Kuendesha gari na sandles kwa traffic ni kosa?

Ni kosa, na lipo kisheria kabisa. Kwa sababu wakati unakanyaga brake/ clutch au accelerator mguu unaweza ukatoka kwenye sandali na kusababisha ajali.
Ni sawa na jingine kuendesha Gari ukiwa umevaa ushungi ni kosa ingawa wengi siku hizi hawajali
 
Kutokana na sheria zilizopo ni kosa kuendesha ukiwa umevaa Sandles. Nafikiri sheria hii ilitungwa kipindi ambacho hakukuwa na haya magari ya Automatic transmission. Kuvaa sandoz na kuendesha Automatic sioni kama ni tatizo kwa kuwa miguu yako inakuwa haipo busy kama ilivyo kwenye Manual transmission.
Nafikiri muda umefika baadhi ya sheria wazi-upgrade.
 
Hiyo ya kuongea na simu ungemwambia akusomee kipengele cha sheria kinachosema usiendeshe huku unaongea na simu, angefungua mafaili yote hakikuti. Inashauriwa usiendeshe huku unaongea na simu lakini hakuna sheria inayokataza. Ushauri unaweza kuukubali au kuukataa. Wakati sheria inatungwa simu hazikuwepo
 
Yap ni kosa kuendesha gari ukiwa umevaa kiatu cha wazi..

Sema watu huwaga wanaendesha kwa mazoea.

Siku trafk akikukamata huna cha kueza..

Ila watu wengi huwaga wanaendesha na sandels huku viatu vingine vikiwa pale karibu na pedal incase..
 
Hapo ni jinsi ya kuongea nae tu kwa sababu yeye hajui/Haoni kama unaendesha gari ukiwa UMEZIVAA Unaweza ukashuka ukamwambia ulikuwa ukiendesha peku peku alivyokusimamisha ndio ukavaa ili usimame
 
Makosa matatu kwa siku sio mchezo...usishangae wakakulizaa kwann umevaa shat
 
Ni kosa, hasa mikoani ndo wanafuatilia
 
Yani traffic wana changamoto kweli, mtu anakiri kutokujua sheria lakni anasema kabambikiwa makosa!! Rotten head!
 
Yes ni kosa. Ngoja nikutafitie kifungu!
 
Kuna sheria na kanuni za sheria, hilo la simu lipo ktk kanuni za sheria ya usalama barabarani
 
Kwa swali lako bila shaka hiyo leseni uliipata ukiwa Garage.

FYI sandal sio sehemu ya vazi rasmi sehemu yoyote. Wala sio vazi la kufanyia shughuli yoyote isipokuwa kuogea

Katika jiji LA Kigali uukionekana na Sandal mtaani unapata adhabu Kali.
Udikiteita huo. Hakuna athali za kuvaa sandal unatembea zako barabarani, ila kwenye gari kuna traffic safety implications wakati wa kuweka gear. Huwa sandal zinanasa kwenye clutch or accelerator pedals! !
 
Nyie Ndio Madereva mnaoleta ajali barabarani,yaani dereva mzima haujui kuendesha gari na mikubanzi ni kosa?
 
mkuu samahani ni hawa hapa kilimani boko magengeni????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…