Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Ukiwa ni mtumiaji wa simu za mkononi na mitandao ya kijamii ni vigumu kujilinda usitambulike wewe ni nani na upo wapi iwapo tu kuna taasisi ina shida na wewe kwa sababu yoyote ile.
Hata hivyo kufuatia mashambulio ya kigaidi ya Israel ya kielektronik huko Lebanon inabidi watu tujiongeze ili iwe ngumu kuripuliwa kutoka mbali kwa kutumia simu na laptop zetu.
Hutaweza kujilinda kirahisi usijulikane maeneo ulipo au unapopita katika safari yako,lakini angalau unaweza ukajilinda na uwezekano wa shambulizi hilo kwa kupendelea kutumia wifi .
Ushauri wa ziada ni kuwa Iwapo wewe ni mfanyabiashara mkubwa au ni mtu wa harakati fulani vile vile epuka kuagiza vifaa vya kielektronik kutoka nje kwa kutumia jina lako moja kwa moja.Kufanya hivyo maajenti kutoka nje au ndani ya nchi wanaweza wakaingilia kati katika mfumo wa usambazaji wa bidhaa yako na kuipandikiza kifaa cha kijasusi au kiripuzi bila wewe kujua.
Kwenye simu zetu za kijanja tunapopakua apps na kujsajili kwenye mitandao ya kijamii tunalazimika kukubali masharti ya matumizi ya apps hizo kwa tamaa tu iwe wepesi kumaliza kazi ya kujisajili bila kusoma kila kipengele cha masharti hayo.
Mara nyingi katika vipengele vinavyokuwemo ni kutoa fursa kwa wao kukupekua muda wowote wakitaka.Iwapo ni mtu una harakati za maana za kibiashara au jambo jengine lolote lile unakuwa umetoa ruhusa ya kupelelezwa na hatimae kuja kudhuriwa.