Jumanne Mwita
JF-Expert Member
- Nov 18, 2014
- 530
- 1,446
Nimekaa nikatafakari sana haya maisha kila biashara nikipanga niifanye naona mtaji haukidhi yaani hautoshi. Naona dhahiri kabisa naenda kuanguka maana life mtaani ndio usiseme hakuna hela na mzunguko umekuwa mdogo sana kwa baadhi ya watu wanaofanya biashara.
Niliwaza nifanye biashara ya Hardware kuja kuuliza mtaji wa kuanza nao nikaona labda barbershop napo kuja kuambiwa mtaji nikasema labda ninunue mazao napo muda wa kusubili besa ikae stoo mwishoe bei ishuke uambulie kuuza kwa hasara yaani kiujumla biashara kwa sasa ni ngumu hasa kama uwe unataka kuanza au unatafuta biashara ya kukulipa hapo hutaweza kama unahela ya mawazo kama mimi.
Kitu nilichojifunza hasa watu wanaofanya biashara wengi wanafanya biashara kama mali kauli unakuta mtu mtaji wake ni 100m mtaji mwingine ni malikauli kama 250m+ hii inamsadia kuzungusha hapa na pale na kumfanya aweze kurudisha kidogokidogo yaani ni kama anamsaidia kumuuzia yule mwenye mtaji wa 250m+ baada ya hapo ataagiza na kupewa mzigo mwingine yaani anafanya kupokea mzigo bila kumalizia malipo baadae atakapo agiza ndio analipa ya nyuma anaendelea muda huo analetewa mwingine hii inawasaidia wengi wafanyabiashara wengi tunaona wanamitaji mikubwa kumbe wanawafanyia wengine kinachombeba ni jina na wateja ambao amejikusanyia hapo anakuwa na uhakika wa kuchukua mzigo na kuuza na kurejesha na kuomba mzigo tena
Mwaka 2019 hadi 2020 nilikuwa Kasulu katika heka heka za utafutaji nilijenga mazoea na jamaa mmoja mfanya biashara aliniamini sana mpaka kufikia kunipa siri hii hata yeye alisema siyo kila mtu namwambia hili ila sababu tumeshibana ngoja ni kwambie.
Aliniambia mengi ila kuna hili aliniambia ukweli kuhusu hicho nilichoelezea hapo juu. Akasema Jumanne unajua sii wote tunamitaji humu mjini sema tunawatu ambao tunafahamiana nao kule mzigo unapozalishwa hivyo wao wanatuamini na kututumia mzigo mimi nalipia usafiri tu. Ila mzigo natumiwa bure, nikiuza narudisha hela yake ile faida naongezea kwenye mtaji ukiisha tena namwambia nashushiwa hapa semi full mkoko napakua mzigo mwingine naweka stoo mtu akija hapa anajua mzigo wote wangu na sifa ananimwagia kumbe haujui nachofanya kwenye biashara.
Sasa wewe mwenzangu na mimi unatanga tanga na mtaji wa million 6 sijui 3 unategemea nani atakuamini akupe mali baadae urejeshe akupe tena mzigo. Hilo ni gumu kama huna connection na tajiri mwenye mtaji, hii nimeitafakali sana leo kila nikigusa namna ya kutoka naona kila njia ngumu yaani life kwa wengine sisi tulikuja kushuhudia ulimwengu baadae tufe tuache lawama hakuna namna maana huna wa kusema hapa nakwama ngoja nikamuone flani hamna ni wewe na roho yako tu.
Ukirudi nyuma wengine wazazi wanategemea utoboe waponee hapo wao walipambana lakini riziki ikawa siyo bahati kwao hivyo tegemeo kubwa limebakia kwa watoto wao na wao wajaribu, na sisi tunajaribu lakini wapi!
Kama unarafiki au ndugu ambae ukimueleza shida yako au changamoto yeyote mnaibeba kama wote basi shukuru sana na ombea M/Mungu asije kutenganisha ukaribu huo au undugu wenu.