May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Kiukweli inatamausha sana kusikia haya matukio ya mara kwa mara yakijirudia ya unyanyaswaji Watoto na Watu ambao ilitarajiwa kuaminiwa na Jamii.
Hainiingii akilini ni kwa vipi Taasisi yenye Wasomi kushindwa kuweka mifumo ya kudhibitiana wao kwa wao...hivi mnashindwa vipi kutambua Mwenendo wa Mwenzenu anayekengeuka mpaka anafikia kufanya madhara makubwa?.
Hamuoni hii mbali na kuitia doa taasisi bali pia inazusha maswali mengi kwaJamii kufikiri labda yanayofanyika ni sehemu ya shughuli za taasisi hiyo?.
Kama nyie mnashindwa kuwa Viongozi kimbilio, na wa kuaminiwa mnataka Jamii imkimbilie nani sasa?.
Ipo haja kwa Uongozi mzima wa Kanisa kutoka mbele na kujitakasa kwa Jamii kuwa ni kwa nini tuendelee kuwaamini ikiwa Jamii haipo salama mikononi kwao?. Hebu mje na mpango utakaoonesha njia mtakazozitumia kuwahakikishia Jamii usalama wao mikononi kwenu.
Haitoshi tu Kanisa kusema inajitenga na muovu au Mkosaji, ni vyema sasa kusikia uwajibikaji wa Kanisa zima na si kufikiri kwamba kwa kutengana naye tu inatosha kurudisha imani ya Jamii, tofauti na hapo ni sawa tu na kuleta ngonjera zile zile zilizokwishazoeleka.
Au mnataka tufikie mahali Jamii iwasuse?.