Kuepuka kulipuliwa kwa kutumia simu yako, tumia WiFi na BLUETOOTH

Ukiwa ni mtumiaji wa simu za mkononi na mitandao ya kijamii ni vigumu kujilinda usitambulike wewe ni nani na upo wapi iwapo tu kuna taasisi ina shida na wewe kwa sababu yoyote ile.

Hata hivyo kufuatia mashambulio ya kigaidi ya Israel ya kielektronik huko Lebanon inabidi watu tujiongeze ili iwe ngumu kuripuliwa kutoka mbali kwa kutumia simu na laptop zetu.

Hutaweza kujilinda kirahisi usijulikane maeneo ulipo au unapopita katika safari yako,lakini angalau unaweza ukajilinda na uwezekano wa shambulizi hilo kwa kupendelea kutumia wifi .

Ushauri wa ziada ni kuwa Iwapo wewe ni mfanyabiashara mkubwa au ni mtu wa harakati fulani vile vile epuka kuagiza vifaa vya kielektronik kutoka nje kwa kutumia jina lako moja kwa moja.Kufanya hivyo maajenti kutoka nje au ndani ya nchi wanaweza wakaingilia kati katika mfumo wa usambazaji wa bidhaa yako na kuipandikiza kifaa cha kijasusi au kiripuzi bila wewe kujua.

Kwenye simu zetu za kijanja tunapopakua apps na kujsajili kwenye mitandao ya kijamii tunalazimika kukubali masharti ya matumizi ya apps hizo kwa tamaa tu iwe wepesi kumaliza kazi ya kujisajili bila kusoma kila kipengele cha masharti hayo.

Mara nyingi katika vipengele vinavyokuwemo ni kutoa fursa kwa wao kukupekua muda wowote wakitaka.Iwapo ni mtu una harakati za maana za kibiashara au jambo jengine lolote lile unakuwa umetoa ruhusa ya kupelelezwa na hatimae kuja kudhuriwa.

We bwege kweli.... Unadhani unaelewa sana teknolojia kuliko Hezbollah au Irani? Nenda huko kafundishane ujinga na wenzio. Myahudi akiamua kukutaka anakula tu kama kawaida.
 
Uchawi ni tofauti na sayansi mkuu. Simu unaweza ukaifungua ukaona. Uchawi ni myth. Uchawi unapendwa TZ yote, kama dini vile. Hio mikoa ina vuma tu.
sio inavuma bali wengi wa watu wanaoishi hiyo mikoa wanapenda sana hayo mambo nikimaanisha ni asilimia 80 ya population
 
Ukiwa ni mtumiaji wa simu za mkononi na mitandao ya kijamii ni vigumu kujilinda usitambulike wewe ni nani na upo wapi iwapo tu kuna taasisi ina shida na wewe kwa sababu yoyote ile.

Hata hivyo kufuatia mashambulio ya kigaidi ya Israel ya kielektronik huko Lebanon inabidi watu tujiongeze ili iwe ngumu kuripuliwa kutoka mbali kwa kutumia simu na laptop zetu.

Hutaweza kujilinda kirahisi usijulikane maeneo ulipo au unapopita katika safari yako,lakini angalau unaweza ukajilinda na uwezekano wa shambulizi hilo kwa kupendelea kutumia wifi .

Ushauri wa ziada ni kuwa Iwapo wewe ni mfanyabiashara mkubwa au ni mtu wa harakati fulani vile vile epuka kuagiza vifaa vya kielektronik kutoka nje kwa kutumia jina lako moja kwa moja.Kufanya hivyo maajenti kutoka nje au ndani ya nchi wanaweza wakaingilia kati katika mfumo wa usambazaji wa bidhaa yako na kuipandikiza kifaa cha kijasusi au kiripuzi bila wewe kujua.

Kwenye simu zetu za kijanja tunapopakua apps na kujsajili kwenye mitandao ya kijamii tunalazimika kukubali masharti ya matumizi ya apps hizo kwa tamaa tu iwe wepesi kumaliza kazi ya kujisajili bila kusoma kila kipengele cha masharti hayo.

Mara nyingi katika vipengele vinavyokuwemo ni kutoa fursa kwa wao kukupekua muda wowote wakitaka.Iwapo ni mtu una harakati za maana za kibiashara au jambo jengine lolote lile unakuwa umetoa ruhusa ya kupelelezwa na hatimae kuja kudhuriwa.
Sidhan kama ni sawa maana hizo pagers zilionekana kuwa sala zaidi kwakuwa hazina mambo mengi zinapokea tu wala hazitumi chochote.
Kama dogo wa silk road alidakwa pamoja na kuwa anatumua public wifi ya library nadhani tena public wifi ni hatari zaidi.
 
Back
Top Bottom