Kufa Kufaana, Hata Msiba Wa Kanumba!

Kufa Kufaana, Hata Msiba Wa Kanumba!

Huu udongo unatafuna watu wazuri.

Rip kanumba. Nakumbuka picha zake ziliuzwa hadi kijijini kwetu picha moja 2000.
 
Wanabodi,
Japo binafsi yangu sii mpenzi wa bongo movies ila huu msiba wa Kanumba umeigusa familia yangu haswa wife na girls wetu watatu ni wapenzi wakubwa wa bongo movies.

Baada ya wife kunisindikiza msiba wa Regia mpaka kwenye mazishi Ifakara leo ni zamu yangu kumkampany kwenye msiba wa Kanumba hivi ninavyoandika niko mitaa ya Sinza eneo la msiba.

Cha kwanza barabara ya Tandale kipande cha mbele ya nyumba ya Kanumba kimefungwa, barabara nzima imeshehenezwa mahema yenye viti watu wamejaa mpaka wamesimama!.

Parking za magari ni kuanzia Kijiweni zikitapakaa mpaka Lion. Kutokana na wingi wa watu, idadi kubwa ya waombolezaji wamejikalia baa za jirani wakijipooza na machungu ya msiba!.

Baa zote zimefurika, wahudumu wanalakamika tangu ile juzi ni hakuna kulala, watu wanakunywa usiku kucha na asubuhi ndio kwanza wanaongezeka mpaka wanashangaa hivi hawa waombolezaji wa msiba huu hawana kwao, au ndio wamehamia Sinza!.

Hoteli zote, lodge zote na guest zote za maeneo haya ziko fully booked na waombolezaji toka ugenini japo hawajaja na mabegi ya nguo!.

Japo ni tukio la msiba, wengi wa wateja ni waombolezaji, kama kawaida ya masuper stars ni full ubishoo wala nyuso za huzuni hazionekani!. Kitu kizuri kuhusu hizi baa zote za jirani, zina make ile mbaya!. Mpaka wanatamani mazishi yangesogezwa mbele kidogo mpaka angalau Jumamosi ijayo!.

Ama kweli kufa kufaana, na jinsi mastaa wa bongo walivyojazana Sinza, wenye baa za hapa wana death wish baada ya Kanumba na mwingine afuatie na mwingine na mwingine alimradi wao waendelee kuzi make!.

RIP Kanumba!.
Leo ni imetimia miaka 10, toka kifo cha nyota huyu wa Bongo Movies, Steven Kanumba, na mpaka Leo, sio tuu pengo lake halijazibika, bali hajapatikana star mwingine yoyote wa kuvaa viatu vyake vikamfiti.

RIP Steven Kanumba, tutakukumbuka milele!.
Paskali
 
Back
Top Bottom