Kuepuka laana, tuweke tozo angalau ya Tsh. 20 kwa kila chupa ya maji ya kunywa kuwanusuru wenzetu wenye mahitaji maalum

Kuepuka laana, tuweke tozo angalau ya Tsh. 20 kwa kila chupa ya maji ya kunywa kuwanusuru wenzetu wenye mahitaji maalum

Siungi mkono hoja, siyo kwa sababu siguswi na matatizo ya watu wengine! La hasha!! Tatizo ni kwa wale watao simamia hilo zoezi. Hao ndiyo watanufaika zaidi kuliko hao walemavu.

Na jambo hili halikubaliki hata kidogo. Halafu isitoshe hiyo tozo inaweza kusababisha viwanda vya maji kufa! Maana itafikia wakati baadhi ya watu wataanza kutembea na madumu ya maji wawapo katika mizunguko yao, ili kupunguza matumizi ya maji ya kununua.
Hapana mkuu, viwanda havitakufa, hilo ni ongezeko kidogo sana ambalo halitakiwa na athari kihivyo
 
Maji ya kunywa ya chupa sio bidhaa ya muhimu kihivyo kwa kuwa kuna mbadala kwa asiye na uwezo wa kuyanunua. Tumekunywa maji ya visima kwa muda mrefu kabla ya maji ya chupa na haijawahi kuwa ishu. Uzuri wa maji ni bidhaa inayogusa watu wote, wacha Mungu na wahuni.

Wewe unataka jukumu hili tuwaachie walevi peke yao?
Hivi ukiwa kkoo maji ya kisima utayatoa wapi au wewe uko mkoa gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakate huko kwa Wabunge na mawazir sisi wanyonge mtuache jamani yaan sijui mnatuonaje mtoa Mada hujitambui katen kwenye sigara na Pombe zenu bia na Konyagi dah!
Begging economy aiwezi kuisha duniani hata utumie policy gan!??
Mkuu Tushome wewe hutaki kusaidia wasiojiweza unataka walevi tu ndio wasaidie? Kumbe wakati fulani tunawalaumu walevi bure tu ila ndio wenye utu na moyo wa ukarimu
 
Begging economy aiwezi kuisha duniani hata utumie policy gan!??
Mkuu, ishu sio kumaliza lakini angalau kupunguza machungu kwa watu wenye uhitaji maalum. Fikiria hao watoto wasio na walezi mfano wawe ni wanao halafu wewe haupo, unawaona lakini huwezi kufanya kitu na kila mtu kawatosa!
 
We umesaidia watu wangapi kuwatoa kwenye extreme poverty?
Ndio maana nasema mtu mmoja mmoja hata tukisaidia haina manufaa sana maana tatizo ni kubwa hiyo tunahitaji policy intervention na ndio ninayoshauri hapo juu.
 
Ujinga wa tozo ni kwamba haizalishi kitu kipya.

Tufikirie mipango ya kuongeza uzalishaji, si ya kugawa vipandepande kile kilichopo.

Fikiria hao watu wana nguvukazi gani na inawezaje kutumika katika uzalishaji wakajisaidia wao na kuisaidia jamii.

Usifikirie tozo.
 
Hawana uwezo/ nguvu kazi kabisa. Fikiria mtu mfano hana mikono na ametelekezwa na ndugu atafanyaje? Kumbuka kuna watu wazima watu afya, wana na degreee ila wasipoajiriwa inabidi waombe hifadhi kwa shemeji, sasa hawa wao watafanya nini bila kusaidiwa?? Au wengine ni watoto yatima na wametelekezwa na jamii wanalala chini ya madaraja.
 
Unaandika hawana mikono, lakini picha zinaonesha wamekinga mikono kuomba.
 
The solution ya kuwasaidia watu walemavu nikupunguza Mishahara ya wanasiasa kitakachopatina kinatosha kuwa-feed walemavu nchi nzima sio busara kumnyonya Mtu ambaye Hana stable economic Over.🙏✍️
 
Unaandika hawana mikono, lakini picha zinaonesha wamekinga mikono kuomba.
Ni mfano tu mkuu, yaani ishu ni nyingi. Hilo la mikono ni mfano. Picha yenyewe ni mfano. Ila suala la uwepo wa watu wa makundi maalum ambao hawawezi kujikimu au kusimama wenyewe kwa sababu ya majanga ya kimaumbile ni suala halisi na la wazi sana.

Kama tunadhani sisi ambao ni wazima kabisa, serikali inapaswa ituhurumie na kutusaidia, kwa nini sisi tusidhani pia kuwa tunatakiwa kuwasaidia hawa ambao wako kwenye makundi maalum?
 
The solution ya kuwasaidia watu walemavu nikupunguza Mishahara ya wanasiasa kitakachopatina kinatosha kuwa-feed walemavu nchi nzima sio busara kumnyonya Mtu ambaye Hana stable economic Over.🙏✍️
Sio kumnyonya mtu mkuu. Ni busara ya kawaida tu. Kukatwa kodi kwa wenye nacho na kuwasaidia wasio nacho ni busara ya kawaida inaitwa distributive justice. Ndio maana matajiri hulipa kodi kubwa ambayo ina subsdize maisha ya masikini.
 
Back
Top Bottom