Kuendelea kuwekewa "mbinyo" na Jumuiya ya kimataifa, ndiyo njia pekee iliyobaki inayoweza kuiokoa nchi yetu katika anguko la kidemokrasia

Matunda gani ambayo mtanzania anafaidi kwenye Nchi yake leo hii!!! Unazijua shule wanazoma watoto wa wanaoitwa wanyonge?!! Unajua gharama za matibabu za hawa wavuja jasho!! Unajua usumbufu wanaopata wakitaka kuchukua mafao yao mara wakistaafu?!! Unajua mazingira wanayofanyia kazi wavuja jasho wa nchi hii!! Mimi uwa nashangaa mtu anaeshabikia watawala wa nchi yetu!! Nchi ambayo haina vipaumbele!! Kila anaeingia anaingia na ujuaji wake!! Leo tunashangilia nchi maskini ina bunge lenye wabunge wa viti maalumu zaidi ya mia moja?!! Wakati kuna maelfu ya shule ambazo hazina madarasa, madawati, maabara, vitabu vya kiada na ziada!! Nyumba za walimu hakuna!!! Leo wabunge zaidi ya mia moja wa viti maalumu wanaenda kulipwa mamilioni ya shilingi kila mwezi, posho, usafiri na viinua mgongo vya kufuru!!! Halafu bado kuna watu wanajiita wazalendo wanashangilia?!!!
 
Ninesikia fununu watawala wetu watawekewa "mbinyo" mkubwa wao binafsi ya kutosafiri kwenda kwenye hizo nchi, kufunga account zao kwenye mabenki ya nchi hizo na kutoleta pesa za misaada kwa nchi yetu.

Je unaviona hivyo vikwazo ni vidogo?
Tuzidishe maombi, abanwe na asife ashuhudie maana halisi ya demokrasia.
 
Huoni aibu??
 
Ninesikia fununu watawala wetu watawekewa "mbinyo" mkubwa wao binafsi ya kutosafiri kwenda kwenye hizo nchi, kufunga account zao kwenye mabenki ya nchi hizo na kutoleta pesa za misaada kwa nchi yetu.

Je unaviona hivyo vikwazo ni vidogo?
Hivi kwa akili yako, kusafiri unakuona kwa maana? Angalikuwa JK sawa. Acha ndoto za alinacha
 
Halafu eti ndiye kinara wa kupambana na wanaofoji vyeti! Lakini pia wanasema ukimuona mtu msibani analia sana kuonyesha kuguswa na msiba ule badi ujue ndiye mchawi.
Kabisa mkuu, kuna kale kamsemo kake ka Maendeleo hayana chama, hata kenyewe tu alishindwa kukamaanisha kwa vitendo
 
Sasa inapotokea watu wenye power, wameiba kura na inapotokea viongozi Wa upinzani wanalalamika na kuwataka wafuasi wao waandamane kwa amani, ambapo inaruhusiwa kikatiba, Jeshi la Polisi linawafungulia kesi ya ugaidi!

Sasa hapo unakuwa na "option" gani ya mwisho, kama si hiyo ya kuomba nchi wahisani waongeze kibano cha vikwazo vya uchumi?
 
Tumeyataka wenyewe.
 
Mkuu,

Hata wakiweka kibano ambacho wewe na wenzio mnataka it shall not make any negative impact to the normal citizens alone, but including the diplomatic mission and other International organizations. In the current era it is pseudo belief to rely on for the developing countries self-reliance economy. Your kids and general pumpkin will be in protracted lamentation and agony from which implications what would be your beneficiary deal?
 
Bora wake mbinyo ili mwisho wa siku tupate mabadiliko. Japo tutaumia, ila bora tuumie kwa muda kuliko kuishi katika hali hii.
Mabadiliko hayalazimishwi wananchi ndio waamuzi, hata utunge uongo na uzushi wa aina yoyo hautafanikiwa na nchi itasonga mbele , Uchaguzi ni maamuzi ya wananchi na demokrasia sio lazima washinde wapinzani.
 
Haya hayana budi kupata mtu wa kututoa hapa tulipo ili tuweze kusimama kama nchi badala ya nchi kuwa mikononi kwa wachache! Bravo comredi
 
Mhhh mbombo ngafu
 
Huyo Mh Lissu alipokuwa Kawe alisema Jiwe/Tume wameandaa kura feki za Jiwe kiasi gani na Jiwe kapata kiasi gani kama unakumbuka?
To be honest, Jiwe hajawahi shinda uchaguzi wowote toka akiwa mbunge
Mkuu umemaliza kabisa...kwenye ubunge wakati huo jimbo la Biharamulo Jiwe alishindwa vibaya sana na Fares Kabuye...alikuja kushinda baada ya jimbo kugawanywa na kuwa Biharamulo Magharibi na Mashariki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…