda kwenye hizo nchi, kufunga account zao kwenye mabenki ya nchi hizo na kutoleta pesa za misaada kwa nchi yetu.

Je unaviona hivyo vikwazo ni vidogo?
Tuzidishe maombi, abanwe na asife ashuhudie maana halisi ya demokrasia.
 
Kura feki zingepitia wapi wakati tayari Lissu kashatuhakikishia hakuna kura feki wala figisu inaharibu utaratibu wa uchaguzi wa mwaka huu!? Na akaongeza kuwa dunia inafuatilia kila kitu kinachoendelea hapa nchini.

Ni wiki na ushee sasa uchaguzi umepita. Dunia imenyamaza wala haizungumzii habari za kura feki wa kura za mabegi! Ila ninyi tu mmejificha kwa uongo mliofundishwa na Antipasu ilikuficha aibu ya matokeo yenu ya uchaguzi. Mpone sasa muanze kufanya kazi acheni kujichechemesha!
Huoni aibu??
 
Ninesikia fununu watawala wetu watawekewa "mbinyo" mkubwa wao binafsi ya kutosafiri kwenda kwenye hizo nchi, kufunga account zao kwenye mabenki ya nchi hizo na kutoleta pesa za misaada kwa nchi yetu.

Je unaviona hivyo vikwazo ni vidogo?
Hivi kwa akili yako, kusafiri unakuona kwa maana? Angalikuwa JK sawa. Acha ndoto za alinacha
 
Halafu eti ndiye kinara wa kupambana na wanaofoji vyeti! Lakini pia wanasema ukimuona mtu msibani analia sana kuonyesha kuguswa na msiba ule badi ujue ndiye mchawi.
Kabisa mkuu, kuna kale kamsemo kake ka Maendeleo hayana chama, hata kenyewe tu alishindwa kukamaanisha kwa vitendo
 
#Uzalendo ni Kazi

".......
Nimesikia fununu kuwa wafadhili mbalimbali, ambao ndiyo huwa wanatufadhili kwa kiasi kinachokadiriwa cha shilingi trilioni 2 kila mwaka "wanakomalia" kuwa ni lazima sharti hilo litimizwe ndipo walete hayo mapesa yao.

Tumesikia kauli zilizotolewa na washirika mbalimbali wakiwemo Umoja wa mataifa, Ubalozi wa Matekani, Ubalozi wa Uingereza, Ubalozi wa Japan na Jumuiya ya nchi za Ulaya za kutotaka kuutambua uchaguzi huu uliopita kuwa haukuwa na viwango vya kuitwa ni uchaguzi uliokuwa Huru na Haki........"

Hiyo mada uliyoweka hapo ulikuwa unamaanisha au unatania?
Je, wewe ni Mtanzania au mkazi wa ughaibuni?
Nchi gani duaniani, viongozi wa kisiasa hutoa haki uliyoikamia nje ya mfumo wa mahakama na kamisheni za kisheria?
Je, ni wapi ulishuhudia au kusikia kwa uhakika HAKI hutolewa bila WAJIBU? [Once you obligationary heed the law it is evident rights and justice is apparent to prevail]

Kushabikia kauli tata kutoka mataifa makubwa dhidi ya nchi yako au jirani yako ni upofu wa moyo na Roho ambapo madhara yake huwezi amini kama yatakuadhibu mwenyewe...
Sasa inapotokea watu wenye power, wameiba kura na inapotokea viongozi Wa upinzani wanalalamika na kuwataka wafuasi wao waandamane kwa amani, ambapo inaruhusiwa kikatiba, Jeshi la Polisi linawafungulia kesi ya ugaidi!

Sasa hapo unakuwa na "option" gani ya mwisho, kama si hiyo ya kuomba nchi wahisani waongeze kibano cha vikwazo vya uchumi?
 
Nchi yetu iko katika mfumo wa vyama vingi kama inavyobainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 3(1)

Kwa Bahati mbaya sana, ingawa Katiba ya nchi inatamka hivyo, watawala wetu wanaonekana kabisa ni watu wasioutaka kabisa mfumo wa vyama vingi na wanatulazimisha watanzania wote turejee kwenye mfumo Wa Chama kimoja cha CCM.

Ushahidi wa wazi ni namna uchaguzi mkuu uliopita ulivyoendeshwa, hadi kutolewa matokeo ya mwisho, ambayo yamempa ushindi Wa asilimia zaidi ya 84, mgombea wake John Pombe Magufuli na kujizolea viti 262 vya ubunge kati ya viti 264!

Sasa kazi ipo katika uundwaji wa Kamati za Bunge, ambapo inatakiwa:-

1. Kamati za hesabu za serikali (PAC)
2. Kamati ya mashirika ya Umma (POAC)
3. Kamati ya serikali za mitaa (LAAC) ni "lazima" ziongozwe na wabunge wa upinzani.

Swali kubwa wanalojiuliza watawala je watawapataje wabunge hao wa upinzani wakati wnyewe ndiyo "waliouvuruga" uchaguzi huo hadi kutopatikana kabisa wabunge hao wa upinzani?

Nimesikia fununu kuwa wafadhili mbalimbali, ambao ndiyo huwa wanatufadhili kwa kiasi kinachokadiriwa cha shilingi trilioni 2 kila mwaka "wanakomalia" kuwa ni lazima sharti hilo litimizwe ndipo walete hayo mapesa yao.

Tumesikia kauli zilizotolewa na washirika mbalimbali wakiwemo Umoja wa mataifa, Ubalozi wa Marekani, Ubalozi wa Uingereza, Ubalozi wa Japan na Jumuiya ya nchi za Ulaya za kutotaka kuutambua uchaguzi huu uliopita kuwa haukuwa na viwango vya kuitwa ni uchaguzi uliokuwa Huru na Haki.

Je, nchi yetu ambayo imegeuka kuwa ombaomba, japo "inajimwambafai" kuwa inaweza kuwa "donor country" itaweza kumudu kuendesha shughuli zake bila kuwategemea hao wafadhili?

Swali muhimu ambalo tunapaswa tujiulize wananchi wote Wa nchi hii, je nchi yetu itakuwa imefuata njia iliyopitia Zimbabwe kwa kuyafanya maisha ya kila Mtanzania kuwa magumu mno kutokana na kiburi cha watawala wetu wa kutaka mfumo wa chama kimoja ambapo ni kinyume cha Katiba ya nchi?
Tumeyataka wenyewe.
 
Sasa inapotokea watu wenye power, wameiba kura na inapotokea viongozi Wa upinzani wanalalamika na kuwataka wafuasi wao waandamane kwa amani, ambapo inaruhusiwa kikatiba, Jeshi la Polisi linawafungulia kesi ya ugaidi!

Sasa hapo unakuwa na "option" gani ya mwisho, kama si hiyo ya kuomba nchi wahisani waongeze kibano cha vikwazo vya uchumi?
Mkuu,

Hata wakiweka kibano ambacho wewe na wenzio mnataka it shall not make any negative impact to the normal citizens alone, but including the diplomatic mission and other International organizations. In the current era it is pseudo belief to rely on for the developing countries self-reliance economy. Your kids and general pumpkin will be in protracted lamentation and agony from which implications what would be your beneficiary deal?
 
Bora wake mbinyo ili mwisho wa siku tupate mabadiliko. Japo tutaumia, ila bora tuumie kwa muda kuliko kuishi katika hali hii.
Mabadiliko hayalazimishwi wananchi ndio waamuzi, hata utunge uongo na uzushi wa aina yoyo hautafanikiwa na nchi itasonga mbele , Uchaguzi ni maamuzi ya wananchi na demokrasia sio lazima washinde wapinzani.
 
Haya hayana budi kupata mtu wa kututoa hapa tulipo ili tuweze kusimama kama nchi badala ya nchi kuwa mikononi kwa wachache! Bravo comredi
 
Vikwazo siyo njia hata siku moja, waambie viongozi wa upinzani wajipange vizuri kwa ajili ya 2025 kuliko kuota kuwa kuwa kuna shortcut ya kutoka mataifa ya nje.

Usidhani kuwa kweli mataifa ya nje yanamchukuia Magufuli kama unvyoamini; Lissu ni mhamiaji wa Ubelgiji, wala makelele yake pamoja na Masterdama wake yabadili chochote kuhusu uhusiano wa Tanzania na nchi za nje. Kuna watu kadhaa waliokuwa wanahusiana na biashara za madini ambazo zilivurugwa na magufuli wamekuwa washinikiza maseneta kadhaa Marekani walioko kwenye kamati ya mambo ya nje kuiwekea pressure serikali ya Tanzania, lakini mambo yote hubakia hapo tu, yaani matamko tu.
Mhhh mbombo ngafu
 
Huyo Mh Lissu alipokuwa Kawe alisema Jiwe/Tume wameandaa kura feki za Jiwe kiasi gani na Jiwe kapata kiasi gani kama unakumbuka?
To be honest, Jiwe hajawahi shinda uchaguzi wowote toka akiwa mbunge
Mkuu umemaliza kabisa...kwenye ubunge wakati huo jimbo la Biharamulo Jiwe alishindwa vibaya sana na Fares Kabuye...alikuja kushinda baada ya jimbo kugawanywa na kuwa Biharamulo Magharibi na Mashariki
 
Back
Top Bottom