Kufahamu mambo yako hapa: Ramli ya kutizama mambo unayotaka

yani mpaka leo bado kuna watu wanapigwa hela kijinga namna hii kwa kudanganywa danganywa tu kwa vitu vya kufikirika.waafrika tuache upuuzi wa kupenda shortcut za maisha ,hakuna cha nyota wala jini ,maisha ni juhudi na maarifa ,jiulize huyo jamaa yeye ukoo wake wote wameshafanikiwa mpaka aje huku mitandaoni eti akufungulie milango kupitia sijui nyota,buku mbili unaiona ndogo ila akizikusanya kwa wajinga wengi ni pesa nyingi .fanyeni kazi tafuteni pesa acheni mawazo ya kishirikina mtaibiwa kila siku na watapeli wanaojifanya wanajua kutatua shida zenu
 
Well kuna kitu hukielewi kuhusu nguvu ya jina la mtu hata awe na majina mia lipo moja ambalo ni lake na sahihi zaidi hivyo katika kutoa majina yake kuna mizani hupimwa ikiwa ni pamoja na muonekano wake wa sura na viganja vyake huamua ni nyota gani na mengine mengi unayotizama hadi kuhukumu nyota ya mtu ni ipi
 
Japo sio lengo la thread lakini kwa mtizamo tu inaonyesha hujielewi tafuta mtu wa imani yako akufanyie maombi maana unapoelekea sio sawa. Kwa maana ungekuwa na akili nzuri si ungeandika ulichoandika.
Pole mwenyezi Mungu atakuongoa.

Rakims
 
Hetu Tufahamishe Kuhusu Jini Huyu, Anayeitwa Karini.... Anakaa Sehemu Katika mwili, na Je nia yake kuwa karibu na binadamu nini?, na Je naweza kumtuma Kazi zangu afanye.??
 
Hetu Tufahamishe Kuhusu Jini Huyu, Anayeitwa Karini.... Anakaa Sehemu Katika mwili, na Je nia yake kuwa karibu na binadamu nini?, na Je naweza kumtuma Kazi zangu afanye.??
Nimeelezea kila kitu kwenye website yangu unaweza kutembelea


Rakims
 
kwanini useme lipo moja una maana hujui kama kuna watu wana majina zaidi ya moja na yote yanatumika ipasavyo,nikiamua kumita mwanangu lionel messi inamaana ndio utatumia kupata hiyo nyota yake.hizi ishu ni tricks tu za kijanja
 
Japo sio lengo la thread lakini kwa mtizamo tu inaonyesha hujielewi tafuta mtu wa imani yako akufanyie maombi maana unapoelekea sio sawa. Kwa maana ungekuwa na akili nzuri si ungeandika ulichoandika.
Pole mwenyezi Mungu atakuongoa.

Rakims
ni upuuzi kutafuta mtu akufanyie maombi,Kama unajua mwenyezi Mungu ataniongoa sasa huyo mtu nimtafute wa kazi gani,mbona watu mnapenda kujifanya nyie ndio madalali au mtu kati kwa Mungu yani ndio mpo karibu nae watu wengine waje kwenu ili mwakonect kwa Mungu the muwachukulie vihela vyao.kila mtu ana nguvu yake na Munguyupo kwa wote ,fanyeni kazi tuache haya mambo ya kishirikina .
 
Kila mtu ana akili zake timamu na hupiga hesabu na kujua nini afanye nini aache nyie wenye kuwa na username mbili mbili hamna tofauti na wale wenye jinsia mbili huku mwema huku muovu hivyo huwa sibishani sana na watu waliooza kifikra.

Jaribu kutizama ni makala gani zinakufaa zaidi kisha nenda huko kateketee kuliko kuleta uongo na kujifanya mwema kwenye threads nyingine.
Wapo watu waliuwa mitume kwa kujiona wanaakili sana kuliko watu wengine unadhani watu hao walikuwa ni watoto wa shetani?? Ni binadamu kama wewe na mimi hivyo historia hujirudia kila siku.

Aliepewa elimu kapewa tu, wewe hata uwe na choyo vipi huwezi kufuta elimu yake na baraka yake.

Rakims
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…