DR HAYA LAND
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 23,928
- 63,499
Sasa kila anayekunywa maji ana pesa au Mkuu haupo Daslama labda hivi akili yako inasense kweli?Sio kumnyonya mtu mkuu. Ni busara ya kawaida tu. Kukatwa kodi kwa wenye nacho na kuwasaidia wasio nacho ni busara ya kawaida inaitwa distributive justice. Ndio maana matajiri hulipa kodi kubwa ambayo ina subsdize maisha ya masikini.
Hapana mkuu, kutoa sio kuwa na pesa bali ni moyo halafu sera ikishapita kila mtu anachangia tu mkuu. Yaani unachotaka ni kukwepa kumchangia mlemavu au yatima Tsh.20 kweli? Kama unadhani unapaswa kuhurumiwa kwa nini usihurumie wenye wakati mkuu kukuzidi?Sasa kila anayekunywa maji ana pesa au Mkuu haupo Daslama labda hivi akili yako inasense kweli?
Safi sana bro, umefikiria mara mbili [tena ni mara tatu katika bandiko lako] ni hatua nzuri sana.Kwa nini? fikiria wewe ndio ungezaliwa mlemavu, huna mikono wala miguu, halafu watu wazima wakatae kutoa angalau kodi ya Tsh 20 kutoka kwenye bidhaa isiyo ya lazima ili na wewe uweze kula na kulala ndani ya nyumba, ungewatafsirije binadamu?
Ukumbuke, wewe ni mzima lakini mafuta tu yalivyopanda bei ukataka serikali iingilie iweke ruzuku ili ununue huduma kwa urahisi, vipi wenzako wasiojiweza na hawana sauti?
Safi sana bro, umefikiria mara mbili [tena ni mara tatu katika bandiko lako] ni hatua nzuri sana.Kwa nini? fikiria wewe ndio ungezaliwa mlemavu, huna mikono wala miguu, halafu watu wazima wakatae kutoa angalau kodi ya Tsh 20 kutoka kwenye bidhaa isiyo ya lazima ili na wewe uweze kula na kulala ndani ya nyumba, ungewatafsirije binadamu?
Ukumbuke, wewe ni mzima lakini mafuta tu yalivyopanda bei ukataka serikali iingilie iweke ruzuku ili ununue huduma kwa urahisi, vipi wenzako wasiojiweza na hawana sauti?
Suluhisho zuri ni kuongeza uzalishaji, fanya mpango uongeze uzalishaji halafu hata kama unataka kuwasaidia utoe kwenye uzalishaji ulioongezeka.Ni mfano tu mkuu, yaani ishu ni nyingi. Hilo la mikono ni mfano. Picha yenyewe ni mfano. Ila suala la uwepo wa watu wa makundi maalum ambao hawawezi kujikimu au kusimama wenyewe kwa sababu ya majanga ya kimaumbile ni suala halisi na la wazi sana.
Kama tunadhani sisi ambao ni wazima kabisa, serikali inapaswa ituhurumie na kutusaidia, kwa nini sisi tusidhani pia kuwa tunatakiwa kuwasaidia hawa ambao wako kwenye makundi maalum?
Shukuran sana mkuu Uhakika Bro yaani kuna vitu ili uvielewe, inabidi ujiweke kwenye upande wa mhanga, inaitwa "empathy" vinginevyo kuna vitu tunaweza kuvichukulia kimzaha lakini ni balaa tupu. Kuna watu wanateseka sana bro.Safi sana bro, umefikiria mara mbili [tena ni mara tatu katika bandiko lako] ni hatua nzuri sana.
Upendo utawale.
Tena pale ulipochagiza wafundishwe skills mbalimbali, asee umethibitisha utimamu wa fikara zako. Endelea na moyo huohuo
Mkuu ni kweli kuna tatizo la baadhi ya watu kula hela za wengine kwa dhuluma, ila hata kwenye taasisi za dini kuna wanaoiba sadaka, wanandugu wanakula mali za yatima ni.k lakini hii haiwezi kuwa sababu ya kutokuwa na mfumo wa kisera wa kuwasaidia watu walio kwenye makundi maalum. Suala tujadili tufanyeje ili tupunguze upigaji.Wengi wanaolipinga bandiko, hawapingi wazo kama wazo. Bali wanapinga uaminifu wa mifumo ya tozo kama itaenda kwa haki.
So tatizo sio hoja uliyotoa. La. Kwa kiasi kikubwa tatizo ni imani 'trust'. Hawaamini mifumo baas.
Kwa wanaojielewa wanajua haya ni madhara ya ukoloni na utumwa, hivyo kubaki bila trust jua moja kwa moja sio takwa lako la ndani bali ni matokeo ya wewe kukubali madhara ya utumwa. Be a stronger man na ishinde hiyo hali, jaribu na unaweza ukaweza
Siku hizi umefanya nini unaandika utopia namna hii? Ni kutafuta ulaji au uko kwenye ulaji mpaka umevimbiwa? Wewe unadhani sh 20 kwa raia wa kawaida ni kitu kidogo? Ukiwa nazo wewe unadhani kila mtu naye anazo? Badala ya kusema serikali ipunguze matumizi ya anasa kama kusafiria bussiness class, kununua magari ya fahari, safari zisizo na lazima, idadi ya wabunge kubwa, kuwa na utitiri wa viongozi ngazi ya wilaya nk wewe unataka kukamua tena wananchi? Kweli waafrika tuna roho za kishetani zilizojaa ubinafsi!unajua misaada ambayo nchi zilizoendelea hutoa kwa nchi maskini ni sehemu ya kodi ya raia wa nchi husika ambazo wanatozwa na serikali zao ili kusaidia maskini kwenye nchi nyingine?
Kwenye jamii yetu kuna watu wenye mahitaji maalum ikiwemo walemavu, Watoto mayatima, waliotelekezwa n.k ambapo watu hawa hawawezi kujinusuru wenyewe mpaka wasaidiwe.
Kwa sasa watu hawa huomba omba mtaani wakitegemea kupewa 200 kotoka kwa raia wachache wenye huruma, wengine wakiomba wakikosa huamua kugeuaka kuwa wezi.
Badala ya kuacha hali hii iwe itakavyokuwa, Ni muhimu tuweke Tozo angalau ya Tsh. 20 kwa Kila chupa ya maji ya kunywa, Fedha itakayopatika itumike kujenga safe house ambazo zina kila huduma (bure) kwa ajili ya makundi haya maalum huku wakifundishwa fani mbalimbali, wanaoweza kujitegemea wanaachwa wanaanza kujitegemea, wanaoshindwa wanalelewa hadi mwisho wa Maisha yao.
Watu hawa hawajapenda kuwa walemavu n.k hivyo ni sahihi na ubinadamu kutumia kodi ya raia wazima kusaidia wenye uhitaji maalum. Hili ni jambo muhimu kiuchumi, Kijamii, Kiusalama na ki ubinadamu. Tunganeni kupigania jambo hili kwa kuwa ni muhumu kwa Taifa na ustawi wa mwanadamu.
Mkuu, kuna aina ya vitu vinapaswa kuwa vya kisera, sio kujitolea. Ukisema kujitolea watajitolea wachache. Fikiria tungesema watu wajitolee kuchangie kujenga shule kwa hiari.Suluhisho zuri ni kuongeza uzalishaji, fanya mpango uongeze uzalishaji halafu hata kama unataka kuwasaidia utoe kwenye uzalishaji ulioongezeka.
Si kuongeza tozo kwa watu waliopigika tayari.
Kuna watu hawawezi kufanya kazi, hawa hawahitaji mikopo, wanahitaji msaada maalum.Mbona hela nyingi sana wakati tatizo lenyewe linaweza kumalizwa kila halmashauri, fikiria kila %10 ya mapato ya halmashauri upelekwa kwenye mikopo ya vikundi mbalimbali je hiyo pesa upelekwa kweli? Kama inapelekwa basi faida/riba yake ifanye kazi hiyo.
Soma vizuri coment yangu, hakuna nilikosema wapewe mikopoKuna watu hawawezi kufanya kazi, hawa hawahitaji mikopo, wanahitaji msaada maalum.
Kumbuka wazungu wanatupa misaada na tunashangilia wakati sisi ni watu wazima na tuna afya nzuri, fikiria walemavu na watoto waliotelekezwa?
Kwani wapi nimesema uongezaji uzalishaji hauwezi kuwa wa kisera?Mkuu, kuna aina ya vitu vinapaswa kuwa vya kisera, sio kujitolea. Ukisema kujitolea watajitolea wachache. Fikiria tungesema watu wajitolee kuchangie kujenga shule kwa hiari.
Saidia wewe kama wewe kuepuka hiyo laana!Ndio maana nasema mtu mmoja mmoja hata tukisaidia haina manufaa sana maana tatizo ni kubwa hiyo tunahitaji policy intervention na ndio ninayoshauri hapo juu.
Mkuu Kiranga la kuongeza uzalishaji na kupunguza ukosefu wa ajira nakubaliana na wewe kabisa. Na nilishaleta mjadala hapa namna ya kupunguza ukosefu wa ajira na kuongeza uzalishaji kwa lufanya reformations kwenye mfumo wa elimu na mfumo wa mikopo miongoni mwa hatua nyinginezo.Kwani wapi nimesema uongezaji uzalishaji hauwezi kuwa wa kisera?
Kiujumla Tanzania hatuna utamaduni wa kutumia nguvukazi vizuri, kuna unemployment kubwa, kuna underemployment kubwa, hata kwa walio na afya nzuri.Hawa Wamachinga wote wana underproduce.
Sasa hao mnaoita vilema ni wachache sana hawawezi kufanya kazi kabisa. Wengi wanaweza kufanya shughuli za uzalishaji.
Tatizo hatujajipanga, tnapenda majibu rahisi kama tozo.
Kuanzia baadhi ya wananchi, wabunge mpaka serikali.
Ukiongeza tozo bila kuongeza uzalishaji mtagawana umasikini tu.
Mkuu kuna suala la maono ya viongozi lakini pia mtizamo wa wananchi walio wengi.Viongozi wangekuwa na maono haya mambo yasingekuwepo.